Ninawashukuru watu hawa kabla mwaka huu kuisha.

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
18,586
50,683
Habari ya wakati huu watu wangu wa nguvu..ninatumia kila mmoja wetu yuko salama kabisa..Kwa mlio hospitali basi ninaachilia roho ya uponyaji mkapate kupona mapema(ukiamini utaokolewa)

Haya twende kazi.😊
Unajua bhana kwenye maisha kuna watu wanaweza kuja Kwa mara moja na kuondoka pindi lengo linapotimia..na kuna wengine wanakaa kabisa na mnakuwa ndugu.

Kuna watu waliingia/wameingia kwenye maisha yangu na kwa namna moja au nyingine wamefanyika kuwa msaada.

1.MUNGU.
Siwezi elezea ukuu wake kwangu.kuna wakati nilipoteza watu lakini Mungu akanena nami “hey mwanangu mimi sijakuacha..ongeza Imani”

2.WAZAZI WANGU.
Hawa ni Mungu wa pili duniani ninazidi kuwaombea uzima na afya wa endelea kuona matunda ya mtoto wao.ninahidi kuwafanyia mazuri zaidi Kwa kadri nitakavyojaliwa.ninawapenda sana.

3.BABA WATOTO WANGU.
Yes sijakosea kuandika ni baba watoto kweli lakini Kwa bahati mbaya au nzuri hatuko pamoja na wala hatuwezi kuwa pamoja.Mungu aendelee kuibariki ndoa yake yeye na mkewe.🙏.huyu mwamba bhana alinitoa from nothing to something siwezi kuelezea zaidi.ingawa hatuko pamoja lakini hainizuii kuuelezea ukuu wa huyu mtu(nitakuwa sina fadhila)
Kuna watu hapa watakuja kusema mbona sasa hukuoana nae?labda tu niseme mambo ya mahusiano ni mengi sana Siwezi kuyaelezea hapa😊.ninamshukuru sana Kwa zawadi ya watoto na kunionyesha maisha..hapa nilipo sasa hivi ni matokeo ya miaka 14 iliyopita baada ya kukutana nae.tulikuwa pamoja lakini kila mtu akashika njia yake.yapata miaka 8 au tisa.sasa ni mume wa mtu.

Yeye na mke wake wamefanyika kuwa msaada mno.ninamuombea mno mkewe Mungu aendelee kumtunza na kumpa uhai.kuna raia zitanishangaa sana hapa😃yes shangaeni tu lakini huyu mdada anamsaada mkubwa sana.Hajui ninamuwazia mema sana na mengi mazuri lakini kubwa zaidi ni kuwa sitokuja kumuumiza Kwa namna yoyote ya kutoka kimapenzi na mumewe(baba watoto wangu).ilichukua miaka kadhaa kuutengeza huu upendo ninaouelezea leo.
Maombi yangu juu yao ni upendo na Amani viendelee .na watoto Mungu aendelee kuwatunza ingawa kuna wakati wananitandikaga maswali😄😄mama..”where is your husband “nilistuka sana siku hiyo maana sikuwahi kufikiri mtoto wa chini ya miaka 10 atakuja kuniuliza swali kama hili😌😌.siku ikitokea nikapata husband basi nitaplay voice note on my wedding..I promise this.


4.M(huyu ni mwanamke)

Si ndugu yangu..alikuwa ni mfanyakazi mwenzangu muda kidogo lakini sana amekuwa mtu wangu wa karibu.amenifundisha mengi mno katika maisha🙏
Mimi na yeye tukikaa pamoja nikuongelea ishu za namna ya kupata pesa tu😄😄ingawa mpka sasa bado hatujazipata😄😄mama tuendelee kuwa na mikakati ipo siku tutazipata.
Tulikuwa tukiongea kila mara tukutanapo bado yanaishi ndani yangu,ninaimani hata yangu yanaishi ndani yako.🥰


5.H (huyu pia ni mwanamke)
Aise huyu mwana tulikuwa tunafanya nae kazi lakini yeye aliacha kazi akaenda sehemu nyingine.huyu dada Siwezi kumsahau katika maisha yangu..alinishika mkono pakubwa mnooo…Mungu ambariki.kuna kipindi nilienda kufanya kazi sehemu fulani na sikuwa na mtu yeyote ninaefahamiana nae isipokuwa yeye lakini pia hatukuwahi kuwa marafiki wala na ukaribu wowote..mwanzo aligoma nisikae kwake Kwa kuwa alikuwa akiishi na boyfriend wake kuhofia pengine ninaweza kumtonesha majeraha yaliyopita(rafiki Yake kipenzi alimvhukulia mchumba wake akaenda kuolewa 🇺🇸)so sad.
Nilimuahidi sitomuumiza Kwa namna yoyote😌hakuniamini ingawa alinipa hifadhi😊😊baadae sana alikuja kuniamini 😍😍
Sasa sio marafiki tena Bali ni ndugu na familia zetu zinafahamiana.Ninampenda kuliko kawaida huyu phaller aise 💞💞anahuruma mno ila ukizingua tu😄😄😄akili Yake anaijua mwenyewe.
We phaller najua utapita huku kimya kimya jua ninakupenda kinyama💕💕ila we mjinga upunguze kunywa gambe 😄😄😄


6.M(huyu ni mwanaume)
Hakuna mwaka nilipitia magumu kama mwaka 2020 aise.uwiiii Mungu huyu hawezi kukupa jaribu pasipo na mlango wa kutokea.
Huyu mwamba Sijui alitokea wapi jamani aise alifanyika kuwa njia kwa kiwango cha ajabu mno..ingawa Kwa mkewe haikuwa rahisi kunielewa lakini mwisho wa siku Ali muelewa mumewe.ninawashukuru mno yeye pamoja na mkewe.Mungu ni mwema mno aise..tumekuwa familia sasa.
Ingawa kuna kazi nilimpa juzi akaleta miyeyusho kishenzi 😄😄nilikasirika….vijitu vifupi na hasira ni pua na mdomo 🤣🤣🤣.alizingua kinyama ila haitakuja kubadilisha mema Yake kwangu😊😊.Mungu azidi kuwatumia hata Kwa watu wengine.

7.C(huyu ni mwanaume pia)
Ananiita mwanangu yes ni mwanae ingawa nafikiri kiumri amenipita miaka miwili aise huyu masta…sijawahi kuhitaji msaada kwake nikakosa ingawa najua kuna wakati nilikuwa nikimpa majukumu makubwa lakini hakuwahi kuonesha kuchukia au kunichoka..kuna watu wanamioyo jamani.binafsi Nina moyo wa kusaidia watu lakini Kwa huyu mwamba..alinipandikiza mbegu ya kuendelea kusaidia watu hata kama kuna wengine walikujeruhi baada ya kuwasaidia.Mungu amtunze yeye,mke wake pamoja na mtoto.mwaka jana alibahatika kupata mtoto wa kiume.ninaimani atakuwa na roho ya upendo kama baba yake 😃😄.
Tumekuwa ndugu sasa yeye na familia yetu.mamamdogo,bamdogo,aunt,mjomba na baadhi ya ndugu wanafahamiana.Mungu ni mwema kila wakati.

:nilisema siku nikija kufanikiwa hawa watu sitokuja kuwasahau kabisa lazima nirudi kuwaambia Asante.kila mmoja Kwa wakati wake alinivusha katika giza totoro.Mungu awabariki kila waingiapo na kilawatokapo.Kwa asilimia fulani yes mikono yangu si mitupu na Asante nimeshaanza kuzitoa

Wengi wako huku Jf(isipokuwa wazazi)na ninaimani watauona huu uzi ingawa nilishawaambia laivu kila mmoja Kwa wakati wake
Mungu azidi kuwabariki na kuwatunza kila iitwapo leo.Ninawashukuru mno.

Hivi nyie mnaoandikaga simulizi ujasiri wa kuandika vile huwa mnautoleaga wapi??🤣🤣🤣hapa nilipo vidole na kichwa vyote vinauma😄.nimejitahidi sana kufupisha

Xoxo…
Chakorii.
 
Hongera kwa kuwa na moyo wa shukrani. Mungu Atakuzidishia wewe pamoja na binadamu wema hawa waliokushika mkono ulipokuwa na uhitaji.

Ila sijui kwa nini. Ujumbe huu umekaa kama vile wa mtu anayeaga. Anaaga kwenda wapi sijui.


Kaa sana katika maombi mpaka mwezi huu wote uishe
Asante sana daddy ..watu wema bado wapo ingawa ukiwaona Kwa macho huwezi kiwajua Mpaka upate kukaa nao Kwa ukaribu.

Sijui kwanini lakini nimeingiwa na wasiwasi ujue.
Ninategemea kusafiri keshokutwa naomba uniombee SYB nami pia ninajiombea.

Wewe ni mtu wa pili unaniambia nikae sana kwenye maombi☹😒
 
Back
Top Bottom