Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Jamani, hiki ni kitendawili, DOWANS ni nani hasa?!!!!!! Kazi kwenu.
Kuanzia leo tutaanza kufunua na kuunganisha vipande vipande vya Dowans. Jumamosi iliyopita (tarehe 7 Machi, 2009) tulipata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Brig. Gen. Al-Adawi mtu ambaye jina lake, na anuani vinaonekana kwenye nyaraka za BRELA kuwa ndiye mmiliki wa kampuni iliyoko kwenye songombingo ya tuhuma za ufisadi ya Dowans. Jumamosi hii iliyopita pia tulipata nafasi ya kuzungumza tena na Brigedia huyo baada ya kugundua kuwa ametuongopea. Kati ya mahojiano ya Jumamosi ile na Jumamosi hii kulifanyika kikao huko Dubai Jumapili ya tarehe 8 Machi, baada ya mahojiano yetu na maamuzi mbalimbali yakachukuliwa.
Leo katika kuifunua Dowans tunaanza na wamiliki tu halafu habari zaidi ya nini kimejiri inakuja wiki hii katika kile tunachokiita "kumfunua Mwali". Kwa vile Waziri Ngeleja amesema anataka mjadala huu wa Dowans ufungwe, tumedhamiria kuhakikisha kuwa tunaufunga kwa namna yetu wenyewe.
Sehemu zote mbili za mahojiano na Gen. Al-Adawi zitarushwa katikati ya wiki hii kupitia mwanakijiji.com na bongoradio.com... USIKOSE KUONGEZEWA MASWALI KWENYE MAJIBU UNAYOFIKIRI UTAYAPATA
NB:*
- Tutaonesha pia jinsi gani Rostam Aziz aliwadanganya watanzania kuwa hakuhusika na suala la ujio wa Dowans na kudai kuwa yeye ni "mkandarasi tu" aliyeomba kazi na "kuambiwa kuacha anuani" yake...
Na mambo mengine ambayo yatakufungua macho kuthibitisha kile unachoweza kuwa umefikiria.. Dowans
Last edited by a moderator: