TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

Pumzika kwa amani kamanda..umekufa kishujaa kwenye uwanja wa mapambano! Mungu aipe Moyo wa ujasiri familia yake katika kipindi hiki kigumu. Amen.
 
Nimelia sana sana, tuliongea juzi. Kwanini afe yeye tu? Hapana aiseee. Nimelia sana tulikua pamoja, Mama yake ndio Mama yangu, familia yake ndio yangu, tukipokuwa shambalai tuliamua kuhamia wote kwenda Magamba school. Why?

pole sana Elli
Mungu amlaze mahali pema kaka yetu Mohammed Mtoi
 
Last edited by a moderator:
Ni msiba mkubwa kwa UKAWA, CHADEMA, wana LUSHOTO, wana MABADILIKO, wana JF, WANABIBII, na watanzania kwa ujumla. R.I.P Mohamed Mtoi.
 
Huyu bwana nimemfahamia hapa hapa JF lakini kifo chake kinaniuma sana.
Kila mara napitia uzi huu nikitumaini nitakuta taarifa kuwa hajafa...
Inasikitisha sana.
Mungu amlaze mahali pema peponi.
 
Elimu uliitoa ,waelewa wakang'amua
Ukweli ulinena, uongo ukautenga,
Uwezo ulionesha, mfano ukawa,
Sasa pumzika maana Mohamed kazi umeifanya na wajibu umetimiza!
 
What exactly happened?

Sawa ni ajali, lakini ilitokeaje....tufahamishwe basis.

Gari imegonga mti? Imepinduka? Zimegongana uso kwa uso?

How? How?......kwa sababu huyu kamanda ni miongoni mwa wana JF ambao possibility yao kuingia bungeni ilikuwa ni over 90%!

Kwa kweli it pains, lakini hatuna jinsi. Kamanda katangulia mbele ya haki.

R.I.P kamanda....lakini tunakuhakikishia huko huko uliko, hamasa yetu ya mabadiliko nje ya CCM ndiyo imeongezeka zaidi!!

Aluta continua!

Kazi ya Mungu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom