Mwaka wa kumi huu au zaidi umeajiriwa (unatumwa tumwa tu); je, ni kitu gani kinakufanya usijiajiri?

Ukijiajiri utatumwa na clients wako au soko. Tabu ipo pale pale

I'd argue wafanyakazi Wana a balanced life style kuliko waliojiajiri. Hii notion kwamba ajira ni mbaya na kila mtu inabidi ajiajiri as though self-employed wote wamefanikiwa is nonsense.
Huu ni ukweli ambao wabinafsi na wachoyo ambao wanabania wenzao kupata AJIRA KWa kivuli cha kuwasagia kunguni wajiari hawataki kuusikia
 
Population ya waliojiariji ni 2/10 wanaotoboa

Tofauti na watumishi 6/10 wanaotoboa


MTumishi anaoption ya kufanya biashara,kukopa kirahisi huku mfanyabiasha anaoption moja tu biashara na kupata mkopo lazma biashara iwe imara

Japo mfanyabiashara free will yake ni kubwa kuliko mtumishi...

N:B..kuhusu kutake risk bussnesman🙌🙌🙌🙌
Tatizo ni nini, elimu au kuna kingine?
 
Nakubaliana na hoja yako, basi wa namna hiyo, elimu haijamfanya awe huru; bali elimu inamfanya awe wa kutumwa tumwa tu
Uhuru wa kweli upo kaburini. Elimu inakupa upana wa ufahamu, kujiongeza. Mtu anaweza hataki kujiajiri.lakini kwenye ajira yake ana fursa za kupiga side hustle za kutosha.
Mfano mtu wa kukopesha bank. anaweza akaungana na wanasheria akawa analengesha Dili za kupiga muhuri wa mwanasheria. Form 20 au 10. Akipiga watu 15 kwa siku. Kwa mwezi ana hela nzito kuliko yule ambaye amejiajiri
 
Kuna mwaka nilijipanga kununua flat screen mpya ya nyumbani. Nikaingia mtandaoni na kuongea na muuza mali kwa njia ya simu. Akanielekeza mpaka dukani nikafika. Nikapokelewa na kijana wa kiarabu nahisi alikuwa O level. Kilikuwa kipindi cha likizo za shule. Akanipeleka kwenye sectiona ya flat screen kwenye duka na kunipa kila sifa ya TV iliokuwa mbele ya macho yangu. Mimi nilikuwa na ingia google na kuandika model namba ya TV na specs zake zipo kama dogo alivyosema. Nilikuwa na budget ya 1M, ila dogo kanishawishi kununua TV ya 1.5 M yenyewe warranty ya miaka 2. Kaniitia mtu wa usafiri na bei kambana na kumshusha. Mali ilifika salama na haijapata tatizo lolote huu mwaka ushapita. Baada ya siku kadhaa ya kununua ile TV, nilipigiwa simu na yule dogo na aliniulizia ufanisi ya TV.

Wenzetu biashara wana wazoesha watoto wao tangia mashuleni. Wakati sisi waswahili kipindi cha likizo tukienda tuisheni mchikichini ili kupanga mabanda mitihani ya taifa. Waswahili tukimaliza vyuoni ndo tuna tembeza CVs na mavyeti.

Na bado hatujashtuka!
 
Uhuru wa kweli upo kaburini. Elimu inakupa upana wa ufahamu, kujiongeza. Mtu anaweza hataki kujiajiri.lakini kwenye ajira yake ana fursa za kupiga side hustle za kutosha.
Mfano mtu wa kukopesha bank. anaweza akaungana na wanasheria akawa analengesha Dili za kupiga muhuri wa mwanasheria. Form 20 au 10. Akipiga watu 15 kwa siku. Kwa mwezi ana hela nzito kuliko yule ambaye amejiajiri
Wengi waliojiajiri, msukumo si pesa tu, bali kuwa huru wa kutokutumwa tumwa n.k
 
Back
Top Bottom