Mvutano waendelea machimbo ya rubi Dodoma

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125




rubi.jpg
Mfano wa madini aina ya Rubi

Sadick Mtulya
WAKATI Wizara ya Nishati na Madini, ikiwa imetoa leseni ya uchimbaji madini ya rubi, eneo la Mtakanini Winza, wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, uhalali wake umezua utata baada ya kuibuka mvutano wa pande mbili zinazogombea machimbo hayo.

Mvutano huo, unaowahusisha wachimbaji wenye leseni na wasiona na leseni,
unaelezwa kuchochewa na viongozi wa serikali kutokana na kufaidika na machimbo hayo.

“Kuna kila dalili ya kuzuka kwa mauaji katika machimbo haya, tayari wiki iliyopita kulitokea vurugu zilizosabibisha vibanda kuchomwa moto pamoja na gari kuvunjwa kioo,’’ alisema juzi Kamishna msaidizi wa madini kanda ya kati, Manase Mbasha.

Mbasha aliliambia Mwananchi kuwa mvutano huo pia umesababisha
serikali kushindwa kukusanya kodi kutokana na wanaochimba madini hayo, hivi sasa kukosa leseni na kwamba wamekataa kufuata sheria ya madini ya mwaka 1998

“Kwa mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 1998, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2006, inataka mchimbaji yeyote wa madini lazima awe na leseni, pia mtu haruhusiwi kuchimba madini katika eneo la mwingine mwenye leseni.
“Lakini wachimbaji haramu (wasio na leseni) wamevamia eneo hili na hawataki kufuata taratibu na kusababisha serikali kukosa mapato,’’ alisema Mbasha.

Kwa mujibu wa barua yenye kumbukumbu namba DA.75/170/02/98 iliyosainiwa na Kamishna wa Madini, Dk Dalay Kafumu kwenda kwa mkuu wa mkoa huo, ilitoa leseni za uchimbaji mdogo 273 kati ya viwanja 514 vilivyogawiwa kutoka kwa waombaji 1,049.

“Leseni zilizosalia zinaandaliwa kwa ajili ya kutolewa,’’ inasema barua hiyo.

Barua hiyo ambayo nakala yake ilipelekwa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa iliagiza kuondolewa kwa wachimbaji haramu katika eneo hilo.

“Tunakuomba uchukue hatua ili viongozi wa wilaya wazingatie utawala wa sheria kwa kuwaondoa wachimbaji haramu katika maeneo waliomilikishwa ili shughuli za uchimbaji zifanyike kwa kuzingatia sheria za nchi,’’ inasema barua hiyo.

Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili, mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Dari Rwegasira alisema kuwa; “Sijui kinachoendelea, malizana nao, hao waliokuambia.’’ akakata simu.

Jumamosi iliyopita gazeti hili, lilimkariri mkuu wa polisi wilayani humo, Zedekia Makunja akisema kuwa polisi itaendelea kupambana na wachimbaji hao kwa lengo la kuwadhibiti.

Msimamo wake huo ulikuja kufuatia mvutano mkali uliotokea kati ya pande hizo mbili kiasi cha kuwalazimisha polisi kutumia nguvu za ziada, ili kuwaondoa wachimbaji hao.

“Askari wapo kwa ajili ya kulinda amani, hawawezi kurusha risasi bila sababu. Tatizo ni kwamba wachimbaji walikaidi amri na kibaya zaidi walianza kutoa maneno machafu na kuwarushia mawe askari.

“Awali wachimbaji wote wasiokuwa na leseni waliambiwa ama watoke au waungane na wenye leseni, lakini wao walikaidi,’’ alisema Makunja.
Chanzo: Mvutano waendelea machimbo ya rubi Dodoma
 
Lazima serikali iwe na mentality ya kibiashara wajameni. Hivi hii mijitu haijifunzi tu? Hivi karne hii bado hakuna utaratibu wa kueleweka kwene sehemu nyeti kama hizo? Hii mijitu ni mipuuzi sana aisee.
 
Back
Top Bottom