Umoja wa Makanisa ya CPCT yafariji waathirika wa Maafa Hanang

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,908
945
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ameishukuru uongozi wa umoja wa Makanisa ya Kipentencoste Tanzania (CPTC) kwa namna walivyoendelea kuonesha upendo kwa kuchangia mifuko 500 ya saruji kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope na mawe kutoka Mlima Hanang’ mkoani Manyara na kuendelea kuwaombea waathirika hao.

Ameyasema hayo mapema Disemba 9, 2023 katika ibada iliyoandaliwa na umoja wa makanisa hayo iliyofanyika katika kanisa la DNPC-Katesh.

Waziri Mhagama alishukuru namna kanisa linavyoendelea kusaidia jamii katika malezi ikiwemo kuwalea kiroho na kusema hii inasaidia Serikali kuwa na vijana na Taifa lenye maadili mema.

“Kanisa ni taasisi muhimu sana, endeleeni kutushauri pale inapobidi na ninawashukuru namna mmeendelea kuungana nasi katika maafa haya kwa kutoa mifuko ya Saruji nasi tutaiwasilisha niwahakikishie itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kwa usimamizi mzuri wa Serikali yetu,” alisema Mhe Mhagama

Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentencoste Tanzania (CPTC) Dkt. Barnabas Mtokambali ameshauri jamii kuendelea kuwaombea waathirika wa maafa hayo huku akitoa rai kuona umuhimu wa kuwapa msaada kwa namna yoyote ili kusaidia na kuonesha upendo kwa matendo lengo ni kuendelea kushikamana kama Watanzania.

“Ni wakati sahihi kuwakimbilia ndugu zetu hawa, tuwaoneshe upendo na Serikali imechukua jukumu hili nasi tuungane nao kwa kuwasaidia ndugu zetu na tukumbuke bado serikali inawahudumia hata wakiwa katika makazi yetu,” alisema Mchungaji Mtokambali

Ametahadharisha uwepo wa changamoto kadhaa zinazoweza kusababishwa na mikusanyiko ikiwemo magonjwa ya milipuko, mmomonyoko wa maadili na tabia zingine zisizofaa na kuwaomba waumini na jamii kwa ujumla kuendelea kuwaombea na kuwastiri kwa namna mbalimbali.

Naye Mbunge wa Hanang’ Mhe. Mhandisi Samwel Hayuma alieleza kuwa amefarijika kwa namna kanisa lilivyowakimbilia na kuendelea kuwaombea katika mapito ya maafa yaliyotokea Wilayani Hanang’.

Aidha alimshuku Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujali na kutoa maelekezo kwa viongozi wake kuratibu na kuhakikisha hali inarejea katika nafasi yake.”

“Mhe Waziri mhagama wewe ni mpambanaji kweli, umefanya kazi kubwa katika kuratibu maafa haya, hakika Serikali inafanya kazi nzuri sana na hii imetupa faraja kubwa kuona Serikali yote ipo hapa Hanang’ tunasema asanteni sana,” alisisitiza Mhandisi Hayuma

Aidha alitumia nafasi hiyo kuwaasa Watanzania kuungana Pamoja kuendelea kumuombea mbeba maono wa nchi hii ambaye ni Mheshimiwa Rais kwa namna anavyotuongoza Pamoja na wasaidizi wake wote.

“Tuone umuhimu na haja ya kuendelea kumuombea sana Rais wetu na viongozi wote wa nchi yetu, Tanzania ni nchi nzuri yenye upendo wa hali ya juu, Tuendelee kuiombea Hanang’ yetu, Manyara yetu na Nchi kwa ujumla,” alisema.

GA-gO0mXwAALd6T.jpg
GA-gO0mXsAAXW0H.jpg
GA-gO0lWYAAre5O.jpg
GA3baalWsAAHBPf.jpg
 
Back
Top Bottom