Mwana FA atakuwa Naibu Waziri mbovu kuwahi kutokea Tanzania. Hatatoa msaada kwa wasanii zaidi ya kuwagawa

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,525
7,377
Huyu amepewa uwaziri na Mama Samia naona watu wengi wameipokea hii habari kama ni habari njema kwenye michezo sanaa na burudani.

Kwa tunaomjua Mwana FA hapa hakuna kitu kipya atafanya kusaidia wasanii na wanamichezo. Huyu i mbinafsi, ana roho mbaya, anaringa ile kuringa sio kitoto, ana dharau, mtu wa fitna na majungu na mchonganishi.

Hakuna lolote jipya atafanya kwenye hiyo wizara zaidi ya kuongeza matabaka kwa wasanii, kuwaharibia wenzake asiowapenda maana huyu jamaa ni ana ile roho ya Kiswahili 100%.

Hapa wasanii na wanamichezo wamepigwa mara mia Dr Abbas japo alikuwa anafanya mambo yake kwa ufahamu mdogo wa sanaa ila alikuwa anafikika anakaribisha kila mtu na hana mipaka wala kutengeneza makundi.

Mwana FA kuwa Waziri ni habari mbaya kwenye sanaa yetu. I wish Nikki wa Pili au Jokate wangekuwa wabunge wapewe hii wizara awa ni wazungu wa roho na wanapenda kuona wenzao wakipiga hatua hawana choyo kama huyu mtoto wa kitanga.
 
ni Naibu Waziri , halafu mbona unajifanya much know sana kuliko hata Rais na Washauri wake?
Rais na washauri wake wamemuweka kisiasa ili avutie watu wa sanaa na burudani na michezo wajisikie ni sehemu ya serikali. Lakini huyu mtoto wa kitanga hakuna jipya atafanya. Nasubiri tuone atafanya nini kipya zaid ya roho mbaya na kauzibe
 
Huyu bitoz amepewa uwaziri na Mama Samia naona watu wengi wameipokea hii habari kama ni habari njema kwenye michezo sanaa na burudani.
Kwa tunaomjaua mwana fa hapa hakuna kitu kipya atafanya kusaidia wasanii na wanamichezo.
Lakini mkuu huyu kijana si ni msomi wa masters maana yake atakuwa na ufahamu mkubwa

Halafu si ni msanii mkubwa tu

Aah basi atakuwa naibu waziri mmoja safi sana
 
Lakini mkuu huyu kijana si ni msomi wa masters maana yake atakuwa na ufahamu mkubwa

Halafu si ni msanii mkubwa tu

Aah basi atakuwa naibu waziri mmoja safi sana
Ufahamu anao ila leadership ni zaidi ya ufahamu. Kuongoza watu au taasisi ni talent ambayo huyu mtoto wa kitanga hana. Shida yake kubwa ni maringo, unafki, uswahili, fitna, uzandiki, roho mbaya na kila kitu kinachofanana na hicho. Trust me anaenda kuwaumiza wasanii wenzake badala ya kuwasaidia.
 
Back
Top Bottom