Mwaka ule ikuwaje Mwakyembe akatamka haya?

Kigogo,

Si baadhi ya Wapemba, viongozi wa CUF, wanaodai kuwa wananyanyaswa nchini na wanakimbilia Kenya (Shimoni) na Uingereza (mpaka Waingereza wameweka ngumu viza zao kwa Watanzania!) kwamba wananyanyaswa na Tanzania hakukaliki? Lakini hao ni waongo kwa sababu wangenyanyaswa mpaka kujifanya wakimbizi, wangekubalika kuishi Unguja na Bara na kuwa na vitega uchumi vyao kibao? That is the connection between KUNYANYASWA na VITEGAUCHUMI. Kweli, kama alivyosema Dk. Mwakyembe, Seif angekamatwa. Ni mhaini tu! Alimfitini mzee Jumbe kuwa alitaka kuuvunja Muungano, mpaka Mzee Jumbe akatimuliwa enzi za Nyerere 1984; akamfitini marehemu Mzee Abdulwakil, mpaka akatimuliwa Seif mwenyewe kutoka CCM! Sasa yeye ndiyo yuko mstari wa mbele kupinga Muungano! Aliyesababisha vifo vya Pemba ni aliyechochea maandamano ya kuvamia kituo cha Polisi Pemba, yeye mwenyewe akiwa hayupo maandamanoni! Mwakyembe alikuwa sahihi, kwa level yoyote aliyokuwa nayo wakati huo, aliposema kuwa Seif ni mhaini na alistahili kukamatwa! Msisahau historia na mambo yalivyotokea, jamani!

Bwassa
 
Back
Top Bottom