Serikali au Taasisi Binafsi naomba muwekeze kwenye michezo hii miwili niliyobuni kutokea hapa hapa Tanzania

Skythelimit

Member
Jul 19, 2023
27
53
Hello heshima kwenu ndugu zangu!

Mimi ni kijana Mtanzania mpenda michezo, na katika kujihusisha sana na michezo, Mungu amenijalia kujipata kwa kuja na aina mbili za michezo.

Mchezo wa kwanza utakuwa ukijulikana kama FENCEBALL au Mpira wa uzio. Na mchezo wa pili utajulikana kama REMAVOLLY.

Unaweza kushangaa nimewezaje kubuni michezo hii, lakini mimi kubuni michezo hii ni jambo la kawaida sana kwa sababu hadi sasa wenzetu wazungu wanaongeza aina tofauti tofauti za michezo mipya kama TEQBALL, PICKLEBALL, PADEL, BADMINTON, RACQUETBALL, ANGLEBALL, BOSSABALL N.K.

Hivyo kupitia michezo hii endapo kama taifa tutafanikiwa kuanzisha mashindano hayo Fenceball na Remavolly faida hizi zitaweza kuja nchini kwetu;
  1. Kuwa na shirikisho la michezo hii hapa nyumbani Tanzania likisimamia michezo hii duniani kote kama ilivyo Fifa kwenye mpira wa miguu.
  2. Vijana wengi wa kitanzania kupata platform ya kuonesha vipaji vyao katika michezo hii mipya.
  3. Kuandaa mashindano ya dunia huku sisi Tanzania tukiwa na faida ya kuanza michezo hiyo mapema na hivyo kuwa wepesi kwetu kuchukua kombe la dunia katika mpira huu wa uzio.
  4. Watanzania kupata fursa ya kuzunguka nchi mbalimbali duniani kwenda kufundisha michezo hii kwa sababu sisi Tanzania ndio tutakuwa waasisi wa michezo hii.
  5. Kuingiza michezo hii kwenye mashindano ya olimpiki yanayofanyika nchi mbalimbali duniani, na hivyo watanzania tukapata fursa ya kujitangaza zaidi.
Udhamini unaotosha kwenye kuanzisha michezo hii ni hasa kupata hall kwa ajili ya kujenga kiwanja cha uzio ukubwa wa 20x30 ndani ya hilo hall ambalo litakuwa na nafasi za mashabiki kukaa.

Uwekezaji ndani ya eneo hili utawezesha kuwa na Academy ya michezo yote kwa ajili ya watoto na vijana na watoto wa kitanzania kukuza carrier zao katika michezo hasa football, tennis, Fenceball, Remavolly, Teqball, table tennis n.k.

Hivyo nawaombeni tulijenge taifa letu katika michezo kwa pamoja.
 
Sio mbaya Ukaandaa Video clip ya Dakika 2 ukionyesha mchezo/michezo hio ilivyo.
 
Back
Top Bottom