Muungano wa Serikali 3 ni bora Sana

Mkuu Nguruvi3

Hii tuhuma imetolewa sana na Wazenj kuwa Tanganyika imejigeuza jina tu na kujiita Tanganyika. Leo umelithibitisha hilo.
Kama ni kweli hili ulisemalo basi yapasa tuwaombe radhi wazenj kwa kuwafanyia hadaa.

Halafu inakuwaje tena, tutake serikali moja?

Kama Tanganyika ilijibadilisha jina tu basi mkuu Nguruvi3 hata kama na mimi ningekuwa Mzanzibari basi nisingejiita mtanzania.
Kwa maneno uliyoyaandika hapa, mtanzania ni mtanganyika.

Mkuu leo umethibitisha ukiini macho wa Muungano.

Yaani Tanganyika haijafa wala serikali ya Tanganyika haijafa. Hili nalo neno!!!

Haya wamekusikia?

Mkuu unajua maana ya ulaghai? hadaa? Vipi utafanya biashara kihadaa hadaa halafu useme unapata hasara?

Leo, mkuu naona umeamua kuimwaga siri hadharani.

Tanganyika haikufa wala serikali ya Tanganyika haikufa!!!??? Ila ilibadili jina tu. Duhhh!!! Hii kiboko, kwa hiyo kwa miaka 48 ni usanii tu na mazingaombwe. Sasa napata idea kwa nini UAMSHO na wazanzibari wanapiga kelele siku zote.

Kama ni hivyo, maana yake hakuna Muungano au haujawahi kuwepo muungano. Ni usanii kwenda mbele na mazingaombwe tu.

Pasco alipokuja na mada yake ya ratification naona aliekewa mkwara wa nguvu.

Kuna la ziada Mkuu Nguruvi3 ambalo unataka kulisema kutuelimisha zaidi? Masikio yetu yako tayari kupokea darsa. Funguka mkuu.
Usisome juu juu nimeandika nikiwa 'sober'. Tanganyika ni sleeping general kwasababu ili uwe na muungano lazima uwe na vitu viwili au zaidi. Kwa vile tuna muungano basi Tanganyika ipo na Zanzibar ipo.
Kwa walioanzisha muungano waliacha Zbar na madaraka yake kuchelea kuonekana imefutwa na Tanganyika.
In other words Tanganyika is recessive unlike Zanzibar which is predorminant.

Hoja hiyo ni kujibu kuwa Tanganyika haijafa kama mnavyosema ila siyo dorminant kwasababu ya Tanzania.
Niliposema kile cha Tanganyika kiwe cha Tanzania nilikuwa na maana ile ile ya cha ZNZ kiwe cha Tanzani. Lakini ukweli usiohitaji kuhitimu darasa la 4C upo wazi kuwa utamuombaje mtu asiye nacho akupe kisichokuwepo?

Nikupe mfano, Elimu ya juu si jambo la muungano, lakini likasemwa liwe la muungano ili Kumsaidia Mzanzibar.
Ni kutokana na hilo ndiyo Maana Mzanzibar yoyote mwenye elimu kasomea bara, kuanzia Maalimu Seif Jussa na wengine walioandikishwa jana(vijukuu).

Nishati siyo muungano lakini Tanganyika ikasema kile cha Tanganyika kiwe cha Tanzania, ndipo ukaona umeme wa bure unavuka kwenda Zanzibar. ZNZ haikutoa au kuwekeza hata senti tano juu ya gharama hizo. Pamoja hayo, kuanzia akina Jumbe hadi Wajuu , vitukuu na vilembwe hakuna anayejua bei ya umeme duniani ni mpaka atoke nje ya ZNZ.
Sababu kubwa ni kuwa cha Tanganyika ni cha Tanzania iliyo na Zanzibar

In short kile cha Tanganyika kilichofanywa kuwa cha Tanzania ni kwa faida ya mzanzibar kwasababu ZNZ haina cha kutoa. Nonda huo ni ukweli, ni free ride msione kama tusi.

Mtakapoondoka kwa amani na si kukimbizwa na mashoka, nadhani siku si nyingi, mtakwenda bandari kupanda meli na mabegi, Tanzania au Tanganyika au Mzizima itakuwepo pale pale ndiyo tafsiri ya sleeping giant.
 
Natamani mtu achambue option zote tatu kwa faida na hasara halafu JF members wachangie na kisha tuchague ipi itakuwa mfumo bora wa muungano....
 
Tanganyika haikufa wala serikali ya Tanganyika haikufa!!!??? Ila ilibadili jina tu. Duhhh!!! Hii kiboko, kwa hiyo kwa miaka 48 ni usanii tu na mazingaombwe. Sasa napata idea kwa nini UAMSHO na wazanzibari wanapiga kelele siku zote.

Kama ni hivyo, maana yake hakuna Muungano au haujawahi kuwepo muungano. Ni usanii kwenda mbele na mazingaombwe tu.

Pasco alipokuja na mada yake ya ratification naona aliekewa mkwara wa nguvu..
Mkuu Nonda kumbe sometimes huwa unakumbukumbu!.
Pasco
 
Back
Top Bottom