Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,894
Najua naweza kuwa naudhi wengi lakini pia nadhani JF is where we dare , baada ya uchaguzi mkuu mwaka ule nakumbuka KAFU waliporwa ushindi na watu walikufa chini ya uongozi wa Mkapa .KAFU waliendelea kupiga kelele sana na walikuwa na point wakati ule , lakini kwa mshangao dakitari wa sheria bwana Mwakyembe ambaye leo anasema ni mzalendo alisimama na kuishauri serikali kumkamata Seif Sharrif na kumweka rumande na afunguliwe mashitaka ya uhaini .Baada ya siku chache Mwakyembe nadhani aliukwaa Ubunge wa EA .Wakati na sasa tofauti yake nini ? Upi uzalendo zaidi ? watu kufa na tena kwa kudai haki yao ya kuporwa kura zao ama leo kulia na mafisadi ndani Chama chake ambacho kilifisadi kura za watanzania wa kule visiwani na yeye hakuona huruma alishiriki ufisadi ule in a way na hakujali hatma ya Tanzania yangu ? Leo etu anaitwa hero ? Mnisaidie kuelewa hili jamani mie bado siamini na sijajua kwa nini Mwakyembe alitoa kauli ile na kumtaka Mkapa amkamate Seif kama mhaini .