Originally posted by mnozya
Kila mwenye akili timamu aliyesoma hiyo makala hawezi akasadiki kama imeandikwa na Kubenea na kuchapishwa na Mwanahalisi. UKWELI NADHANI MWANAHALISI IMEANZA KUFILISIKA KIUCHAMBUZI. Nilijiuliza hivi kweli hata Ndimara Tegambwage hakuweza kumshauri, maana namwamini yule mzee ni kichwa.
Mtu anaweza kuwa na chuki/ugomvi/wivu/hasira binafsi na Kubenea as a person, lakini lazima wote tukubali kuwa gazeti la Mwanahalisi limekuwa ndiyo chombo pekee cha habari hapa Tanzania chenye kuthubutu kuwataja mafisadi wakubwa nchi hii wa Richmond, EPA na wengine bila kuogopa.
Wahariri wa magazeti mengi Tanzania wameshakuwa compromised na mafisadi (wanakunywa nao chai) au wamefungwa minyororo na wamiliki wa vyombo vya habari ambao wamekuwa wanaingilia sana uhuru wa vyombo hivyo. Pamoja na mapungufu yake makubwa as a person, Kubenea bado amekuwa anatoa mchango mkubwa kwenye mapambano dhidi ya ufisadi kupitia kwenye gazeti lake.
Tumpe mtu sifa yake hata kama hatumpendi kwa sababu binafsi au kwa mapungufu yake. MWANAHALISI so far limekuwa kiboko cha mafisadi na ndiyo limeweza kumgonga JK bila uoga.
Long live MWANAHALISI, pamoja na mapungufu yake