clemence
JF-Expert Member
- Mar 31, 2011
- 594
- 212
Swali kuwa ni lini mwalimu alikuwa rafiki wa Gadafi na angekuwa hai angesema nini kuhusu kifo cha Gadafi ni dalili kuwa mwandishi amekosa hoja na ni mvivu wa kufikiri. Ni mtazamo kuwa kila alilopenda Mwl. Nyerere ndilo sahihi na kila alilolichukia sio sahihi. Ni mtazamo kuwa hakuna anayeweza kuwa na maoni sahihi ila Nyerere. Mwl Nyerere alikuwa mwanadamu wa damu nyama na mifupa.
Hakuwa malaika wala hakuwa mtume wa mwenyezi mungu. Yapo mazuri aliyoyafanya tunapongeza na kuyaenzi na yapo mabaya aliyofanya tunyamaza na kuyaepuka bila kuathiri heshima ya Mwalimu. Kutokana na hali ya Mwl Nyerere kuwa mwanadamu wa kawaida hawezi kuwa kipimo kwamba kila aliyemchukia yeye au kila aliyekuwa hana mahusiano na yeye basi ni mtu mbaya.
Waheshimiwa tunaheshimu sana maoni yenu lakini msitulazishe kuamini mambo mengine kama tunavyoiamini Biblia. Zama za zidumu fkra za Mwentekiti (Mtu mmoja) zimepita sasa kila mwananchi afikiri na fikra zake ziangaliwe. Kama Gadafi alifanya mabaya yasemwe na kama Gadafi alifanya mazuri nayo yapongezwe.
Jibu swali mkuu