Muungano wa Serikali 3 ni bora Sana

Bajeti ya ZNZ ni bilioni 600, ni ndogo kuliko bajeti ya elimu ya Tanganyika. Sasa 50/50 hawa watatoa nini?

Bajeti ya usalama na ulinzi ya ZNZ hakuna ndio maana wanang'angania serikali 3 au mkataba. Kama ingekuwepo 50/50 ya bajeti ya ulinzi maana yake ni kuwa ZNZ ingetoa bilioni 400 na kubaki na bilioni 200 kama bajeti.

Msisahau kuwa hawa WZNZ wanachukua mishahara kutoka hazina Dar, hawalipi wabunge, BLW ua viongozi wastaafu. Wote wanalipiwa na Tanganyika, sasa ukisema 50/50 itoke wapi? hawana 50 hawa, wanakinga mkono.

Jiulize kwanini wameacha hoja ya kuvunja muungano wamekomalia serikali 3 au mkataba, wanajua kuwa asilimia 60 ya shuguli za serikali yao zinatoka Tanganyika. Fungueni macho Watanganyika, hapa ni kuliwa tu halafu mnatukanwa na kuchomwa moto.

Jiulize, hivi wewe Mtanganyika unataka muungano wa nini, ukusaidie nini? Hawa wanapenda pesa yako wewe kwao ni Kafir tu.
Waacheni waende zao, kwanini hamuioni mbali zaidi ya pua zenu Watanganyika?

Hatimaye umenishawishi na nimekuunga mkono. Ila 2nd option iwe serikali1
 
Nonda, mimi ni mpenzi wa Pan Africanism nikiamini kuwa mpaka wa Kenya na Tanzania ni hypothetical kwasababu hakuna alama.

Niliwahi kuishi maeneo ya Tarakea na Mjasani Tanga, sikuwahi kuona tofauti yoyote nikiwa upande mwingine
serikali 3 mimi nilimuunga mkono kwa wakati huo na mazingira ya nayakati zile.
Hoja ya Nyerere niliikubali kwa wakati ule na mazingira yale.

Kutokana na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kiutamadni duniani, sioni sababu ya muhimu ya kuwa na muungano unakuwa mateso na adha kwa pande zote. Lakini kinachonisukuma sana kuona kuwa hatuna sababu ya kuwa na muungano na ZNZ ni ukweli kuwa wenzetu wamejenga chuki ya dhati dhidi yetu. .....

Tukuatane UN, EAC, SADC, FIFA, IOLYMP, WBO, n.k. Huko tutakuwa na misimamo ya pamoja kwasababu tunatoka kanda moja na tunaweza kuongea kiswali kuwazuga wasiojua. Tukitoka nje, kila mtu na lake.

Usinilaumu mimi kusema ukweli,walaumu WZNZ waliojenga chuki ya dhati mioyoni mwao dhidi ya Mtanganyika hadi kufikia mahali pa kuona ya kuwa kumtoa roho Mtanganyika ni rahisi kuliko kupata dumu la petroli.
Ya kwamba huyu ni Mtanganyika, kafir, malaya, jambazi ambaye hafai kuishi ZNZ. Hii ndiyo imetufikisha hapa.
Fikiria chuki hiyo itakapokuwa reciprocated nini kitatokea? kabla haijatokea LET ZNZ GO PEACEFULLY

Nguruvi3

Bado wewe ni mshabiki wa Pan Africanism?

Kama ndio, basi rai ya Mwalimu ya serikali mbili ya Tanganyika na ya Zanzibar ndio itatupeleka huko EAC na EA federation na kupiga hatua ya juu kidogo( mbele) katika umajumui wa Kiafrika.

Wakati Azimio la Zanzibar linapitishwa ambalo liliua azimio la Arusha, Mwalimu Nyerere alikuwa hai bado, nafikiri hilo lilipelekea pia katika kutoa rai yake hiyo kiaina kama umeshindwa kutafsiri rai yake.

Bila shaka Serikali ya Tanganyika itajiunga EAC na serikali ya Zanzibar itajiunga EAC kama entities zinazojitegemea. Kwani nani anakuwa mwanachama EAC? Kwa hiyo Mwalimu alitoa idhini ya kuunda upya/ kuundua Muungano.

Nini hapo usichokifahamu?

Lawama ya kujisemea "vineno" ambavyo vitasaidia kujenga chuki katika jamii iende na ielekezwe kwa kila mmoja wetu ambaye anachochea mzuka. Huchukui kidumu cha petroli kukimimina pale palipo na moto tayari ukitegemea kuwa unasaidia kuuzima moto huo.

Kuna mwakilishi ,habari imeletwa hapa JF, kuwa ni "kafir" lakini amechaguliwa huko Zanzibar kuingia baraza la wawakilishi. Kulikuza hili na kuanzisha/ kuzifufufua hizi za mwarabu, mtwana unajibebesha jukumu ambalo utalijutia siku likiripuka.

Mkuu Nguruvi3 una busara ya kutosha kuweza kuzima / kuzidhibiti hisia / hasira zako kwa wapiga kelele na kusaidia kuondoa mazingaombwe ya Muungano. Tunaweza kuazima utaalamu wa madakatari wanaofanya upasuaji kuondoa maradhi kwa kupiga sindano ya ganzi.

Tusaidie mgonjwa apoe kwa kupunguza maumivu na machungu kwa upeo wa mwisho wa uwezo wetu, hata kama ni kumkata kiungo kama hiyo ndio tiba yake..Nia au lengo ni kuhakikisha baada ya yote kutokea basi inaibuka Malaysia na Singapore zilizo na neema.Hili linawezekana.

Hoja zako zinatosha kuwaongezeo upeo wa kuona mbali walengwa bila kuamsha mzuka na wakishafahamu hayo mazingaombwe watadai kile ambacho unawashawishi wadai.

Usichukulie kuwa nakulaumu kwa kusema ukweli, la....chagua njia nzuri tu ya kusema ukweli wenyewe. Ni ushauri tu.
 
Nonda,
Huu wa kwetu hauwezekani kwanini wenzetu mnang'anga'ania huko. Kwanini tusikiutane kama nchi tofauti.
Kwanini mnataka kuwa na Tanganyika kimkataba au serikali 3. Kuna kitu gani?

Pan Africanism inaweza kuwa through SADC, EAC, ECOWAS n.k

Maalimu kasema ZNZ ipewe kiti UN, sasa kuna nini kimebaki mnachodhani tunaweza kushirikiana. Bendera, wimbo wa taifa, taasisi kama ZMO, baraza la mitihani n.k.

Labda kuna kitu sikielewi tushirikiane nini tena maana hatuna cha kushirikiana.
Halfu sheikh, WZNZ wanaitaka ZNZ ya mwaka 1963 sasa wawe bado unang'angania muwe na Tanganyika huoni huo ni uslaliti Maalimu.
 
Nonda,
Huu wa kwetu hauwezekani kwanini wenzetu mnang'anga'ania huko. Kwanini tusikiutane kama nchi tofauti.
Kwanini mnataka kuwa na Tanganyika kimkataba au serikali 3. Kuna kitu gani?

Pan Africanism inaweza kuwa through SADC, EAC, ECOWAS n.k

.
Maalimu Nguruvi3
Soma post #42 mkuu.

Asiyejua maana mkuu haambiwi..........

Ubarikiwe,mkuu
 
Maalimu Nguruvi3
Soma post #42 mkuu.
Asiyejua maana mkuu haambiwi..........Ubarikiwe,mkuu
Nonda, kila mara huwa hujibu ninachokiuliza unazunguka zunguka tu hapo ndipo tulipo kwama. Ukisoma post# 43 nimeuliza maswali yasiyo na uchochezi wala chuki kwa minjaili ya kuelewa.

Hakuna ubishi kuwa muungano wetu na hasa chuki za WZN hauna maana ya muungano tena. Imekuwa ni kero au mazingaombwe. Chuki hiyo imeshavuka bahari na Watanganyika wanajiuliza kuna nini wanachofaidika nacho ndani ya huu muungano?

Soma wanajamvi wote wanauliza muungano unatusaidiaje. WZN wanasema wanataka nchi yao yenye kiti umoja wa mtaifa, EAC n.k. Kila jambo wamejitenga na hakuna wanachotaka tuwe na ushirika isipokuwa kile kinachowasaidia wao na si muungano. Wenzetu wanaweka sheria za kumzuia mhalifu Mtanganyika lakini ni wepesi sana wa kutafuta fursa Tanganyika.

Wakati wanataka kujitenga, kuna kundi limeng'ang'ania tuwe na serikali 3 au mkataba. Hapa panachanganya, kama hatuna vitu common, hizo serikali 3 au mkataba ni wa nini? Kwanini tusitengane tukaishi kama tulivyo na Wakenya?
Lakini wenzetu hawa wa mkataba na tatu hawana hoja ya kuelezea kuwa nini kiwemo katika mkataba au tatu.

Kwa maneno mengine kuna wanachofiicha na hapo hakuna uaminifu, kama hatuaminiani kwanini tuishi kwa mashaka na tusivunje muungano ambao hauna faida ZNZ na hauna faida kabisa Tanganyika zaidi ya hasara.

Nadhani tujadiliane kwa kujibu maswali na kutumia akili zetu, tusiazime mawazo ya watu wengine ili tuweze kufikiri, ni hatari sana kumkabidhi mtu mwingine ubongo wao. Hebu nijibu maswali ya post 43 kwanza.
 
Spendi Ubepari,

Umekuwa mwepesi wa kupiga madongo lakini hoja yako siyo ya msingi ni lazima ujibu swali la msingi Serikali tatu itasaidia vipi kutatua tatizo la lawama za kubaguliwa zinazotoka Zanzibar? Kama unafikiria serikali tatu itatatua tatizo la Muungano una ndoto za mchana!
 
Je! suala la uraisi wa Muungano, litakuwa kwa zamu??????? Miaka 5 raisi atoke upande huu na mitano ijayo atoke upande wa pili????????? Je! mawaziri wa muungano watakuwa 50 kwa 50???????? Je! ajira za idara za muungano zitakuwa 50 kwa 50?????? yaani jwtz 50% watoke bara na 50% visiwani?????? Hapo yakhe tutakuwa wote wanajeshi, sie tutakubalini yakhe!!!!
 
Nonda, ........kwa minjaili ya kuelewa.

Hakuna ubishi kuwa muungano wetu .......hauna maana ya muungano tena. Imekuwa ni kero au mazingaombwe......Watanganyika wanajiuliza kuna nini wanachofaidika nacho ndani ya huu muungano?

Wakati wanataka kujitenga, kuna kundi limeng'ang'ania tuwe na serikali 3 au mkataba. Hapa panachanganya, kama hatuna vitu common, hizo serikali 3 au mkataba ni wa nini? Kwanini tusitengane tukaishi ...?
Lakini wenzetu hawa wa mkataba na tatu hawana hoja ya kuelezea kuwa nini kiwemo katika mkataba au tatu.

Kwa maneno mengine ........kwanini tuishi kwa mashaka na tusivunje muungano ambao hauna faida ZNZ na hauna faida kabisa Tanganyika zaidi ya hasara.
Mkuu Nguvuri3

Nakusoma vyema tu lakini inaonekana umeshindwa kutegua kitendawili cha mwalimu.

Naomba uzipitie hizi.
1. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-moja-nchi-moja-taifa-moja-5.html#post4415616

2. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...cha-zanzibar-un-kirudishwe-4.html#post4439091

3. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...cha-zanzibar-un-kirudishwe-4.html#post4439205

Sasa nikuulize. Wewe unataka Muungano uvunjike? Tuuvunje? Uvunjwe?

Kama jibu ni ndio...Kabla ya muungano kulikuwa na serikali ngapi ? Zipi?

Mwalimu anasema ziwepo serikali ngapi? Zipi?

Maana yake nini?

Au wewe unafahamu serikali moja au tatu hapo?

Bado hutaki kuipigia debe, Tanzania yenye serikali mbili? Ya Tanganyika na ya Zanzibar?

Au unataka tung'ang'anie mazingaombwe?

Mkutano, mashirikiano itakuwa EA federation kama unavyosema ndio itakavyokuwa. Suluhisho rahisi limetolewa na mwenyewe muunda muungano lakini tumekuwa wazito kuelewa.
 
Nonda, sijui niweke maswali yangu vipi ili nieleweke, hata hivyo nadhani hii ni fursa nzuri sana ya kuwaeleza Watanganyika kwanini tuvunje muungano.

Ni fursa nzuri kwasababu Wazanzibar wameng'ang'ania mkataba au serikali 3. Wasichoweza kueleza ni kuwa hizo serikali 3 zishughulikie nini ikiwa kila jambo tumeshatengana na hata yale tunayodhani yanatuunganisha kama mambo ya nje hutayataki tena.

Hatari kubwa ni kuwa Zanzibar itaendelea kudai hata kile isichostahiki. Kwa mfano, wamedai kuwa tume ya katiba iwe na wajumbe sawa kutoka kila upande. Hilo ni sawa, kinachotatiza ni kuwa ZNZ hiyo hiyo haidai mchango sawa wa kuendesha serikali ya muungano, mambo kama ya ulinzi ameachiwa Tanganyika.

Kwa uchache ni kuwa ZNZ inautaka muungano kuliko Tanganyika vinginevyo wasingebaki kutaka serikali 3 au mkataba.
Kwanini wanataka muungano kama wanavyodai
1. Soko kubwa kwa shughuli zao za kijamii lipo Tanganyika
2. Ustawi wa uchumi wa ZNZ unategemea sana Tanganyika.
3, Soko la ajira za WZNZ linategemea Tanganyika
4. Gharama za ulinzi na usalama zinategemea Tanganyika
5. Gharama za kuendesha serikali ya mapinduzi zinategemea Tanganyika
6. Ufinyu wa ardhi ni tishio kwa mustakabali wa ZNZ,ni Tanganyika wala si Kenya au Uganda wanakoweza kupata uhondo walio nao sasa

Katika orodha hiyo hakuna hata kimoja Tanganyika inategemea ZNZ. Kuvunjika kwa muungano ni mateso kwa WZNZ.
Njia gani wanatumia?
1. Kudai mkataba ili yale mambo yatakayowasaidia kama Ardhi, udogo wa bajeti, na nishati kama umeme viendelee kupatikana bure.

2. Serikali 3, ile ya tatu ni ya mambo yanayohusu matatizo ya ZNZ.

Wasichokijua; Kurejea kwa Tanganyika ni kuondoa kila jambo na kila upande uwe sawa kwa kila kitu. Tanganyika haitakubali kuwaajiri zanzibar kama ilivyo sasa wakati Mtanganyika hatapata ajira visiwani kama ilivyo sasa.
MZNZ itabidi aje Tanganyika kama mwekezaji, masikini wasioweza kulipia hata nauli huo ndio mwisho wao.

Kuhusu Nyerere, yeye aliwahi kusema kama ZNZ watasema hawataki muungano hawezi kuwapiga mabomu. Kauli zake zililenga nyakati hizo na hakika wakati umebadilika. WZN hawataki muungano na hakuna haja ya kuwapiga mabomu. Tatizo ni kuwa wamegawanyika, washirazi wakitaka utawala wa sultani na wanyamwezi wakiyataka mapinduzi.

Nonda, ni kitu cha ajabu sana leo tukitumia mawazo ya Nyerere kuhusu muungano. Huyu Nyerere kule ZNZ ni Laanatullah sasa iweje hata uthubutu kuweka mawazo yake? Nyerere ni muasisi wa muungano lakini wapo wenye nchi wanaoamua hatima ya nchi zao, hao ni mimi na wewe kutokana na mazingira tuliyo nayo.

Mazingira tuliyo nayo yanasema kuwa muungano hauna faida kwa pande zote, moja ikionewa na nyingine ikibeba mzigo wa gharama na lawama. lIlilo jema ni kuachana tukiwa na mapenzi kwasababu haitatokea hata siku moja Tanganyika ikaihitaji ZNZ, lakini ZNZ inaihitaji Tanganyika hata leo hii na hilo ndilo chimbuko la serikali 3 au mkataba.
Serikali 3 ni jawabu baya kwa WZNZ na mkataba lazima Tanganyika ielezwe itafaidika na nini?

Nimekusaidia kujibu maswali na nadhani utatumia fikra na siyo link kufikiri.
 
Mkuu Nguruvi3
Napenda unavyopanga mistari.

Ukivunja Muungano utaunda serikali ipi kwa upande wa Tz bara(nchi iliyokufa kwa maelezo ya wengine)?

Zanzibar wataunda serikali ipi?

Sasa tupige debe la Tanzania yenye serikali mbili! Kama Nyerere alivyotoa rai.(baniani m-baya kiatu chake....)
 
we ni mjinga tanganyika tuko mil zaidi ya 40 zanzibar wapo zaiidi ya mil 3 sasa ukisema tugawane 50/50 ni sawa......
Mimi mjinga, ... Hebu unitoe ujinga!. ....Mtoto akililia wembe mpe!. Akihitaji uwakilishi sawa mpe na gharama achangie sawa na wewe! Akishindwa alale mbele. Mzigo wa kuwahudumia wanasiasa na watumishi wengine toka visiwani ni mzigo kwetu!.
 
Mkuu Nguruvi3
Napenda unavyopanga mistari.
Ukivunja Muungano utaunda serikali ipi kwa upande wa Tz bara(nchi iliyokufa kwa maelezo ya wengine)?
Zanzibar wataunda serikali ipi?
Sasa tupige debe la Tanzania yenye serikali mbili! Kama Nyerere alivyotoa rai.(baniani m-baya kiatu chake....)
Nonda, kwasahivi hakuna sababu ya kuwa na serikali 2,3 au mkataba. Tayari Tanganyika na ZNZ zimeshakuwa na mashaka na ule uvumilivu umekwisha. Unapokuta mkurugenzi MZNZ ameachiwa kinoti cha 'Rudi kwenu ZNZ' hapo hamkani si shwari.
Kwahiyo la muhimu ni kutengana na hilo ndilo jibu na mwarobaini.

Kuhusu kufa kwa Tanganyika, hapa kuna kitu kinawasumbua watu wasichokielewa. Nchi si jina. Cambodia inaitwa Campchea, Burma inaitwa Myammar. Congo iliitwa Zaire na sasa Congo na inaweza kuitwa Zaire ikibidi.

Kilichotokea ni kubadilisha jina lakini serikali ya Tanganyika haijafa. Ukisoma katiba utaona huyo aliyechukua jina aliambiwa 'kila kilichokuwa cha Tanganyika kitakuwa cha Tanzania'.
Kwa maneno ya kijeshi ''Tanganyika is a sleeping General''

Hata katika Mazingira tuliyonayo MZNZ anaona aibu sana kuitwa Mtanzania, popote pale alipo. Kazaliwa Dar es Salaam, kasomea Dar mpaka madigrii lakini bado anajisikia dhalili kuitwa Mtanzania, atajitambulisha yeye ni Mzanzibar.
Kujitoa kwa ZNZ kutakuwa na jambo moja tu kubaki na Tanzania kama jina au kurudi Tanganyika.
Jambo zuri ni kuwa tayari kuna experience ya majina na hilo si tatizo.

Ama kwa upande wa ZNZ kutakuwa na tatizo kwasababu adui yao atakuwa hayupo. Namna ya kugawana kitumbua itazingatia mambo mengi. Je, una ndevu za kutosha? ni za katani au makumbaa?
Je, ujaji wako ZNZ ulifuata taratibu? a)Ni Mshirazi mzawa asilia (b) Ni zao la utumwa.
Je, wewe ni muunguja au Mpemba, unayajua na kuyathamini mapinduzi?
n.k. Lakini hilo si tatizo kubwa kwavile uwe na ngozi ya chungu au ya dhahabu wote watakuwa katika nchi ya neeghma!

Fikiria, kwanini ZNZ ina makamu wawili? halafu waangalie kwa uzuuri na kituo! Ukishajua kwanini utakubaliana na maneno yangu hapo juu.

LET ZNZ GO!
Serikali 3 ni mzigo wa misumari na samadi kwenye mgongo wa Mtanganyika
Mkataba, hatuna tunachohitaji ZNZ mkataba wa jambo gani na kwanini
?
 
sasa ni miaka 50 kama muungano una faida kenya na uganda wangeomba kujiunga,,,suluhisho la dhulma hii aloianzisha nyerere ni kila umbape kuchukua ubao wake.
 
Nonda,
Kuhusu kufa kwa Tanganyika, hapa kuna kitu kinawasumbua watu wasichokielewa. Nchi si jina. Cambodia inaitwa Campchea, Burma inaitwa Myammar. Congo iliitwa Zaire na sasa Congo na inaweza kuitwa Zaire ikibidi.

Kilichotokea ni kubadilisha jina lakini serikali ya Tanganyika haijafa. Ukisoma katiba utaona huyo aliyechukua jina aliambiwa 'kila kilichokuwa cha Tanganyika kitakuwa cha Tanzania'.
Kwa maneno ya kijeshi ''Tanganyika is a sleeping General''
Mkuu Nguruvi3

Hii tuhuma imetolewa sana na Wazenj kuwa Tanganyika imejigeuza jina tu na kujiita Tanzania. Leo umelithibitisha hilo.
Kama ni kweli hili ulisemalo basi yapasa tuwaombe radhi wazenj kwa kuwafanyia hadaa.

Halafu inakuwaje tena, tutake serikali moja?

Kama Tanganyika ilijibadilisha jina tu basi mkuu Nguruvi3 hata kama na mimi ningekuwa Mzanzibari basi nisingejiita mtanzania.
Kwa maneno uliyoyaandika hapa, mtanzania ni mtanganyika.

Mkuu leo umethibitisha ukiini macho wa Muungano.

Yaani Tanganyika haijafa wala serikali ya Tanganyika haijafa. Hili nalo neno!!!

Haya wamekusikia?

Mkuu unajua maana ya ulaghai? hadaa? Vipi utafanya biashara kihadaa hadaa halafu useme unapata hasara?

Leo, mkuu naona umeamua kuimwaga siri hadharani.

Tanganyika haikufa wala serikali ya Tanganyika haikufa!!!??? Ila ilibadili jina tu. Duhhh!!! Hii kiboko, kwa hiyo kwa miaka 48 ni usanii tu na mazingaombwe. Sasa napata idea kwa nini UAMSHO na wazanzibari wanapiga kelele siku zote.

Kama ni hivyo, maana yake hakuna Muungano au haujawahi kuwepo muungano. Ni usanii kwenda mbele na mazingaombwe tu.

Pasco alipokuja na mada yake ya ratification naona aliekewa mkwara wa nguvu.

Kuna la ziada Mkuu Nguruvi3 ambalo unataka kulisema kutuelimisha zaidi? Masikio yetu yako tayari kupokea darsa. Funguka mkuu.
 
Nonda, sijui niweke maswali yangu vipi ili nieleweke, hata hivyo nadhani hii ni fursa nzuri sana ya kuwaeleza Watanganyika kwanini tuvunje muungano.

Ni fursa nzuri kwasababu Wazanzibar wameng'ang'ania mkataba au serikali 3. Wasichoweza kueleza ni kuwa hizo serikali 3 zishughulikie nini ikiwa kila jambo tumeshatengana na hata yale tunayodhani yanatuunganisha kama mambo ya nje hutayataki tena.

Hatari kubwa ni kuwa Zanzibar itaendelea kudai hata kile isichostahiki. Kwa mfano, wamedai kuwa tume ya katiba iwe na wajumbe sawa kutoka kila upande. Hilo ni sawa, kinachotatiza ni kuwa ZNZ hiyo hiyo haidai mchango sawa wa kuendesha serikali ya muungano, mambo kama ya ulinzi ameachiwa Tanganyika.

Kwa uchache ni kuwa ZNZ inautaka muungano kuliko Tanganyika vinginevyo wasingebaki kutaka serikali 3 au mkataba.
Kwanini wanataka muungano kama wanavyodai
1. Soko kubwa kwa shughuli zao za kijamii lipo Tanganyika
2. Ustawi wa uchumi wa ZNZ unategemea sana Tanganyika.
3, Soko la ajira za WZNZ linategemea Tanganyika
4. Gharama za ulinzi na usalama zinategemea Tanganyika
5. Gharama za kuendesha serikali ya mapinduzi zinategemea Tanganyika
6. Ufinyu wa ardhi ni tishio kwa mustakabali wa ZNZ,ni Tanganyika wala si Kenya au Uganda wanakoweza kupata uhondo walio nao sasa

Katika orodha hiyo hakuna hata kimoja Tanganyika inategemea ZNZ. Kuvunjika kwa muungano ni mateso kwa WZNZ.
Njia gani wanatumia?
1. Kudai mkataba ili yale mambo yatakayowasaidia kama Ardhi, udogo wa bajeti, na nishati kama umeme viendelee kupatikana bure.

2. Serikali 3, ile ya tatu ni ya mambo yanayohusu matatizo ya ZNZ.

Wasichokijua; Kurejea kwa Tanganyika ni kuondoa kila jambo na kila upande uwe sawa kwa kila kitu. Tanganyika haitakubali kuwaajiri zanzibar kama ilivyo sasa wakati Mtanganyika hatapata ajira visiwani kama ilivyo sasa.
MZNZ itabidi aje Tanganyika kama mwekezaji, masikini wasioweza kulipia hata nauli huo ndio mwisho wao.

Kuhusu Nyerere, yeye aliwahi kusema kama ZNZ watasema hawataki muungano hawezi kuwapiga mabomu. Kauli zake zililenga nyakati hizo na hakika wakati umebadilika. WZN hawataki muungano na hakuna haja ya kuwapiga mabomu. Tatizo ni kuwa wamegawanyika, washirazi wakitaka utawala wa sultani na wanyamwezi wakiyataka mapinduzi.

Nonda, ni kitu cha ajabu sana leo tukitumia mawazo ya Nyerere kuhusu muungano. Huyu Nyerere kule ZNZ ni Laanatullah sasa iweje hata uthubutu kuweka mawazo yake? Nyerere ni muasisi wa muungano lakini wapo wenye nchi wanaoamua hatima ya nchi zao, hao ni mimi na wewe kutokana na mazingira tuliyo nayo.

Mazingira tuliyo nayo yanasema kuwa muungano hauna faida kwa pande zote, moja ikionewa na nyingine ikibeba mzigo wa gharama na lawama. lIlilo jema ni kuachana tukiwa na mapenzi kwasababu haitatokea hata siku moja Tanganyika ikaihitaji ZNZ, lakini ZNZ inaihitaji Tanganyika hata leo hii na hilo ndilo chimbuko la serikali 3 au mkataba.
Serikali 3 ni jawabu baya kwa WZNZ na mkataba lazima Tanganyika ielezwe itafaidika na nini?

Nimekusaidia kujibu maswali na nadhani utatumia fikra na siyo link kufikiri.

Mkuu Nguruvi3,

Ninaposoma hii michango yako huishia kujiuliza maswali mengi.

Hitimisho lako huwa Zanzibar inang'ang'ania muungano na Tanganyika inapata hasara.

Kwa maneno mengine Zanzibar inapata faida, Tanganyika haing'ang'anii muungano.

Inaingia akili , ikiwa Zanzibar inapata faida na inang'ang'ania muungano
Lakini haingii akilini hata kidogo ikiwa Tanganyika inapata hasara na inataka kuendelea na muungano na hata kuudumisha zaidi.(kuunda serikali moja).

Tanganyika inapata hasara na yenyewe inategemea misaada na wafadhili lakini inamwadhibu kila Mzanzibari anayesema, "Tanganyika inatunyonya, inatukaba koo."

Tanganyika inahakikisha inaiba uchaguzi na kumweka madarakani Rais huko Zanzibar ambaye anatetea sera ya CCM ya serikali mbili kuelekea moja.

Tanganyika inalipa mishahara, inagawa umeme bure, inasomesha wazenj, inawapa ulinzi...yaani sielewi, Tanganyika inafanya haya yote ili iingie hasara na iinufaishe Zanzibar?

Naona kama kuna kitu hakiko sawa hapa au ndio mazingaombwe yenyewe?
 
Back
Top Bottom