Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
[B]Wana_JF:
Toleo la leo la Mwanahalisi ni moto wa kuotea mbali. Limekwenda hadi mvunguni na kuanika uongo uliokubuhu alioutoa Mwenyekiti wa Kampeni za CCM, Abdulrahmani Kinana kuhusu ‘ukodishwaji' wa ndege za serikali kwa matumizi ya kampeni za CCM zilizofanywa na mke wa Rais, Salma Kikwete.
Gazeti hilo limethibitisha ‘risiti' (invoice) zilizotolewa na Kinana mbele ya waandishi wa habari wiki iliyopita ni feki – zilighushiwa na maafisa wa CCM wakishirikiana na baadhi ya wale wa serikali.
Kikubwa katika ‘risiti' hizo ni kasoro kubwa katika namna zilivyojazwa – kwamba zilionyesha fedha hizo zinazokusanywa na kitengo cha Wakala wa Ndege za Serikali (za ukodishaji ndege) zinaingizwa katika Vote Na 062 na Sub Vote 087, wakati katika mipangilio ya mahesabu ya serikali hakuna kabisa vifungu hivyo vya mpangilio vya fedha.
Nikipata soft copy ya stori hii nitawawekeeni hapa.
[/B]