MwanaKJJ Ijumaa: Kutoka UKAWA kuelekea UKUTIUKUTI?

CCM wanaipractice katiba ndani ya chama chao? Tangu lini? Sasa wameanza na kutoiheshimu na katiba ya nchi. Watangaze basi rasmi kwamba Tanzania haina katiba Rais ataamua atakavyo na hakuna mwenye haki ya kuzuia maamuzi ya Rais na pia vyama vya uupinzani vimefutwa ili turudi enzi za ujima za chama kimoja.

Vinginevyo huu unafiki wa nchi yenye kufuata utawala wa sheria kupitia katiba ya nchi na nchi yenye mfumo wa vyama vingi wakati kuna dikteta ambaye haheshimu yote haya lazima unafiki huu upingwe na wote wanaoitakia nchi yetu mema.
Mkuu hapo ndipo mnapokosea. Mnahalalisha kosa kwa kosa et kwa kuwa ccm wamefanya vile nasi tutafanya vivyo hivyo. Hapo ndipo mnapokosea. Walah nakuambia iyo sept mosi mtapata mandezi tuu .Tena ikiwa jumatatu ndo hamtopata watu. Andaeni nguvu na mfungue moyo ili watakapopitisha upupu msikimbie. Yangu macho . Siku iyo ntapiga mision town zangu kama kawa yaan. Maana siasa n utapeli tuu. Leo ukiambiwa hii nyeusi kesho utaambiwa no hiyo n nyeupe siyo nyeusi. Aliekuwa anaiita nyeupe ataanza kusema no hiyo nyeusi. Just like vicious cycle of poverty
 
....hakika wewe ndie mwenye maono!, hawa wengine wote mbayuwayu wasiojielewa, eti kisa mtu fulani alitoka ccm akaenda Chadema, basi nae akaamua kutoka Chadema na kurudi ccm!, haya ni madhara ya akili iliyotawaliwa na njaa!

Juzi tu hapa katoka kusema, Magufuli akinipa cheo sitakataa!, huyu mtu ni wakumhurumia tu, anyway nilishasikia mahala mtu akizeeka akili yake inarudi kuwa ya mtoto!
..unapomquote mtu kama Nguruvi anaejengaga hoja zake objectively,jaribu angalau kupunguza 'mihemko' na kutoa kejeli za rejareja ili angalau ufanane nae!
..ndio wenzio tunavyojifunza kukomaa kwenye uchambuzi!
 
Usikurupuke wewe! lini nimesema kwamba CHADEMA haikosei? Narudia tena na kwa taarifa yako nimeshaikosoa CHADEMA humu si mara moja au mbili. Nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi na pia ina katiba ambayo kuna vipengele vinavyohusu vyama vingi na kuvipa haki ya kuendesha shughuli zao mbali mbali ikiwemo uwezo wa kujadili lolote Bungeni kuhusu mustakabali wa nchi na pia kufanya shughuli zake za kukutana na Watanzania kila kona nchini bila kuingiliwa na yeyote yule ndani ya Serikali au CCM.

Udikteta nchini lazima upigwe vita kwa kila hali. Tumeona nchi zenye madikteta ambazo mwisho wake siku zote haukuwa mzuri. Tuna katiba ya nchi lazima iheshimiwe, tuna vyama vya upinzani lazima viheshimiwe na Viongozi na Wabunge wake wote wapewe haki wanazostahili ndani ya katiba ikiwemo kufanya shughuli mbali mbali bila kudhbitiwa na yeyote yule.
Anyway ...unajua nakuheshimu Babu ...pia najua bado unaamini lakini kama hupati ugali hapo ufipa ipo siku utajua hawapo serious. Hizi drama zinachosha in short ....tunahitaji damu mpya na mbinu mpya za kuikomboa Tanzania ...JPM anajitahidi sana ....tumuunge mkono na kumkosoa fairly badala ya kufanya propaganda kwenye kila issue....haiwasaidii Watanzania zaidi ya tamaa ya kwenda ikulu.
 
Mwanakijiji kama kawaida yako umenena!

Hivi hawa UKUTA ndio waliokuwa wanatwambia wanatetea Mtanzania anayekula mlo mmoja kama kiboko!? 'Demokrasia' tangu lini ikaliwa, mwenye njaa akashiba! Demokrasia ya kweli inahusiana sana na matakwa na mahitaji ya wengi. Tuwaombe hawa ndugu zetu wakumbuke kwamba demokrasia pia ina maana ya "wengi wape". Watanzania walio wengi a.k.a maskini wanyonge, wanacholilia usiku na mchana ni maendeleo yao. Angalau nao wale milo mitatu kama wanavyokula hao walioshiba ambao wanawashawishi wenye njaa waandamane! Tunawaomba viongozi wa vyama vya upinzani wawe na huruma na wananchi.

Hawa wenzetu wanachopigania ni nini hasa? Kwao wao madaraka na kutaka kushika dola ni muhimu zaidi kuliko mustakabali wa wananchi na taifa kwa ujumla? Inavyoonekana wanataka zaidi kuvutia huruma za 'wawekezaji' wa demokrasia kutoka nje kuliko wananchi wanaolilia maendeleo. Hizi siasa zenu za kuwa Copy Cats wa siasa za nje hazitufai nchini mwetu.

Viongozi wa CHADEMA tunaomba mmwache Rais na serikali yake wawatumikie wananchi kwa miaka mitano waliyopewa na wananchi. Subirini 2020 mtuambie Rais Magufuli na serikali yake wamekosea wapi na ninyi mtatufanyia mini mkichaguliwa. Kwa sasa maandamano yenu hayamsaidii chochote mwananchi anayehitaji MAENDELEO!
Maendeleo my foots hakuna endelea lolote mambo hayafanyiki kwa utaratibu leo dom kesho sukari majipu.... Bila blah blah mtaanza kazi Hasa lini?! Maana naona hata hamjui mlipotoka mlipo wala mtapoenda 10yrs tutakuwa hapahapa
 
Magufuli amechaguliwa na kuungwa mkono na watu ambao walikuwa wanatamani mabadiliko ya kweli. Atahukumiwa na wananchi hao ifikapo 2020.

CohzXvNUkAAPtu1.jpg
 
ukutiukuti-990x660.jpg

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna hatari kwamba endapo CHADEMA haitajiangalia vizuri katika hali yake ya kupoteza mwelekeo ambao tunaiona sasa hivi inaweza uko mbeleni ikaja na harakati nyingine za kuhamaisha watu kuandamana dhidi ya serikali au juu ya jambo fulani na wakaamua kuiita “UKUTIUKUTI”! Tunaweza kuwaona siku moja watashikana mikono na kuanza kuzunguka kwa pamoja huku wakitaka wengine nao washiriki kucheza na kurukaruka huku wote wakiimba “ukuti ukuti, wa mnazi, ukiingia upepo watetema!”

Nina sababu ya kuhofia hili.

Tulipokuwa watoto wadogo tulicheza michezo mbalimbali ambayo ilitufundisha misingi mbalimbali ya kimaisha. Kupitia michezo hiyo tulijifunza urafiki, kusaidiana, kushirikiana, kuwa mwangalifu, ujanja na hata mahusiano kati ya watu wa jinsia tofauti. Kwa kadiri tulivyokua ndivyo michezo mbalimbali tuliipita tukaingia katika aina nyingine za michezo hadi kwenye shule na vyuo vya juu. Michezo ambayo tulicheza ni mingi na ilikuwa na aina yake ya ushindani; kuanzia Kombolela, Kula Mbakishie Baba, Kioo Alikivunja Nani, Banchikicha, Turinge Bayoyo, na michezo mingine mingi ya utotoni.

Katika michezo yote hiyo naamini ipo ambayo hadi leo ukikumbuka inakupa tabasamu kwani inakurudisha miaka ile ya kutokuwa na hatia na furaha ya maisha; mmoja wa hiyo ni huu wa “ukuti ukuti”. Watoto kutoka mtaani au hata mtaa wa jirani walijikusanya pamoja mara nyingi baada ya michezo mingine yote kuisha wanashikana mikono katika mduara na kuanza kuimba huku wakizunguka na kuruka ruka. Huu ni miongoni mwa michezo iliyohusisha watoto wa kike na wakiume.

Wanapofika mwisho watoto wameanguka, wanacheka na kuagana au kwenda majumbani mwao wakiwa na furaha. Ni miongoni mwa michezo ambayo hata dada na kaka zao wakubwa waliweza kujumuika nao na hivyo kuendeleza mahusiano mazuri.

Siasa zetu sasa hizi zilipofika hasa kwenye Chama kikuu cha upinzani nchini cha CHADEMA ni kuwa tusipoangalia wanaweza au tayari wamefikia mahali pa kuanza kuja na harakati kama burudani. Tangu walipoanza na Operesheni Sangara, Operesheni Mzizima, M4C, wengi tuliona hatari ya kampeni hizi zenye majina mbalimbali ambayo labda matokeo yake yanaweza kubishaniwa. Kwa wanaojua mimi sikuwahi kuwa shabiki wa lile dubwasha la UKAWA ambalo naamini lilichangia sana kuvuruga upinzani na mwelekeo wa upinzani kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Lakini kama vile ndugu zetu hawataki kujifunza au wamegoma kujifunza baada ya kikao chao kingine wameamua kuja na kampeni nyingine au operesheni nyingine ambayo sasa wameamua kuiita “UKUTA” ukiwa ni umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania. Kimsingi, wameamua kuja na operesheni ya kupinga uongozi wa Rais Magufuli ambaye baadhi yao wameamua kumuona anaongoza kwa hulka za kidikteta.

Nina uhakika wa kutosha kati ya operesheni zitakazoshindwa vibaya ni hii. Kwa sababu wakati ile nyingine kwa kiasi ziliakisi hisia za Watanzania wengi na zilibeba kwa kiasi maudhui ya matamanio yao hii ya sasa ni operesheni ya wasomi wachache (the few elite) ambao wanaamini kinadharia na kwa sababu zao za kisomi kuwa Magufuli ni dikteta. Wanaamini hivi na wanataka watu wa kawaida ambao hawaoni huo udikteta wa Magufuli waunge mkono. Operesheni hii itafeli kwa sababu, mamilioni ya Watanzania waliokuwa wanalalamikia watoto wao kukosa madawati leo wanaona madawati yanatengenezwa na kupatikana kwa wingi, waliokuwa wanalalamikia watu kutokuwajibika au kuwajibishwa wanaona watu vigogo wanawajibishwa kila kona, na wale ambao walikuwa wanataka kuona serikali inasimamia vizuri watendaji wake wanaona hilo linatokea tena bila kupepeseana macho.

Wale ambao wanafikiri kuna haki ya kuonekana kwenye luninga live na kuamua kugoma kwa sababu hawaonekani live wanaweza kupata shida. Wananchi wa kawaida wanajua ipo haki ya kujua (right to information) lakini hakuna haki ya kuonekana. Kuandamana kutaka watu waonekane “live” wakati watu wanapata nafasi ya kujua hatabila kuona kwa wengine ni kuanza kuchanganya mambo.

Wale ambao kwa muda mrefu walikuwa wanataka mafisadi washughulikiwe bila huruma leo hii wanaanza kupinga serikali ambayo imeanzisha na kutenga fedha tayari kwa ajili ya mahakama maalumu ya kushughulikia wahujumu uchumi na mafisadi. Sasa unagoma ili kiwe nini? Serikali iache mpango huo? Unagoma ili serikali isihamasishe ujenzi wa madarasa mapya na kwa haraka? Unagoma ili watu wabovu na wasio na weledi wasiendelee serikalini? Unagoma ili tuendelee tulikokuwa?

Ndio maana hofu yangu ni kuwa tusipoangalia baada ya harakati hizi kushindwa; ndugu zetu wapendwa hawa wanaweza wakaja na operesheni “UKUTI UKUTI”. Hii itakuwa ni operesheni ya aina yake, watu wataambiwa wasimame pamoja kuonesha umoja lakini ni umoja katika kuzunguka duara! Tatizo la kuzunguka duara ni kuwa halikomi!

Binafsi ningependa kuiona CHADEMA inarudi na kuwa chama cha siasa na kufanya mambo yake kama CHADEMA, na kupitia taasisi zake. Hizi operesheni zake mbalimbali siyo tu zinapoteza muda mrefu lakini pia zinatishia zaidi uhai wake kama chama cha siasa na kwa vile viongozi wake bado hawajawajibishwa kwa madudu yao ya mwaka jana, basi wanaweza kabisa kwenda kuipoteza CHADEMA kuelekea 2020. Na wasije wakadhani kumlaumu Magufuli kwa madudu yao kutawapatia simanzi kwa wananchi; Magufuli amechaguliwa na kuungwa mkono na watu ambao walikuwa wanatamani mabadiliko ya kweli. Atahukumiwa na wananchi hao ifikapo 2020. Na mabadiliko hayo watu wameyaona; hayahitaji kupewa jina la operesheni.

Ni matumaini yangu baada ya kutoka M4C hadi UKAWA na kutoka UKAWA hadi UKUTA, wanaCHADEMA na wale wenye kuamini siasa za upinzani watakuwa wamechoka na hawatokuwa tayari kuimbishwa tena UKUTI UKUTI au KUMBAYA MY LORD KUMBAYA!

Kwani, tukianza kufanya siasa kama burudani, wananchi na watu wanaotuamini wanaweza waka wanasubiria kama watu wanaosubiria wimbo mpya wa Diamond, Ali Kiba na wasanii wengine.

Soma Zaidi: Mwanakijiji Ijumaa

Zee kunduchi sana hili
 
Hatuhalalishi kosa kwa kosa. Wewe ndiye uliyelileta hili la mambo ya ndani ya CHADEMA. Mimi nachozungumza hapa ni kuidharau katiba ya nchi ambayo inaweza kuiingiza nchi gizani. Hayanihusu ya CCM kukiuka katiba yake ni mambo ya ndani ya CCM lakini pale katiba ya nchi inapokiukwa kwa dikteta kujipa madaraka ambayo hanayo ndani ya katiba ya nchi hili ni lazima tulipige vita kwa nguvu zote.

Katiba haijampa nguvu Magufuli, Tulia au Ndugai awazuie UKAWA jukadili chochote ndani ya Bunge kwa mustakabali wa nchi yetu. Kumbuka Tulia kwa maagizo ya mkuu wale alizuia mjadala wa lugumi toka kwa UKAWA na pia akazuia mjadala wa kufukuza wanafunzi UDOM. Dikteta sasa hivi kazuia UKAWA kufanya maandamano nchini, kufanya mikutano nchini na kwa kudai siasa zifanywe na waliochaguliwa tu na wakati huo huo yeye anafanya siasa na wasiochagulia.

Siasa ni watu na watu ni siasa hakuna kipengele chochote ndani ya katiba kinachompa nguvu magufuli kuzuia Vyama vya upinzani kufanya shughuli zao nchini hadi 2020, HAKUNA huo ni ukiukaji mkubwa wa katiba ya nchi. Halafu UKAWA wakilalamika anaanza kutumia kauli za vitisho.

Mkuu hapo ndipo mnapokosea. Mnahalalisha kosa kwa kosa et kwa kuwa ccm wamefanya vile nasi tutafanya vivyo hivyo. Hapo ndipo mnapokosea. Walah nakuambia iyo sept mosi mtapata mandezi tuu .Tena ikiwa jumatatu ndo hamtopata watu. Andaeni nguvu na mfungue moyo ili watakapopitisha upupu msikimbie. Yangu macho . Siku iyo ntapiga mision town zangu kama kawa yaan. Maana siasa n utapeli tuu. Leo ukiambiwa hii nyeusi kesho utaambiwa no hiyo n nyeupe siyo nyeusi. Aliekuwa anaiita nyeupe ataanza kusema no hiyo nyeusi. Just like vicious cycle of poverty
 
Kwa wenye upeo finyu wa kufikiri kama wa kwako hilo ndilo mnaliloliona kwamba CHADEMA inapoteza muelekeo, lakini ukweli ni kwamba anayeleta tafrani zote hizi nchini anayedhani yeye ni Mungu hastahili kukosolewa, anayekurupuka kila kukicha na vitisho vyake uchwara, aliyelewa madaraka ndani ya miezi tisa tu.

Tanzania ni nchi ya vyama vingi kamwe hana ruhusa yoyote ile ya kutaka kuvidhibiti vyama vya upinzani ndani na nje ya Bunge na kufanya hivyo ni kukiuka katiba ya nchi.

Tafakari kwa kina kabla ya kuandika pumba.
Povu,jazba,ma2c yanini kwenye kubadilishana mawazo Na kujenga hoja mkuu?
 
Ahsante sana kwa heshima ila mie sijafikia ubabu, mimi pia nakuheshimu sana pia ila naona unaanza kupotoka kwa kuandika mambo ambayo hayana kichwa wala miguu (samahani kwa haya) Tanzania ni nchi yetu sote hakuna chama ambacho kina haki zaidi kuliko vyama vingine (kwenye katiba hakuna kitu kama hiki) Hakuna kiongozi wa chama mwenye nguvu zaidi ya viongozi wengine wa upinzani. Hakuna kiongozi aliyepewa haki ya kukiuka katiba ya nchi ili tu asikosolewe ili tu akurupuke kila anapojisikia kukurupuka bila kujali maslahi ya nchi na wananchi.

Inapotokea kiongozi kujiona yeye ni MUngu hastahili kukosolewa, inapotokeoa kuona kiongozi kila leo ni kutisha wananchi tu na wapinzani kwa kauli zake za vitisho na inapotokea kiongozi hataki kuiheshimu katiba ya nchi. Wote tulikemee hili kwa nguvu zote bila kujali itikadi zetu kwa faida yetu na vizazi vijavyo. Tanzania ni moja tu hakuna Tanzania nyingine ikiingia gizani watakaoisoma namba si wapinzani pekee bali Watanzania wote bila kujali itikadi zetu.

Anyway ...unajua nakuheshimu Babu ...pia najua bado unaamini lakini kama hupati ugali hapo ufipa ipo siku utajua hawapo serious. Hizi drama zinachosha in short ....tunahitaji damu mpya na mbinu mpya za kuikomboa Tanzania ...JPM anajitahidi sana ....tumuunge mkono na kumkosoa fairly badala ya kufanya propaganda kwenye kila issue....haiwasaidii Watanzania zaidi ya tamaa ya kwenda ikulu.
 
Unangoja mpaka nchi itumbukie gizani ndiyo uonyeshe jazba kwa hali ilivyo sasa nchini!? Kujikinga na ugonjwa siku zote ni rahisi mno kuliko kuutibu ugonjwa wowote ule.

Povu,jazba,ma2c yanini kwenye kubadilishana mawazo Na kujenga hoja mkuu?
 
Ahsante sana kwa heshima ila mie sijafikia ubabu, mimi pia nakuheshimu sana pia ila naona unaanza kupotoka kwa kuandika mambo ambayo hayana kichwa wala miguu (samahani kwa haya) Tanzania ni nchi yetu sote hakuna chama ambacho kina haki zaidi kuliko vyama vingine (kwenye katiba hakuna kitu kama hiki) Hakuna kiongozi wa chama mwenye nguvu zaidi ya viongozi wengine wa upinzani. Hakuna kiongozi aliyepewa haki ya kukiuka katiba ya nchi ili tu asikosolewe ili tu akurupuke kila anapojisikia kukurupuka bila kujali maslahi ya nchi na wananchi.

Inapotokea kiongozi kujiona yeye ni MUngu hastahili kukosolewa, inapotokeoa kuona kiongozi kila leo ni kutisha wananchi tu na wapinzani kwa kauli zake za vitisho na inapotokea kiongozi hataki kuiheshimu katiba ya nchi. Wote tulikemee hili kwa nguvu zote bila kujali itikadi zetu kwa faida yetu na vizazi vijavyo. Tanzania ni moja tu hakuna Tanzania nyingine ikiingia gizani watakaoisoma namba si wapinzani pekee bali Watanzania wote bila kujali itikadi zetu.
Chadema haitendi inachohubiri na hawapendi kukosolewa kwavile tu hawana dola. Zama hizi za JPM tutajadili mustakabali wa taifa hili na kuelewana bila kuhusisha uvyama. Sisi kama wananchi tunaweza kujisimamia wenyewe nje ya vyama hivi ndumilakuwili.
 
Toka Dr Slaa atoke Chadema basi umeondoka nae...Kwa JK udini ulikusumbua sana
 
CCM inatenda wanayohubiri? Tangu lini? Sasa tunalivua gamba ili kuwafukuza wale wanaokichafua chama chetu. Nimejitoa kafara ili kupambana na mafisadi (halafu tunamuona mpambanaji anakata kona kimya kimya kuhusu Lugumi, UDA, Escrow, Pride, IPTL, MV Dar etc) Nimejitoa sadaka ili kuwatetea wanyonge nchini halafu tunaona Wanafunzi 8,000 wanafukuzwa usiku wa manane na polisi wenye mbwa, na silaha kali na mjadala wa udhalilishaji wa hawa Watanzania wenzetu unazuiliwa ndani ya Bunge ili tu Serikali ya mheshimiwa asiyestahili kukosolewa isiadhirike . Yote haya huyaoni au kuyasikia Mkuu!? Lini umeanza kuwa na upofu na ukiziwi!?

Chadema haitendi inachohubiri na hawapendi kukosolewa kwavile tu hawana dola. Zama hizi za JPM tutajadili mustakabali wa taifa hili na kuelewana bila kuhusisha uvyama. Sisi kama wananchi tunaweza kujisimamia wenyewe nje ya vyama hivi ndumilakuwili.
 
CCM inatenda wanayohubiri? Tangu lini? Sasa tunalivua gamba ili kuwafukuza wale wanaokichafua chama chetu. Nimejitoa kafara ili kupambana na mafisadi (halafu tunamuona mpambanaji anakata kona kimya kimya kuhusu Lugumi, UDA, Escrow, Pride, IPTL, MV Dar etc) Nimejitoa sadaka ili kuwatetea wanyonge nchini halafu tunaona Wanafunzi 8,000 wanafukuzwa usiku wa manane na polisi wenye mbwa, na silaha kali. Yote haya huyaoni Mkuu!? Lini umeanza kuwa na upofu!?
Tatizo lako kuu ni uvyama na kufundishwa kupiga propaganda at any cost. Nikiitaja Chadema unaitaja CCM kama cover up ya Chadema! Nimekwambia kama hupati ugali ufipa unapaswa kuipima fairly kupitia ahadi zao.
 
ukutiukuti-990x660.jpg

Daaah nilifikiriaga kuwa wewe unaweza ukawa political analyst mzuri, ambacho ninaweza kukisema sasa hv ni kuwa kumbe wewe ni mshabiki wa siasa tu... Mediocre..! Kuna jamaa alikuwa anatetea rasimu ya katiba ya Warioba lakini akawa wa kwanza kula tapishi lake...

Back
Top Bottom