Elections 2010 MwanaJF, Umejiandaaje kulinda kura yako?

Ramos

JF-Expert Member
May 13, 2010
498
130
Ni wazi kuwa wanaJF wengi hapa ni wapenda HAKI. Naamini kati yetu tupo tutakaopiga kura mwaka huu. sasa nauliza umejiandaaje kulinda kura yako mwaka huu. Kumbuka kuwa siku hizi haki haidaiwi, inapiganiwa...
 
Ni wazi kuwa wanaJF wengi hapa ni wapenda HAKI. Naamini kati yetu tupo tutakaopiga kura mwaka huu. sasa nauliza umejiandaaje kulinda kura yako mwaka huu. Kumbuka kuwa siku hizi haki haidaiwi, inapiganiwa...

Ni point ya muhimu sana mkuu!...Maana kupiga kura ni jambo moja, na kufuatilia hatima ya kura yako ni ishu nyingine!...mimi for sure nitapiga kura, lakn kwa bahati nzuri eneo nililopo lina hali kubwa sana ya upinzani, na kuna watu toka sasa wamejiandaa kwa hali na mali, na nitaungana nao!
 
Kura ni siri yangu na sina mamlaka ya kuingilia wale ambao watahesabu kura hizo baada ya mimi kukamilisha Jukumu langu la kupiga kura
 
Kwa kuwa namwelewa mwizi wa kura zangu ni CCM.

Nimetambua kuwa ni wajibu wakuhamasisha wanaharakati na vyama mbadala kufanya kazi ya ziada ili kuelimisha wapiga kura kubaini wezi wa kura hata kabla ya kupiga kura kwani wezi nao hufanya maandalizi mapema ya kupiga kura. Kazi hii nimeshaanza na ninaendelea kufanya, sihitaji kulipwa na mtu, nattumia raslimali nilizonazo kkufanikisha kazi hii ngumu. Ni muda mzuri kila mwenye nia njema na nchi kushiriki katika kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kuzilinda kura zao.

Naomba kama una mbinu za ziada za kulinda kura utushirikishe ili tuzitumie.
 
Back
Top Bottom