Saharavoice
JF-Expert Member
- Aug 30, 2007
- 3,883
- 2,374
Una maana wanaohubiri ubaya wa kitimoto wameshawahi kuonja walau kidogo?
Wangeonja wange hubiri utamu wa kitimoto.
Una maana wanaohubiri ubaya wa kitimoto wameshawahi kuonja walau kidogo?
TRL walijua kuwa mkuu anasafiri?
Maana lazima wabehave na kurekebisha mambo kama wanajua the big boss yumo ndani ya mchuma.
Angekata ticket kwa kutumia jina la mtu mwingine, halafu akasema anaangalia tu treni then anazama mchumani bila maafisa kujua.
Hapa ndipo nashindwa kuwaelewa watu. Hivi hata mtu akifanya jambo jema kwa kuwa itikadi yako ni tofauti na ya kwake linabadilika na kuwa baya???? Hapa Mwakyembe kakosea nini? Hivi yeye kufuatilia utendaji wa Shirika hili ambalo limekuwa kama ndoo mbovu ambayo kila jitihada za kujaza maji zimeshindikana kutokana na kuvuja nalo limekuwa kosa!!!!!!!!!! You are not serious. Kutokana na kupitia physically masuala yaliyo chini ya Wizara yake anajiweka katika nafasi nzuri ya kutoa maamuzi au ushauri sahihi tofauti na kukaa kwenye kiyoyozi na kungojea kila siku apokee taarifa za walio chini yake ambazo sometimes zinakuwa sugar quoted. Kwa kusafiri na wananchi ni sehemu mojawapo ya kupata mawazo raw from horses mouth. Maana mawazo aliyoyapata hayajachakachuliwa kwa maslahi ya yeyote maana ameyapata live kutoka kwa wadau wa usafiri huo. Hivyo nina hakika amejifunza jambo jipya.
Hongera bro. Mwakyembe keep it up lakini uyafanyie kazi na uyaweke bayana uliyoyaona na jinsi unavyokusudia kuyafanyia kazi.
Kimsingi ni uongozi dhaifu kutaka kuhusika na kila linalo tokea kwenye wizara;kwa mfano eti magufuli asafiri kwa basi ili kujua udhaifu wa barabara!Uongozi mzuri ni pale mkuu anapojenga uwezo kusimamia watendaji walio chini yake ili mambo yaende!!!!Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe amesema kuwa hakupata kusinzia njia nzima, wakati akisafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa treni, kwakuwa anafanya utafiti wake.
Waziri Mwakyembe amesema kuwa hakuweza kusinzia kwakuwa alihitaji kujiridhisha na hali ya usafiri wa treni na pia kujionea hali halisi ya wananchi wa Tanzania sehemu ambapo treni linapita.
'Nimejifunza mengi sana;ya Wizara yangu na Wizara nyinginezo' alisema Dr.Mwakyembe. 'Nitatumia niliyoyaona kwa maslahi ya Taifa' aliongeza.
Chanzo: Mimi mwenyewe niliyeambatana naye kwenda Dodoma kwa treni...
Inakuingia Akilini mwako kwamba Mtu ambaye amekuwa kiongozi katika serikali na mashirika yetu ya UMA kwa muda mrefu Kama mwakyembe analazimika kufanya safari ya namna hii ili kujifunza au kujionea mwenyewe ama matatizo ya usafiri wa treni au ya wananchi huko treni inakopita kama anavyoropoka huyu jamaa.
Maisha ya hao wananchi hao yanatofauti gani na yale ya wananchi wa Jimboni kwake Kyela? Majuzi alisema amepanda daladala kutoka mwenge kwenda tegeta na anadai kwamba tatizo pekee aliloliona na gharama kubwa ya nauli, matatizo ya wanaotumia usafiri wa daladala yanatofauti gani na wale wanaotumia treni?
Ni tatizo gani la usafiri wa treni mwakyembe amejifunza kupitia safari hiyo? alienda kuona kama kweli injini inazima zima? haya sasa siku hiyo haikuzima, kwa hiyo ametoka na picha gani hapo? kwamba habari za kuzima zima kwa injini za treni na hujuma za kishenzi zinazofanywa za kung'oa mataruma ya reli ni za uongo?
Give me a break.
Acha upofu wa fikra wewe. Mtu yeyote ambaye analazimika kufanya ziara ama experiements kama unavyosema wewe ili kubaini matatizo yanayowakabili wananchi wake hafai kupewa nafasi yoyote ile ya kisiasa. na kwa msingi huu Mwakyembe anakalia hiyo ofisi kinyume na matarajio ya kisiasa.
Huyo mtu na experiment yake mimi siwafahamu, labda unipe taarifa zake zaidi, hivyo mpaka sasa mfano wake hauna uhusiano wowote ni utoto aliofanya mwakyembe.
Utoto kutumia gogo kwenda Dom au ni upi mkuu? Mbona ni usafiri ambao wanapaswa kuutumia wote hao?
Kimsingi ni uongozi dhaifu kutaka kuhusika na kila linalo tokea kwenye wizara;kwa mfano eti magufuli asafiri kwa basi ili kujua udhaifu wa barabara!Uongozi mzuri ni pale mkuu anapojenga uwezo kusimamia watendaji walio chini yake ili mambo yaende!!!!
Hatuhitaji waziri wa mambo ya ndani kwa mfano,kukamata wezi na kuwapeleka polisi ili tuseme ni kiongozi bora!
Kwa hili simuungi mkono mwakyembe hata kidogo.
Grow up. that Guy did not travel, he was sending quite a different message.
Utoto kutumia gogo kwenda Dom au ni upi mkuu? Mbona ni usafiri ambao wanapaswa kuutumia wote hao?
mkuu nikumbushe shirika lipi la umma Mwakyembe alifanya.
we sangara kudadadeki...simaanishi kutadadeki namaanisha lile tusi la kike....ile sumu bado inamsumbua huyu.
Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe amesema kuwa hakupata kusinzia njia nzima, wakati akisafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa treni, kwakuwa anafanya utafiti wake.
Waziri Mwakyembe amesema kuwa hakuweza kusinzia kwakuwa alihitaji kujiridhisha na hali ya usafiri wa treni na pia kujionea hali halisi ya wananchi wa Tanzania sehemu ambapo treni linapita.
'Nimejifunza mengi sana;ya Wizara yangu na Wizara nyinginezo' alisema Dr.Mwakyembe. 'Nitatumia niliyoyaona kwa maslahi ya Taifa' aliongeza.
Chanzo: Mimi mwenyewe niliyeambatana naye kwenda Dodoma kwa treni...