Yaani kwa jinsi ninavyo fuatilia mafisadi hawa, hadi naogopa. Yaani wamekuwa macho makavu kiasi kucheza na pesa za walalahoi kiasi hicho. Kawaida wavuja jasho wakimkamata mwizi kaiba simu, au kuku mtaani, ni mafuta ya taa, tairi shingoni kuenda mbele. Sasa hawa jamaa ushahidi uko wazi wamekula mabilioni kibao ya wavuja jasho. kama hamuwezi kuwahukumu watoeni kwa wavuja jasho mbona sheria huko zinatafuta waharibifu? Ooh kiliwaa kikawa, kikaenda kikarudi mpaka lini?