Mwakyembe mgonjwa afya yake yadorora; ngozi yavimba mwili mzima. Yadaiwa alitegeshewa sumu

Nimezungumza na mke wa Dr Mwakyembe bi Lina Mwakyembe asubuhi hii amesema Mwakyembe hajalishwa wala kupewa sumu isipokuwa ni kweli kuwa anaumwa amepata inflammation kwenye ngozi lakini anaendelea vizuri.Kwahiyo mrusha taarifa kuwa maelishwa sumu na anakimbizwa India kapotosha sijui alikuwa analengo gani!
 
Mkuu kapewa sumu wapi ? Yuko wapi na wanamkimbiza India muda huu kwa ndege ipi ? Ya Rais au ndege gani ? Kwa nini India hapo Muhimbili wameshindwa ?Je atafika India kama umesema hali ni mbaya ?

Dowans hao wanaitaka ile pesa .Kazi kubwa sana .
dowans, mwakyembe, sita, lowasa ndo hao hao, wacha wamalizane.
 
lengo la hawa watu ni kutaka kusingizia kuwa amelishwa sumu na wapinzani wake.....kuna watu mabingwa kwa uongo duniani na mwanzisha mada hii ni mmoja wa waongo duniani
 
Nimezungumza na mke wa Dr Mwakyembe bi Lina Mwakyembe asubuhi hii amesema Mwakyembe hajalishwa wala kupewa sumu isipokuwa ni kweli kuwa anaumwa amepata inflammation kwenye ngozi lakini anaendelea vizuri.Kwahiyo mrusha taarifa kuwa maelishwa sumu na anakimbizwa India kapotosha sijui alikuwa analengo gani!

asante mheshimiwa kwa taarifa, wengine maswali yameshaanza kuwa mengi kichwani.
 
Kwa nini apelekwe India wakati hospitali ya maana ya MUHIMBILI ipo?

huu ndio ufisadi wenyewe...muhimbili wa avifaa na madaktari

ikishindikana si wampeleke hapo Nairobi hospital

why India?

Hilo nalo ni swali la kuulizwa na mtu mstaarabu? Pole
 
24 hours mtandao upo, nifanyeje? kwa raha zangu, Gozi linajuwa kundekeza, limeniwekea mitandao kibao nisikose raha zangu, TTCL, TiGo, BB. iPad 2 with wifi and 3G, Ji kompyuta lenyewe nililozawadiwa hivi karibuni ndio usiseme Dell XPS i7 with built in JBL sound system halafu nnaweza kulirusha kwenye ji 52" 3D screen la uhakika nikalitazama kwa mbali, unanini weyee? kwa raha zangu babu, halafu oohhh limbwata mbaya, nani kasema?

mweee nimecheka sana FaizaFoxy. Duu. Lakini nimekukubali kuwa we ni mkali kwenye IT, hata theluth sikaribiii. hongera.
 
Kwa nini apelekwe India wakati hospitali ya maana ya MUHIMBILI ipo?

huu ndio ufisadi wenyewe...muhimbili wa avifaa na madaktari

ikishindikana si wampeleke hapo Nairobi hospital

why India?

Muhimbili kwa walalahoi kama wewe
hawa wakubwa akikohoa tu au akipiga chafya anakimbizwa India, London huko
 
Nimezungumza na mke wa Dr Mwakyembe bi Lina Mwakyembe asubuhi hii amesema Mwakyembe hajalishwa wala kupewa sumu isipokuwa ni kweli kuwa anaumwa amepata inflammation kwenye ngozi lakini anaendelea vizuri.Kwahiyo mrusha taarifa kuwa maelishwa sumu na anakimbizwa India kapotosha sijui alikuwa analengo gani!

AKSANTE KWA TAARIFA HIYO, Ninaiamini 100% kwa kuwa umeitamuka kwa uwazi, hukuficha uso wala utambulisho wako nje ya jamvi hili
 
Nimezungumza na mke wa Dr Mwakyembe bi Lina Mwakyembe asubuhi hii amesema Mwakyembe hajalishwa wala kupewa sumu isipokuwa ni kweli kuwa anaumwa amepata inflammation kwenye ngozi lakini anaendelea vizuri.Kwahiyo mrusha taarifa kuwa maelishwa sumu na anakimbizwa India kapotosha sijui alikuwa analengo gani!

Basi itakuwa allergy muheshimiwa
 
Rwanda kwa sababu ya mtu mmmoja?

hebu tupumzishe sie

Mbona Kigoma Malima naye alilishwa sumu na hamkusema kuwa Rwanda itatokea?

Bila kusahau IMRAN KOMBE mlimuua na maisha yameendelea kama kawaida

tunaaangalia na umuhimu wa mtu mwenyewe, ndiyo maana hata wewe ukifa leo inawezekana sana hata ndg zako na majirani wasipate habari! Na hata wakipata wanaweza wasiomboleze,na wakiomboleza inaweza kuwa geresha tu au wakaja sababu ya kaubwabwa! nimekusoma sana naona una mambo ya kisomalisomali wewe!
 
Ndugu wana JF hizi ni taarifa za uhakika kabisa, Dr. Mwakyembe Kapewa sumu amevimba mwili mzima hali ni mbaya nilipopata habari hizi walikuwa wanafanya mpango kumkimbiza India. Nitarudi nikipata habari kwa undani

Nawakilisha

Wamemuwinda mpaka wamempata.Inasikitisha mtu mwenye uchungu na nchi kama huyu kuangamizwa.Tunamuomba Mungu amnusuru mtumishi wake.Amen!
 
Jamani mgongeeni senksi na yule aliyebreak news, msimpendelee Invisible !!

invisible kapata thanks 10, aliyebreak news(BobT) kapata thanks 3, na wote wametoa taarifa shallow

halafu bado wapo wanaoona umaana wa 'thank you', kujuana tuu
 
Chanzo ni yeye kutowalipua mafisadi siku alipokuwa na nafasi ya kufanya hivyo. akawasitiri akijua watamsifu, sasa wanaona ni mwiba, njia rahisi ya wao kuwa huru ni kumwondosha mapema.

kajichongea kaburi

mkuu uko sahihi kabisa...tuliwah kumwambia...na kuna kipindi alidhni hao watu wamekuwa nduguze akawa hata anashiri nao hafla mbali mbalia........haoni mwenzake sitta alivyo ndumila kuwili......
 
Wamemuwinda mpaka wamempata.Inasikitisha mtu mwenye uchungu na nchi kama huyu kuangamizwa.Tunamuomba Mungu amnusuru mtumishi wake.Amen!

kama kweli wamemnywesha sumu.....basi tena hakuna jinsi...huko india huwa wanapelekwa tu...maana hata steven kibona alipelekwa huko na wakasema amekula vyakula vyenye sumu na mwenzake wote wakafa...
 
Nimezungumza na mke wa Dr Mwakyembe bi Lina Mwakyembe asubuhi hii amesema Mwakyembe hajalishwa wala kupewa sumu isipokuwa ni kweli kuwa anaumwa amepata inflammation kwenye ngozi lakini anaendelea vizuri.Kwahiyo mrusha taarifa kuwa maelishwa sumu na anakimbizwa India kapotosha sijui alikuwa analengo gani!

Many thanks Regina, this is so ambigious info, ila umetupa ukweli na ww ni MP so i take it a correct info, hivi Dr. Mwakyembe hawezi kuingia JF kwa jina lake kamili? Huyu ni msomi why hiding indoors?
 
Ndugu wana JF hizi ni taarifa za uhakika kabisa, Dr. Mwakyembe Kapewa sumu amevimba mwili mzima hali ni mbaya nilipopata habari hizi walikuwa wanafanya mpango kumkimbiza India. Nitarudi nikipata habari kwa undani

Nawakilisha
Bob T,
kwanza karibu jf.
Pili mtu akipata madhara yoyote ya mwili kutokana na food poisoning, mwenye mamlaka ya kutoa taarifa kuwa madhara ni ya sumu ni madaktari na sio wewe.

Uamuzi wa kumpekeka mgonjwa India huamuliwa na madakitari na baada ya kujiridhisha tiba za nyumbani haziwezi.

Kwa vile uliahidi ungerudi baada ya kupata taarifa za uhakika na mpaka sasa hujarudi. Hebu soma hii post ya Mhe. Mtema
Nimezungumza na mke wa Dr Mwakyembe bi Lina Mwakyembe asubuhi hii amesema Mwakyembe hajalishwa wala kupewa sumu isipokuwa ni kweli kuwa anaumwa amepata inflammation kwenye ngozi lakini anaendelea vizuri.Kwahiyo mrusha taarifa kuwa maelishwa sumu na anakimbizwa India kapotosha sijui alikuwa analengo gani!
.

Ni ustaarabu kama BobT. utarejea humu na kuomba msamaha kwa uzushi wako uliotuletea humu!.
 
Ndugu wana JF hizi ni taarifa za uhakika kabisa, Dr. Mwakyembe Kapewa sumu amevimba mwili mzima hali ni mbaya nilipopata habari hizi walikuwa wanafanya mpango kumkimbiza India. Nitarudi nikipata habari kwa undani

Nawakilisha

NIMETOKA SASA HIVI KWA MWAKYEMBE AFYA YAKE KWELI IMEDORORA SANA LAKINI CHANZO BADO KUJULIKANA 100%

Ahsante kwa taarifa ambazo zimenifanya leo asubuhi niende nyumbani kwa Mwakyembe, (Mtongani, Kunduchi Beach, Dar es Salaam). Kwa kweli afya ya Mwakyembe ni mbaya sana. Kwa wengi waliomwona katika miezi mitatu iliyopita, afya yake ilionekana kuwa na mgogoro. It was just a question of time.

Kwa kuwa kuna conflicting medical diagnosis ya matatizo ya Mwakyembe, Wizara yake imeona akachunguzwe sehemu nyingine. Wapo madaktari wanadhani chanzo ni "food poisoning", wengine wanadai ni "exfoliative dematitis" (naomba msiniulize), wengine wanadai ni kisukarti na wengine wanasema ni "fungi infection". Ikiwa hata akina Kubenea wanapelekwa nje kwa uchunguzi na matibabu na wanaendelea kuwananga waliowapeleka, sembuse Mwakyembe?

Let's be fair. Hivi nani ata-rejoyce Mwakyembe akifa? I wish him all the best. Naona hali imebadilika hapa nyumbani kwa Mwakyembe, nawaona wasaidizi wa Mkuu nwa Nchi wakivinjarivinjari kwenye nyumba yake. Naondoka nisje nikakutwa hapa!

Jajimkuu
 
Back
Top Bottom