Mwakyembe katibu mkuu wa wizara yako ndio atakuharibia kazi.

Swala la Eng Chizi bado lina maswali mengi sana lakini kama kawaida ya wanahabari wetu hili ndio limepita! Wakati mwingine nashangaa kwanini hawa wanahabari wanazidiwa na hata wale wa magazeti ya udaku ambao hufatilia stori mpaka hatua ya mwisho kila kona ingawa zinakuwa binafsi sana.
Hivi lini JF itakuwa na gazeti kuleta mapinduzi ya ufukunyuzi wa habari tanzania?
 
Kwa kweli waandishi wa Tanzania nao low scores, haiwezekani hujuma kubwa hii isipate coverage kwenye magazeti na badala yake habari za kina shibuda ndiyo zinajaa.Eng. chizi hajatendewa haki na hawa katibu mkuu na waziri wanamaswali mengi ya kujibu.wakeup you journalists
 
imenikwaza sababu siku ile ya uzinduzi hadi tulichelewa safari ikidaiwa kuwa katibu mkuu ameizuia, hatukatai mabadiliko kabisa ila atcl ndio kwanza ina mwezi na ndio imeanza safari zake kisha mizengwe kama hiyo.pia kauli zake ni za kuikomoa atcl tu na si vinginevyo. kaka angu wengi hawaitakii mema ndege yetu.

Chizi pindi anafanya uzinduzi wa safari ya dar/tabora/kigoma/dar nilikuwepo uwanja wa ndege na alijinasibu kufanya vizuri ndani ya muda mfupi na akaonesha malengo yake kwa shirika.Nilimsifu sana.Lakini tatizo lililoipata ndege yetu kigoma unalifahamu na hata ukienda mwanza airport ipo nyingine pale imekuwa scrapper.

Tatizo kwa Mwakyembe sio uwezo wa Chizi tatizo hapa ni taratibu za upatikanaji wake ndo unahojiwa.
 
Mh wewe ni waziri ambaye umeteuliwa juzi tu, inawezekana haujui nini kinaendelea ndani ya wizara yako. Sisi kama watanzania ni muda mrefu sana tumeilalamikia serikali yetu kuwa tunahitaji ndege kwa ajili ya safari za anga.

Ni juzi tu Katibu mkuu wako alitamka maneno kuwa ndege hiyo isiruke mpaka itemize mashart yote.hali ya kuwa ndege imetimiza masharti yanayotakiwa kuruka. Je katibu mkuu alikuwa na dhamira gani kuizuia ndege isiruke? Kama mdau wa usafiri wa anga ilitustua sana kuona katibu mkuu ambaye ndie mtendaji wizarani na mtegemewa na wananchi ndio anakuwa mtu wa kwanza kuikwamisha ndege ya watanzania isifanye kazi.

Wiki mbili baadae baada ya ndege ile aina ya B 737 – 500 kuanza safari zake DAR- JRO- MWZ-DAR tukasikia ndege ile imepokea vitisho kuwa itafanyiwa hujuma. Ni wiki moja sasa tangu vitisho hivo vitolewe, na leo tunaona DIRECT MR. CHIZI ambaye ndio ameisimamia ndege ile mpaka kuileta hapa nchini amesimamishwa kazi.

Kuna haja gani ya kumuondoa MR CHIZI katika nafasi ambaye tumeona matunda yake? Au ni kwa vile alikaidi amri ya katibu mkuu wake ya kutoiondoa ndege kwa visingizio kuwa haijatimiza mashart? Hali ya kuwa imetimiza? Au kosa lake ni kuisimamia hii ndege mpaka ikapatikana? Au ni kwa vile yeye katibu mkuu hakushirikishwa ipasavyo katika kuileta ndege hii?? Nina maswali mengi ya kujiuliza kuhusu huyu katibu mkuu na namna alivyo mfukuzisha kazi mr chizi.Kiukweli katibu mkuu anakitu kimejificha nyuma yake kuhusu hii ndege na ATCL kwa ujumla.

Mh Mwakyembe hujuma kwa ndege zina fanyika katika mazingira tofauti, katika kile katibu mkuu alidai kuwa “tutaona itafika wapi” sasa ndio ameanza kwa kukushawisi wewe ili kumsafisha DIRECTOR CHIZI ambaye ameileta kisha na ndege hiyo kurudi kwao ili yeye KATIBU MKUU anufaike anavyonufaika katika makampuni mengine ya NDEGE ambayo yanamtumia kuisambaratisha ndege hii.

Tuna wasi wasi na katibu mkuu huyu ambaye inaonekakana yupo nyuma ya kikundi Fulani ambacho kina mtumia ili kuiua ndege hii ambayo inatumika kufanya safari za ndani ya nchi.

Sisi kwetu hii ni hujuma kubwa ambayo imefanywa na kiongozi wetu wa serikalini bila kuangalia maslahi ya taifa na badala yake anaangalia maslahi yake binafsi.

Kama waziri wa wizara husika tunaomba ukae na wadau mbali mbali wa secta ya anga ikiwemo AIR TANZANIA ili upate maoni yao.Hatuja pendezwa na hatujafurahia maamuzi ya katibu mkuu huyo kukushawishi kumsimamisha kazi DIRECTOR CHIZI.

Ahsaante sana
Madau.
Hakuna lolote wizi mtupu
 
I wish Mwakyembe angekuwa anayasoma haya maoni ingekuwa njema sana!
On a serious note kuna watu wanaihujumu ATCL the same to reli ili waweze jinufaisha either kwa hisa kwenye hayo makampuni au kwa kumiliki indirectly fleet.
Waziri wetu work on hao wahujumu bse ata iyo ndege ya kukodi utashngaa imepata ajari in no time ili hao akina Precision wapate inflate bei
 
Safi sana Kombe Sana.
Tatizo lipo kati ya masalia ya Nundu na Katibu Mkuu Ndugu Chambo na Mwakyembe ameingia kichwa kichwa bila tathimini ya kina.Tatizo bado linaonekana katika kupata CEO wa ATCL ,hivi Eng Chizi alijiteua kukaimu nafasi hiyo ?,na kama aliteuliwa na Nundu ,Chambo kama Katibu Mkuu alifanya nini na Bodi ya ATCL pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu Mkuu Utumishi.?.Uzembe na jeuri ya Chambo ndiyo kifo na udhaifu mashirika mengi yaliyo katika wizara ya uchukuzi,siyo reli,ATCL yenye unafuu japo ni mashirka muhimu katika ustawi wa uchumi wa nchi.Kipindi cha nyuma vyombo vya habri zilinadika tishio la Chambo kumweka ndani Chizi kama angeendelea na kazi ya kuleta na kurusha ndege iliyokodiwa ya ATCL.Kama kuna matatizo ya kiufindi mamlaka kama TCAA ndiyo ingetoa sababu za kina juu ya ubora na usalama wa ndege hiyo lakini mpaka sasa inaonyesha ndege hiyo ina ubora.Mwakyembe asipoangalia atajikuta anatumika kama mpira wa kiume kwa Chambo na kuvuruga shirika badala ya kujenga.

Hakuna Bodi...:confused2: how can they run business like this?...
 
Swala la Eng Chizi bado lina maswali mengi sana lakini kama kawaida ya wanahabari wetu hili ndio limepita! Wakati mwingine nashangaa kwanini hawa wanahabari wanazidiwa na hata wale wa magazeti ya udaku ambao hufatilia stori mpaka hatua ya mwisho kila kona ingawa zinakuwa binafsi sana.
Hivi lini JF itakuwa na gazeti kuleta mapinduzi ya ufukunyuzi wa habari tanzania?

I like this...yaani hawawezi kuendelea na tabia hii...insulting our intellect... na wanahabari hawafanyi investigative reporting to get to matter of the issue.

Napenda wazo la JF kuwa na gazeti
 
Huyu Katibu mkuu wa wizara hii Chambo sijui analindwa na nani maana kila aendapo anaharibu tu na kugombana na wenzake na haguswi .....walimuonya Nundu kuwa pale kwa Chambo umefika utatoka wewe yeye utamuiacha tangu EPA Chambo anapeta hadi sasa....nadhani ana ma God Father wakali sana wanamlinda kwa nguvu zote!!!chezea mtandao fisadi wewe??Mwakyembe umeuvaaagaa

.....Ikulu
 
Wanajamvi, mie nimesha andika sana kuhusu Omar Chambo, huyu ndio kiini cha matatizo makubwa ktk wizara ya uchukuzi! Alipoteuliwa kutoka Nishati na Madini na kuwa Naibu Katibu mkuu by then Miundombinu wengi tuliguna maana tunajua uwezo wake ulikuwa mdogo! Wakati tukishangaa haikupita hata miaka 2 akapewa ukatibu Mkuu.....tulishangazwa sana na kumshangaa mteuzi.!

Chambo hana uwezo kabisa! Amejaa majungu, chuki, vinyongo, vitisho na ufisadi! Kila shirika na taasisi iliyokuwa chini yake aliingilia mamlaka za Wakurugenzi wakuu na walipotofautiana alitishia kuwang'oa. Analazimisha 10% kwenye kila mradi. Mifano michache, pamoja na matatizo ya aliyekuwa CEO wa TANROADS Ephraem Mrema, mwanzo walikuwa marafiki wakubwa, akitaka pesa anakatiwa, Mrema alipoona jamaa anapitiliza akawa anamkatalia na ndipo bifu kati yao lilipoanza na kutiwa petrol na Chambo hadi kuhakikisha ameondoka. Wengine ni Ma-Dg wa TAA Eng. Prosper Tesha, pamoja na kazi nzuri aliyoifanya TAA alihakikisha anafanya mizengwe hadi akamtoa pale, wapo wengi akina Sekirasa wa Sumatra nz wengineo.

Chambo ameharibu vya kutosha wizara ya Miundombinu na sasa Uchukuzi. Matatizo makubwa ya reli, bandari, Atcl, TCAA, SUMATRA, TAZARA etc amechangia kwa kiasi kikubwa halafu watu wanauliza na kushangaa kwanini tupo hapa! Kama miundombinu iliyo asili ya maendeleo ya kiuchumi yapo ICU tutegemee nini? Muujiza gani Chambo ataleta? Anatamba kuwa yeye ni mteuliwa wa Rais hakuna wa kumbabaisha. Ndio maana jamii inaamini kuwa kwa vile ni mtoto wa fundi (matehemu baba yake alikuwa mganga wa Bwana mkubwa) na kwa kulipa fadhila hawezi kumuondoa. Kwa madudu yake kwanini tusiamini??????!?
 
Hilo ni kweli kabisa Ndugu Chambo ni kimeo kweli kweli la kujiuliza kwa nini Rahisi aliyemteua amemwacha huyu jamaa huku akimwondoa Mh. Omary Nundu ilhali mtu mharibifu kama huyu kabaki bado katika wizara nyeti kama kwa mustakabari wa taifa letu Tajiri linalotafunwa na michwa kama hawa kina Omary Chambo wasio na uwezo wa kuliongoza.
Hii ndiyo Tanzania Bwana
 
Back
Top Bottom