Mwanafunzi mjamzito amtaja Paroko
Katika hali inayoonekana kuwashitua wengi, mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari ya Farkwa amemtaja Paroko wa Parokia ya Farkwa, Padri Godian Simpinge, kuwa ndiye aliyempa mimba.
Tukio hilo lilikuja baada ya wanafunzi wawili wa sekondari hiyo, mmoja wa kidato cha kwanza na mwingine kidato cha tatu kukutwa na ujauzito, kufuatia zoezi la upimaji wa mimba lililoendeshwa na shule hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mkuu wa shule hiyo, Rajabu Yengela, alisema zoezi hilo lilifanyika Aprili 22 mwaka huu. Alisema mwanafunzi mwingine wa kidato cha nne ambaye naye alihisiwa kuwa na ujauzito alitoroka wakati wa zoezi hilo likiendelea.
Mwalimu Yengela alisema mwanafunzi wa kitado cha kwanza alikutwa na ujauzito wa miezi sita, huku mwenzake akiwa na miezi minne toka apate ujauzito.
Mwalimu Yengela alisema, baada ya matokeo hayo, bodi ya shule iliagiza wanafunzi wote waitwe ili waeleze waliohusika kuwapa mimba hizo kisha wachukuliwe hatua.
Alisema, katika kikao cha bodi, mwanafunzi aliyetoroka wakati wa kupima alipatikana baada ya wazazi wake kubanwa na uongozi wa shule, ambapo alimtaja mwanafunzi mwenzake wa shule ya Sekondari ya Msakwalo (jina tunalo) kuwa ndiye aliyempa ujauzito huo. Lakini yule wa kidato cha kwanza (majina tunayahifadhi) akamtaja Padri Simpinge na kwamba ilikuwa ni wakati alipokuwa akiuza duka la Parokia.
Mwanafunzi huyo alifafanua kwamba Oktoba mwaka jana alichukuliwa kwenda kuuza duka la Parokia ya Farkwa wakati akisubiri matokeo yake ya darasa la saba.
Alisema mwezi Novemba, siku na tarehe ambayo haikumbuki, 'Baba' Paroko huyo alimtaka waende wakafanye mahesabu ya mauzo ofisini kwake na walipoingia ndani, Paroko huyo akafunga mlango na kuanza kumpapasa, baadaye akamwangusha chini na kumbaka.
Alisema Februari aliondoka parokiani hapo na kwenda kuishi na dada yake, lakini wakati wote huo hakujua kuwa ni mjauzito kwa kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukutana kimwili na mwanaume tangu azaliwe.Kaimu Katibu Tarafa wa Farkwa ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Farkwa, James Mayaka, alisema anashangaa kuona jeshi la polisi wilayani Kondoa likionekana kushindwa kulishughulikia suala hilo licha ya kuwa na vielelezo vyote ikiwemo kadi ya kliniki ya mwanafunzi huyo iliyomtaja paroko huyo kuwa ndiye mwenye ujauzito huo.
Alisema ofisi yake ilipokea barua kutoka kwa mkuu wa kituo cha polisi cha Kwamtoro ikimtaka atume mgambo kwenda kuwakamata watu wawili, mmoja akijatwa kwa jina moja la Corneli kuwa ni mtuhumiwa namba moja na jina la pili likiwa la Padri Simpinge akitajwa kuwa mtuhumiwa namna mbili katika kosa la kumpa mimba mwanafunzi huyo.
Nilimpigia simu kumuuliza mkuu wa kituo, Corneli ni nani na anaingiaje katika kesi hiyo wakati mwanafunzi huyo katika maelezo yake yote amemtaja padri na hata katika kadi ya kliniki amemwandika padri kuwa ndiye mwenye ujauzito, nikajibiwa kuwa ninachotakiwa ni kutekeleza agizo kwa mujibu wa barua hiyo, alisema mtendaji huyo.
Alisema wahusika wote hawakupatikana na kwamba padri huyo alikuwa safarini.
Kwa upande wake, diwani wa kata ya Farkwa, Gabriel Madge, alisema suala hilo baada ya kuona kuwa linasuasua waliamua kumwandikia barua mkuu wa wilaya ya Kondoa, Saidi Bwanamdogo, ili hatua zaidi zichukuliwe.
Alidai kwamba padri huyo ametuhumiwa siku nyingi kwa kuwarubuni kimapenzi wanafunzi wanaokaa katika bweni lililopo Parokiani hapo, lakini hawakuwahi kupata uthibitisho wa kumchukulia hatua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Omary Mganga alipoulizwa kuhusina na tukio alisema padri huyo tayari ameshatiwa mikononi mwa polisi na mara baada ya kukamilika kwa upelelezi huo atafikishwa mahakamani.
CHANZO: NIPASHE