MwanaHalisi limedoda, limekwisha sasa

mnozya

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
207
44
Binafsi naona limefilisika kimawazo na kiuchambuzi.

Mimi ni msomaji sana wa Mwanahalisi ila toleo la jana kuna makala ya Kubenea ihusuyo UDINI KUINGIA BUNGENI, likijenga hoja kuwa mawaziri waislamu wanaonewa ama kukamiwa kwa sababu ni waislamu likitolea mfano wa mgongano wa Ghasia na Jenista, Dialo na Kawambwa na likahoji Mbona hao wabunge hawakuwa wakali baada ya serikali kupitia Chikawe kutoa tamko la mahakama ya kadhi? Kubenea akamailizia kwa uchambuzi wa kama mtoto wa chekechea eti ni kwa sababu chikawe ni Mkristo.

Kila mwenye akili timamu aliyesoma hiyo makala hawezi akasadiki kama imeandikwa na Kubenea na kuchapishwa na Mwanahalisi. UKWELI NADHANI MWANAHALISI IMEANZA KUFILISIKA KIUCHAMBUZI.
Nilijiuliza hivi kweli hata Ndimara Tegambwage hakuweza kumshauri, maana namwamini yule mzee ni kichwa.

Hivi kweli Kubenea alitaka wabunge wawe wakali kuhusu kadhi wakati akijua ni suala linalosigana na KATIBA YA JAMHURI? Hivi kweli Kubenea alitaka hao wabunge wawe wakali ili hali Tanzania ni nchi isiyo na dini? Iweje Mabudha nao wakitaka mahakama yao, na Wakristo watake mahakama yao katika mfumo wa KISERIKALI?

Kuanzia jana nimeingiwa na mashaka sana na uwezo wa kufikiri, na kuchambua wa Kubenea.
 
UKWELI NADHANI MWANAHALISI IMEANZA KUFILISIKA KIUCHAMBUZI
Nadhani usimlaumu Kubenea kwa habari ya Jana. ile habari ndio iliokuwepo ndani ya Bunge. kwani tayari baadhi ya wabunge wamezungumza waziwazi kama wanasakamwa. SOMA Tamko la Msambya kuhusu mahakama ya kahi alivyosema.
 
Kuelekea 2010 kuna kila aina ya mizengwe kunyong'onyeza wapambanaji dhidi ya ufisadi na mafisadi. Kubenea songa mbele, kaza buti, simamia unachokiamini. IKO SIKU ukweli utadhihiri, haki itatawala, mafisadi watagwaya.
 
UKWELI NADHANI MWANAHALISI IMEANZA KUFILISIKA KIUCHAMBUZI
Nadhani usimlaumu Kubenea kwa habari ya Jana. ile habari ndio iliokuwepo ndani ya Bunge. kwani tayari baadhi ya wabunge wamezungumza waziwazi kama wanasakamwa. SOMA Tamko la Msambya kuhusu mahakama ya kahi alivyosema.

Siamini wala sikubali kuwa kila kinachozungumzwa na wale jamaa ni pointi. Kuzungumza Msambya siyo hoja iwe habari yenye uzito kama ile. PIA KUBENEA ALITOA COMMENTS ZAKE KWENYE HIYO MAKALA. Pia kumbuka ile ni makala na si reported news.

Mwaka 1995 Nyerere akiwa Mbeya alisema kuwa mtu mwenye akili akikwambia kitu cha kipumbafu na wewe ukalibeba atakuona ni Mpumbafu. Namaanisha ile makala haikuwa na viwango vya Kubenea na Mwanahalisi lile nilijualo.
 
Binafsi naona limefilisika kimawazo na kiuchambuzi.

Mimi ni msomaji sana wa Mwanahalisi ila toleo la jana kuna makala ya Kubenea ihusuyo UDINI KUINGIA BUNGENI, likijenga hoja kuwa mawaziri waislamu wanaonewa ama kukamiwa kwa sababu ni waislamu likitolea mfano wa mgongano wa Ghasia na Jenista, Dialo na Kawambwa na likahoji Mbona hao wabunge hawakuwa wakali baada ya serikali kupitia Chikawe kutoa tamko la mahakama ya kadhi? Kubenea akamailizia kwa uchambuzi wa kama mtoto wa chekechea eti ni kwa sababu chikawe ni Mkristo.

Kila mwenye akili timamu aliyesoma hiyo makala hawezi akasadiki kama imeandikwa na Kubenea na kuchapishwa na Mwanahalisi. UKWELI NADHANI MWANAHALISI IMEANZA KUFILISIKA KIUCHAMBUZI.
Nilijiuliza hivi kweli hata Ndimara Tegambwage hakuweza kumshauri, maana namwamini yule mzee ni kichwa.

Hivi kweli Kubenea alitaka wabunge wawe wakali kuhusu kadhi wakati akijua ni suala linalosigana na KATIBA YA JAMHURI? Hivi kweli Kubenea alitaka hao wabunge wawe wakali ili hali Tanzania ni nchi isiyo na dini? Iweje Mabudha nao wakitaka mahakama yao, na Wakristo watake mahakama yao katika mfumo wa KISERIKALI?

Kuanzia jana nimeingiwa na mashaka sana na uwezo wa kufikiri, na kuchambua wa Kubenea.

Thanks, keep your eyes on this gazzete, they are behind JK!
 
Naomba address yao nitaenda kuwapa pongezi "physically".
Hili ni gazeti haswaaa!!! la watanzania!!! Tena la wasomi!! Mzamlendo Msomi lazima asome gazeti hili.
HONGERA MWANAHALISI!!
 
Pole kwa hali ya sintofahamu iliyokuandama kichwani kutokana na ugonjwa wako sugu. Mwanahalisi linachapa na kuuza nakala nyingi kuliko magazeti yote yaliyo makini hapa nchini, ukiachia yale ya Shigongo (ya udaku). Linachapa zaidi ya nakala 70,000 kila wiki na ni gazeti la Kswahili lenye circulation kubwa kuliko yote hgapa duniani.

Rekodi ya kuchapisha nakala nyingi iliwahi kushikiliwa na RAI huko nyuma lakini Mwanahalisi limekaa kileleni kwa takriban miaka mitatu au zaidi.

Linakaa siku 3 hadi nne kwenye meza za mauzo kwa sababu baada ya kutoka watu huliuzia kwa siku kadha baadaye. Na pia nitasema kuwa newsroom ya Mwanahalisi, ingawa ni ndogo, ni ya kisasa zaidi (most modern) kuliko zote nilizowahi kutembelea hapa jijini.
 
Huyu anafanya makusudi kujaza board ya JF na mabandiko yake ili yale ya maana yasiendelee kujadiliwa ipasavyo. Nadhani inabidi tususie kufungua threads anazoanzisha!
 
Ni kweli kabisa. Anafanya makusudi tu kwani thread hii ilishaanzishwa na Mnozya tangu last year. Asante MODS kwa kuona ujinga wa MS na kuziunganisha thread hizi.
 
We ndo umenena mkuu!
Pole kwa hali ya sintofahamu iliyokuandama kichwani kutokana na ugonjwa wako sugu. Mwanahalisi linachapa na kuuza nakala nyingi kuliko magazeti yote yaliyo makini hapa nchini, ukiachia yale ya Shigongo (ya udaku). Linachapa zaidi ya nakala 70,000 kila wiki na ni gazeti la Kswahili lenye circulation kubwa kuliko yote hgapa duniani.

Rekodi ya kuchapisha nakala nyingi iliwahi kushikiliwa na RAI huko nyuma lakini Mwanahalisi limekaa kileleni kwa takriban miaka mitatu au zaidi.

Linakaa siku 3 hadi nne kwenye meza za mauzo kwa sababu baada ya kutoka watu huliuzia kwa siku kadha baadaye. Na pia nitasema kuwa newsroom ya Mwanahalisi, ingawa ni ndogo, ni ya kisasa zaidi (most modern) kuliko zote nilizowahi kutembelea hapa jijini.
 
Huyu anafanya makusudi kujaza board ya JF na mabandiko yake ili yale ya maana yasiendelee kujadiliwa ipasavyo. Nadhani inabidi tususie kufungua threads anazoanzisha!

Thanks BoraMaisha huyu jamaa inabidi akifungua thread yake akute macartoon like this

:welcome::violin::peep::sorry:
 
Labda mtu hapendi baadhi ya waandishi wake..
.
Sidhani kama mtu anaweza kulichukia gazeti kwa sababu ya waandishi wake, japo anaweza lichukia ama kwa editorial policy yake (Wahariri), ama kwa wamiliki wake, kama watamfluence editorial.

Waandishi/contributors wanabaki ni waandishi tuu na watahukumiwa for what they write na sio kwa gazeti gani wanafanya/andikia.

Nikirudi kwa Mwanahalisi, nadhani huku kukosekana kwa vigongo vyenye msisimko, kunatokana na kufuata profesionalism ya taaluma ya habari, kwa maoni yangu it has something to do with Kamwaga kukaa sebuleni na Kubenea kuingia chumbani. Hivyo Mwanahalisi linahama toka cheap politics tabloid into serious issues, well research political agenda, and there is price to pay, watawapoteza wale wasomaji wao wapenda udaku wa kisiasa.

Kama survival ya Mwanahalisi ni udaku wa kisiasa ili wauze sana, basi kuna uwezekano Kamwaga akalazimika kupelekwa chumbani na sebuleni akarejea mwenye nyumba mwenyewe Kubenea hivyo kuendeleza udaku wa kisiasa na agenda zilizokusudiwa just for survival not for professionalism.

All the best Wanahalisi wote.
 
Kaka habari yako ni nzuri saana, kwa upande wangu mimi namchukulia Kubenea kama JK tu kitabia maana ni watu wa visasi tu sasa katika jamii ukishakuwa na visasi basi ndo umekwisha watu kwanza hawataamini habari zako kwa kuwa hawako certain kuwa umeandika habari hii kumkomoa mtu au la? Nilistaajabu saana especially kipindi cha nyuma na hicho ndicho kimemdondosha huyu jamaa kumuweka Lowasa na Rostam front page kila siku mpaka vipofu wa mawazo wakaona mbona kila siku hawa wapo hapa na ni kwa mabaya tu? Sasa Basi kaka mimi huwa naona kuna kasoro unapotoa hoja kwa kusema kwa mtu mwenye akili timamu hawezi fikiri hivi au vile hilo si neno zuri maana wewe una kipimo gani na hoja yako? umepima wapi? hii ni open forum hivyo hija yako inaweza ikawa tofauti na wengine wanavyofikiria na hapa hapa wakakupa facts ukakubaliana nao unajua wewe ndo unakuwa huna akili timamu? Hivyo toa hoja usiweke biasness.

thanks mkuu wangu
 
sasa pasco unasema mpenda mageuzi, mwanahalisi nalo linasema mpenda mageuzi. sasa mbona mtafautiana uansema sio professional. ninwasiwasi na wewe
.
Malaria Sugu, huna haja wala sababu ya kuwa na wasiwasi na mimi kuwa mshabiki wa mageuzi huku nikili cricitisize Mwanahalisi, ndio maana kuna Zitto/Dr/Slaa na Mbowe ni wanamageuzi and yet not the same na Lipumba/Mrema/Mbatia/Mtikila na wote ni wanamageuzi.

Hata wana CCM kama Nape/Sitta/Mwakiembe/Kilango etc pia ni wana mageuzi japo wako ndani ya CCM hao wakipigana from within.
Bado unawasiwasi?.
 
Umejibu vema Pasco.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom