GHIBUU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 4,432
- 3,006
Zanzibar imeungana na nani ? Na chini ya mfumo gani?
Na Laila Abdulla,
Katika makala iliopita, nilizusha swali : Zanzibar imeungana na nani ?.Jibu wazi ni kuwa , Zanzibar haikuungana na Tanzania,April,26,1964,kwavile, tuliona hadi tarehe ile, nchi kwa jina hilo haikuwapo katika ramani ya dunia. Tanganyika ilioungana na Zanzibar tarehe hiyo,ilifutwa na kutoweka kwa kanuni yaani -decree-alioitunga Mwalimu Nyerere mara tu baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri hiyo mpya. Hiyo,ilikuwa ndio kanuni yake ya kwanza kuipitisha kama Rais wa Muungano.
Mwalimu Nyerere, alifahamika kuwa tayari kuchelewesha uhuru wa Tanganyika ili nchi zote 4 za Afrika Mashariki:Kenya,Uganda,Tanganyika na Zanzibar, zijiunge na Shirikisho la Afrika Mashariki.
SWALI:
Laiti ndoto hiyo ingetimilia na haingetiwa munda na mzee Kenyatta wa Kenya, je, Mwalimu angeliifuta Tanganyika katika ramani ya dunia kama alivyoifuta siku ilipozaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?
Inafahamika kuwa ,Marekani na washirika wake wa Kambi ya Magharibi hasa Uingereza na Ujerumani Magharibi-FRG- hazikupendezwa na upepo uliokuwa ukivuma kisiwani Zanzibar kama vile kuanzisha uhusiano wa kibalozi na China ya kikominist,Urusi,Ujerumani Mashariki na Cuba. Waziri wa nje wa Marekani, Dean Rusk,aliwati shindo Marsi Kenyatta,Obote na Nyerere, kuchukua hatua dhidi ya kile alichokiita "communist menance in Zanzibar" – ushawishi wa kikoministi visiwani Zanzibar alioiita "Cuba of East Africa"-Cuba ya Afrika Mashariki.
Mwalimu akiitikia mwito huo, alivaa njuga kuyazima mapinduzi ya Zanzibar .Katika ziara pekee Zanzibar, April,1964, Rais Kenyatta alifika Uwanja wa Ndege kwa mazungumzo na Sheikh Karume lakini, aliishia hapo tu na baadae kurdi Kenya.
Obote, Rais wa Uganda, alikuwa tayari kwa shirikisho.Mwalimu ndie alieshika bendera. Alikuwa hata tayari kwa muujibu wa taarifa, kumuachia mzee Kenyatta urais.Sielewi kwanini hata hivyo,mzee Kenyatta alikataa mpango wa shirikisho la Afrika Mashariki na kuhiyari Kenya ifuate mkondo wake pekee.Je, hakumuamini Mwalimu?
Shabaha ilikua dola kuu 3 za Afrika ya Mashariki-Kenya,Uganda na Tanganyika kuidhbiti Zanzibar na kuyazima mapinduzi yake pamoja na kuzuwia Zanzibar kuendelea kuwa Mecca ya Afrika Mashariki ya kueneza UISLAMU.. Marekani,Uingwereza na hata Ujerumani Magharibi iliokasirishwa kwa Zanibar kuitambua (GDR) au Ujerumani Mashariki,hazikutaka kuona Cuba ya Afrika Mashariki ambayo mwaka 1 baadae ilikua kumpokea Che Guevera katika maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa mapinduzi hapo Januari, 1965 kabla hajaelekea Kongo (D.R.C) kupitia Tanzania-bara.
Mwalimu akawaambia Marekani ana Karata nyengine :Vipi kudhibiti mambo Zanzibar. Karata yenyewe, ni MUUNGANO kati ya Tanganyika na Zanzibar na Marekani ikatoa baraka zake. Tanganyika kubwa yenye wakaazi milioni 20 wakati ule kuidhibiti Zanzibar iliokua na wakaazi laki 5. Nkurumah, alimkosoa Mwalimu kwa kusaidia kuyazima mapinduzi ya Zanzibar.
Tarehe 18,April,1964 akamwita mzee Karume aende Dar-es-salaam kwa mazungumzo.Sielewi, Mwalimu alimtikisa mzee Karume kiasi gani siku hiyo,kwani, hakurudi Zanzibar kama ilivyopangwa siku ile na akalala Dar hadi siku ya pili yake April, 19,1964.
Tarehe 22 April, washirika 2 wakubwa wa mzee Karume wakiwa nje ya Zanzibar- Abdulrahman Babu ( waziri wa nje na biashara) akiwa Indonesia kwa ziara rasmi na Sheikh Aboud Jumbe ,waziri wa ndani akiwa kisiwani Pemba kwa maswali ya usalama,Mwalimu Nyerere alitua Zanzibar na hati ya "MUUNGANO". Jumbe anaeleza katika kitabu chake "The Partner-ship" ndege yake ikitua Zanzibar ile ya Mwalimu ikiruka kurudi Dar. Mzee Karume alinyimwa washauri wake wakubwa na wasomi-Babu na Jumbe.
Sisi Wazanzibari, kila JANUARI 12, tangu 1964, tunasherehekea "mapinduzi" na tunaiita serikali yetu hata hii ya leo ya "UMOJA WA TAIFA" inayotuunganisha sote, "serikali ya Mapinduzi" bila ya kufahamu kuwa,MUUNGANO ulipikwa kama jungu la kuyaua mapinduzi.Sababu ni kuwa, mkondo wa mapinduzi ya Zanzibar haukuipendeza Marekani na washirika wake wa Magharibi.Kumbuka wiki tu baada ya mapinduzi ya Zanzibar, hapo Januari 20, Jeshi la Tanganyika nalo liliasi na Mwalimu akaenda kujificha.Jeshi la Kenya na hata la Uganda yakafuata.Kidole kilinyoshewa Zanzibar.Mwalimu alirudishwa madarakani na majeshi ya Uingereza yaliozima uasi. Ni majeshi ya serikali ile ile iliomkatalia msaada Sultani huko Zanzibar.
Mzee Karume, hakuridhia MUUNGANO kwa hiyari kinyume na hekaya nyingi tunazosikia.Ni dhahiri kuwa, April 18,1964, alitikiswa mno kule Dar-essalaam. Mwalimu yasemekana ,alitishia kuondoa askari wake kiasi 300 aliowaleta Zanzibar kuimarisha mapinduzi bila ya hata kuwapo Makubaliano ya Kimataifa kufanya hivyo. Na Mwalimu angefunga mapatano hayo na serikali gani ,ile ya Sultani ? Mzee Karume, alitaka kulinda usalama wa serikli yake kutokana na vitisho vya manuwari za Marekani, zilizokuwa zikizunguka Bahari ya Hindi wakati ule.
Mzee Karume, hakuwa na haki ya kuiunganisha Zanzibar bila ya ridhaa ya Wazanzibari ambao hadi leo miaka 47 baadae,hawakuulizwa wanataka Muungano au hawataki na serikali ya Tanzania haithubutu kuwauliza. Zanzibar si shamba lake binafsi mzee Karume bali ni mali ya wazanzibari na wala si mali ya ASP au CCM Zanzibar. Lakini, kutokana na hali ya mambo , Karume alihisi bora nusu-shari kuliko shari kamili. Mmoja aliekuwa karibu nae sana mzee Karume,aliwahi kuninon'goneza usia aliowapa "wandani wake" wa Afro-shirazi party: Aliwausia wasiregeze kamba katika mawasili 3 kwa Tanzania- bara:
Rais aliemfuatia- Sheikh Aboud Jumbe,aliregeza kamba na laiti hangeunganisha chama ASP na TANU,Mwalimu Nyerere , asingeweza kumuuzulu kule Dodoma, 1984.Jumbe, angelimzindua Mwalimu ambae wakati ule ndie kinara wa CCM -supreme. Jumbe, amesoma na kuelimika,lakini Karume alionesha busara.
Kuna taarifa kuwa mwaka kabla kuwawa kwa Karume,hakujakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja baina yake na Mwalimu bali kupitia wajumbe kama Bohke Munanke. Sijui nini ingelikuwa hatima ya MUUNGANO huu bila ya Tanganyika ,laiti mzee Karume angelikuwa hadi leo yuhai?
MFUMO WA MUUNGANO NI UPI ?
Wakati mzee Karume alitumia busara kubakisha mihimili ile 3 ya dola mikononi mwa Zanzibar,Rais Aboud Jumbe, msomi,hakukawia kutambua makosa yake na haraka akataka kurekebisha makosa. Kupitia mawakili wake- Wolfgang Dourado na Swanzi, (Mghana) Jumbe, alimkumbusha Mwalimu kuwa ,MFUMO wa MUUNGANO wetu ni wa aina ya "Shirikisho".
Na tafsiri ya "Shirikisho" ni unakuwa na shina ( centre) na Tawi ( constituency) na madaraka ya kila upande, hufafananuliwa wazi ili kila mmoja, asimuingilie mwenziwe katika mambo yake.(Ya MUUNGANO NA YSIO MUUNGANO). Sasa ukiunda CHOMBO cha 3-yaani chama na kukifanya kina kauli ya mwisho "supreme", basi unakuwa umevunja Mapatano ya MUUNGANO au (Articles of the Union ). Mwalimu akatanabahi hawezi kushinda mbele ya wanasheria.
Dourado aliwahi kudai eti Mwalimu ni mwepesi wa kuwachezea akili wanasiasa ,lakini hudunda kwa wanasheria.Hoja yake ikawa nguvu za dola: kuwatia korokoroni wanasheria wa Jumbe : Dourado na Swanzi. Hatima ya Jumbe, ilijulikana Dodoma,1984 alipouzuliwa na kutoruhusiwa kurudi Zanzibar. Swali langu linabaki lile lile:
KIONGOZI GANI ATAIBUKA ZANZIBAR KUMVIKA PAKA KENGELE na kuwazindua wenzetu wa Tanzania-bara kwamba, Zanzibar haikubadilisha "SULTANI wa kiarabu" kwa "SULTANI wa Dodoma"?
Bila ya Tanganyika, hakuna Muungano,kwani haingii akilini mwa wazanzibari na hata watanganyika wenye kuwaza na kufikiri kuwa , siku ya kuzaliwa mtoto -Tanzania- April,26,1964 ,kwa kiini macho cha kuchanganya udongo, mzee mmoja kati ya 2-Tanganyika, anafariki dunia?
Zanzibar bila ya Tanganyika hapo imeungana na nani wenzetu?
SULUHISHO LIWAPI?
Suluhisho ni kuifufua Tanganyika na kuunda Muungano mpya wa serikali 3 na unaokubalika au kama ilivyopangwa awali na waasisi. Mfumo ni shirikisho, ndoto ya awali ya Mwalimu Nyerere alioachana nayo akishika njia ya "UNITARY STATE"-nchi moja. Lakini, Mwalimu aliwakemea wabunge 55 waliodai serikali ya Tanganyika na aliwaambia kwamba, kwa "CCM haiingii akilini kutoka serikali 2 kwenda 3." Wazanzibari wanamwambia na wao "haiingii akilini kutoka serikali 2 kwenda 1,kwani, kuridhia hivyo, ni kujitia kitanzi dola ya Zanzibar.
Kwa CCM-Zanzibar (zamani ASP) wakati wa kuchagua umewadia: ina jukumu kubwa kwa Zanzibar :ama kuachana na sera ya CCM-bara (ambayo waziri mzalendo Mansour Himidi, ameshasema ni butu) ya serikali 2 kwendea 1 au kushikamana na sera hiyo na Kuihini Zanzibar na vizazi vyake vijavyo . Historia hapo itawahukumu ni "MAHAINI" wa Zanzibar.Sidhani viongozi wa CCM- Zanzibar, wangependa kuingia katika historia na doa hilo. Kwani, NANI ANGEPENDA KUMKHINI MAMA YAKE MZAZI?
View attachment 34549

- Msiunganishe Jeshi
- Msiunganishe fedha (sio sarafu bali akiba ya Zanzibar na muulizeni Jamali aliemuita "chori wee alipomuendea kwa swali hilo".
- Msiunganishe chama-yaani ASP kuungana na TANU.