Mwaka Mpya na Maisha Mapya... Ooh, Glory to God!

Ms Judith

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
2,563
918
wapendwa,

nnatumaini mnakumbuka vizuri thread yangu hii hapo chini:

https://www.jamiiforums.com/mahusia...0-nzito-za-maisha-yangu-ooh-glory-to-god.html

kwa sasa niko safarini kurudi dar. safari hii ni ya pekee kwangu kwa sababu huko dar pamoja na mambo mengine, nitayahitimisha rasmi maisha yangu ya sasa na kuanza maisha mapya kabisa ya ndoa.

sasa huu ndio wakati ambao mchakato wotw ule unafikia hitimisho kwa ndoa itakayofungwa katikati ya mwezi huu. awali nilitegemea ingefungwa mapema zaidi ila kuna mambo yaliingilia hapo kati na tukalazimika kuisogeza mbele.

nawashukuru wote mnaendelea kuniombea na kwa kweli bado nahitaji maombi yenu ili tukio hili likamilike salama na pia tuendelee kuombeana kwa maisha salama na matulivu ndani ya ndoa.

nawashukuru sana kwa yote na kuwatakia kila la heri katika mwaka huu 2012, tuzidi kuombeana bila kuchoka.

Mungu awabariki sana wapendwa

Glory to God!
 
wow wow Judith,Im happy 4 u.
Nakutakia kila la kheri,ndoa ni tamu sanaaa asikwambie mtu,hongera kwa hatua ulizofikia na Mungu akamilishe yote bila vikwazo.
 
ayaaaaa.................. yaani na hesabu zote zile nilizokupigia nimekukosa????................ dah!...................... haya bana, kila la heri................... niachie hata shoga yako basi asee, mi hata mchumba wa kuzugia mtaani tu sina!...................
 
Miss Judith Mungu akutangulie mpendwa,hatua unayoiendea ni ya ushindi sana,kila la kheri
 
ayaaaaa.................. yaani na hesabu zote zile nilizokupigia nimekukosa????................ dah!...................... haya bana, kila la heri................... niachie hata shoga yako basi asee, mi hata mchumba wa kuzugia mtaani tu sina!...................

Jamani we mtu ulipotea hadi nikakusahau,mwee,wapi pearl?
 
Hongera sana Miss. Judith,
Mungu awajalie amani, furaha, upendo wa milele katika ndoa yako.
 
Jamani we mtu ulipotea hadi nikakusahau,mwee,wapi pearl?

duh, we mutu cheusi una kumbukumbu ni balaa!!!........................jamani Lulu wangu mie!! ...................kwa kweli nitakunywa sumu juu yake!! ..................... aisee, Pearl mzima kabisa, itabidi nimwambie apite hapa asome mwenyewe manake ni long time...................... dah, JF safi sana..................ilinisaidia sana...................... yaani mtoto kama malaika!!.................. watu walipigana vikumbo weeee, mwenye akili zake kichwani nikajinyakulia taaaaarrrttiiiiiiiiib kabisa................ tena bila jasho ...................... teh teh......................

si tuko hapahapa dar bana ....................yale mambo yetu yalikwenda swaaafi kabisa na sasa tunakula bata tu mtoto Lulu................. karibu siku moja bana uone na yale maendeleo mengine ya akina mama teh teh..........................na wewe hongera sana mwaya, naona hapo kwenye avatar kitu kishakuchanganyia......................... mzee anastahili nishani kwa kweli..................... happy new year 2012...................
 
Kila la kheri, Miss Judith, nakutakia mafanikio mema ktk ndoa yako tarajiwa. Mungu awe nawe daima.
Amin.
 
mkuu BAK................. kibao kikali sana hicho.................... thanks, nimesuuzika .............
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom