MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,772
- 4,054
Monday, 25 January 2010 08:44
Na Mwandishi Wetu, Tanga
SHULE Kongwe ya Sekondari ya Usagara iliyoko jijini Tanga inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa Walimu wa Masomo ya Sayansi na imebainika kuwa mwalimu mmoja analazimika kufundisha somo kwa wanafunzi 1,697.
Mwalimu huyo analazimika kufundisha mikondo 40 hali ambayo inadaiwa kusababisha kuporomoka kwa ufaulu.
Mkuu wa Shule hiyo Bw. Said Saadan aliliimbia Majira mara baada ya uzinduzi wa Kituo cha kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa sekondari hiyo, TESA, kuwa shule yake yenye wanafunzi 1697 ina walimu watatu wa masomo ya Sayansi, kila mmoja akifundisha somo mojawapo kati ya Hisabati, Jografia na Fizikia.
Bw. Saadan aliiomba serikali, taasisi na mashirika kusaidia kuongeza walimu wa masomo hayo ili kuinua kiwango cha ufaulu katika masomo hayo.
Awali Mwenyekiti wa Kimataifa wa TESA, Bw Omari Nundu ambaye ndiye aliyesaidia ujenzi wa kituo hicho, aliwataka wanafunzi hao kukitumia vizuri kuongeza kiwango cha ufaulu katika masomo yao.
Hafla hiyo ilitumika kukusanya fedha za kusaidia shule hiyo, ambapo sh. milioni.7.6 zilichangwa na wanafunzi wa zamani wa sasa, wazazi, walimu na wafanyabiashara maarufu wa jijini Tanga ili kuisaidia shule hiyo.
Miongoni mwa watu mashuhuri waliosoma katika Shule hiyo ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Alhaj Salim Kisauji, Dkt. Sachack wa Hospitali ya Tamta, Mzee Shash Lal, Injinia Omari Nundu, Ahmad Keya na Mwanvita Kabwanga