Mwalimu mmoja wanafunzi 1,700 Usagara

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054

Monday, 25 January 2010 08:44
Na Mwandishi Wetu, Tanga

SHULE Kongwe ya Sekondari ya Usagara iliyoko jijini Tanga inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa Walimu wa Masomo ya Sayansi na imebainika kuwa mwalimu mmoja analazimika kufundisha somo kwa wanafunzi 1,697.

Mwalimu huyo analazimika kufundisha mikondo 40 hali ambayo inadaiwa kusababisha kuporomoka kwa ufaulu.

Mkuu wa Shule hiyo Bw. Said Saadan aliliimbia Majira mara baada ya uzinduzi wa Kituo cha kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa sekondari hiyo, TESA, kuwa shule yake yenye wanafunzi 1697 ina walimu watatu wa masomo ya Sayansi, kila mmoja akifundisha somo mojawapo kati ya Hisabati, Jografia na Fizikia.

Bw. Saadan aliiomba serikali, taasisi na mashirika kusaidia kuongeza walimu wa masomo hayo ili kuinua kiwango cha ufaulu katika masomo hayo.

Awali Mwenyekiti wa Kimataifa wa TESA, Bw Omari Nundu ambaye ndiye aliyesaidia ujenzi wa kituo hicho, aliwataka wanafunzi hao kukitumia vizuri kuongeza kiwango cha ufaulu katika masomo yao.

Hafla hiyo ilitumika kukusanya fedha za kusaidia shule hiyo, ambapo sh. milioni.7.6 zilichangwa na wanafunzi wa zamani wa sasa, wazazi, walimu na wafanyabiashara maarufu wa jijini Tanga ili kuisaidia shule hiyo.

Miongoni mwa watu mashuhuri waliosoma katika Shule hiyo ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Alhaj Salim Kisauji, Dkt. Sachack wa Hospitali ya Tamta, Mzee Shash Lal, Injinia Omari Nundu, Ahmad Keya na Mwanvita Kabwanga
 
Afadhali hata hao wana huyo mwalimu mmoja.
Kuna shule inakimbiwa na walimu,
kwa hiyo wanafunzi wanafundishana wao kwa kwao........
Hatari sana
 
Afadhali hata hao wana huyo mwalimu mmoja.
Kuna shule inakimbiwa na walimu,
kwa hiyo wanafunzi wanafundishana wao kwa kwao........
Hatari sana

Watafundishana nini sasa? Inatakiwa kuwalipa pato kubwa sana waalimu wa bush kuliko wa mjini kutokana na mazingira waliyonayo!
 
Tanga? tafutaneni wenyewe huko tanga. unafikiri walimu wa hayo masomo hamna? kuna kitu hapo. mambo ya asubuhi unaamka unajikuta upo ufukweni nani anayaTaka?.
 
.......Tanga balaa kule sioni ajabu walimu kukimbia. Nina rafiki alipata kazi nzuri tu Tanga lakini alivyoenda akakuta vioja mwenywe alikimbia kazi.
 
nenda kaulize shule yoyote ya dar hapo. utakuta somo 1 walimu kama millioni hivi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom