Muunganiko wa mapacha wawili Zitto & Maalim Seif kuleta historia mpya?

Teh Teh Teh

Member
Nov 13, 2009
41
9
MUUNGANIKO WA MAPACHA WAWILI: Zitto & Maalim: HISTORIA MPYA?

Na. Dr. Goodluck Kateti.

KUNA kila dalili kwamba muda si mrefu kutoka sasa, Makamu wa Rais na Waziri Kiongozi mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Shariff Hamad, atajiunga na Chama cha ACT Wazalendo kufuatia mgogoro mkubwa uliokikumba chama alichokiasisi cha CUF.

Hadi wakati naandika andishi hili, Maalim Seif na wenzake wametumia mbinu zote za kihalali na kisheria kujaribu kukinasua chama chao kutoka katika mikono na makucha ya dola, lakini inaonekana wamenyimwa nafasi hiyo.

Kwa Maalim Seif, na wenzake katika mapambano ya kudai haki, maisha bora na maendeleo kwa Watanganyika na Wazanzibari, hakuna namna iliyobaki ya kuendeleza mapambano hayo zaidi ya kutafuta chombo kingine cha kufanikisha safari hiyo.

Dalili zote zinaonyesha kwamba chaguo la Maalim Seif litakuwa ni chama cha ACT Wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

Kama kuna jambo ambalo limeonyesha ubobezi wa kisiasa wa Maalim Seif na wenzake, basi jambo hilo ni uamuzi wa kujiunga na ACT ambacho ni miongoni mwa vyama vichanga lakini vilivyojipatia umaarufu mkubwa kwa Watanzania.

Uamuzi huu una manufaa makubwa kwa mapambano ya kudai haki na maisha bora kwa Watanzania kwa sababu unaunganisha watu wawili ambao walikuwa wanahitajika kuwa pamoja kwa muda mrefu lakini pengine wakati wake ulikuwa haujafanyika bado.

Pengine, huu ndiyo wakati ambao Mwenyezi Mungu alitaka jambo lake litokee na mgogoro wa CUF ulikuwa namna moja ya kufikia hapo. Labda nieleze kidogo kuhusu watu hawa.

Pipa na mfuniko

Wakati Maalim Seif akiwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar kwenye miaka ya 1980, Zitto alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi huko Kigoma. Zitto amemsoma na kumheshimu Maalim Seif tangu angali mdogo.

Zitto ameingia kwenye siasa za kitaifa chini ya miongo miwili tu iliyopita. Huyu ni mwanasiasa kinda ambaye anahitaji malezi ya mwanasiasa aliyebobea na anayejua nini kinahitajika na kwa wakati gani.

Wakati huohuo, ujana wa Zitto unamaanisha kwamba anayajua na ameyaishi machungu ya vijana wa Kitanzania ambao ndiyo asilimia 70 ya Watanzania wote.

Hata katika mitandao ya kijamii, Zitto ndiye mwanasiasa wa Tanzania anayefuatiliwa na Watanzania wengi zaidi kuliko mwingine yeyote ukiondoa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Muunganiko huu wa Zitto na Maalim unamaanisha kwamba unakutanisha watu ambao wanahitajiana na kila mmoja ana sifa ambazo zinasaidia kupunguza mapungufu ya mwenzake. Ni kama pipa na mfuniko wake.
Uvumilivu

Hakuna mwanasiasa wa Kitanzania ambaye amepita katika njia ya Maalim Seif. Huyu amepata kuwa Waziri Kiongozi na baadaye kuwa mfungwa wa kisiasa huku akishughulikiwa na vyombo vyote vya propaganda ya dola kama mhaini.

Ikumbukwe kwamba madhila haya yote yalimkuta Maalim wakati nchi ikiwa ni ya chama kimoja na vyombo vyote vikiwa ni vya serikali na chama tawala.

Hawa wote, asubuhi, mchana, jioni na usiku walikuwa wakimtukana, kumkashifu na kumdogosha Maalim kwa propaganda chafu za kila namna. Kama Maalim angekuwa na roho nyepesi, pengine leo tusingekuwa naye hapa duniani maana alipita katika wakati mgumu mno.

Leo hii, miongo mitatu baadaye, Maalim yu hai na anaendeleza mapambano akiwa pengine ndiye mwanasiasa anayependwa na Wazanzibari wengi kuliko mwingine yeyote. Kama kuna tuzo inapaswa kutolewa kwa sababu ya uvumilivu wa kisiasa, Maalim Seif anatakiwa kutunukiwa tuzo hiyo.

Zitto naye amepita kwenye njia hiyohiyo. Tangu mwaka 2012, Zitto Kabwe amekuwa mwathirika wa mashambulizi ya kipropaganda kutoka kwa wana CCM na vibaraka wao.

Hata hivyo, Zitto alipitia katika mtihani mgumu zaidi kisiasa wakati alipokuwa katika mgogoro na chama chake cha awali cha Chadema hadi kufikia uamuzi wa kujiuzulu ubunge na kufukuzwa kutoka katika chama alichoshiriki kukijenga kama ilivyokuwa kwa Maalim na CUF.

Kati ya mwaka 2013 na 2015, Zitto alikuwa ni target ya mashambulizi ya mtandao wa propaganda wa Chadema iliyokuwa na nguvu kubwa katika magazeti na mitandao ya kijamii na kupewa kila aina ya majina ikiwamo msaliti na mengine mengi.

Kama ilivyokuwa kwa Maalim Seif, Zitto aliweza kupita katika kipindi hicho kigumu na kufanikiwa kuanzisha na kukisimamisha chama chake ambacho leo kinafahamika kwa kuwa chama chenye ajenda, itikadi na maono makubwa kuhusu Tanzania inayotafutwa.

Kama Zitto angekuwa mwanasiasa asiye mvumilivu na mwenye ngozi ngumu, leo hii angekuwa amepotezwa kwenye siasa. Lakini Zitto Kabwe yupo na pengine ndiye mwanasiasa kipenzi cha vijana kuliko mwingine yeyote hapa nchini.

Uvumilivu huu wa Zitto na Maalim ni silaha muhimu sana katika Tanzania yetu ya sasa ambayo inapita katika majaribu mazito na inahitaji watu wenye uvumilivu wa pekee kuwapitisha watu wake.

Moyo wa kusamehe

Pamoja na machungu yote aliyoyapitia, Maalim Seif mara zote amekuwa tayari kukutana na watesi wake kwa faida ya watu wake. Ndiyo sababu alikubali kuwa sehemu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), hata kama wale alioungana nao walikuwa ndiyo wamevuruga uchaguzi.

Maalim Seif ni rafiki mzuri wa baadhi ya viongozi wa CCM waliowahi kumtesa huko nyuma. Kwa faida ya Zanzibar, amewahi kufanya mazungumzo ya Mwafaka na watu ambao walikuwa na kauli za kero na kifedhuli lakini walienda sambamba hadi kupata suluhu ya kuwatoa Wazanzibari katika wakati mgumu.

Zitto naye ana sifa kama hizo. Pamoja na vibaraka wa CCM kumshughulikia kwa nguvu zao zote, pengine yeye ndiye mbunge wa upinzani anayeweza kujisifu kuwa na urafiki wa dhati kabisa na wabunge wa CCM.

Yeye na marehemu Deo Filikunjombe walionyesha kwamba chama tawala na upinzani wanaweza kufanya kazi kwa karibu kwa maslahi ya taifa. Kama ambavyo Maalim anafanya Zbar kila inapobidi.

Ingawa aliondoka Chadema kwa mgogoro, leo hii Zitto hajaonyesha kinyongo chochote kwa chama hicho na mara zote amekuwa karibu na wabunge na viongozi wa Chadema katika matukio yote muhimu yanayohitaji ushirikiano wa pamoja.

Muungano wa Zitto na Maalim Seif unafungamanisha viongozi wawili ambao matendo yao yameonyesha kwamba wako tayari kusahau yaliyopita na kusonga mbele kwa maslahi ya taifa.

Tanzania ya sasa inapita katika kipindi kigumu na ni wazi kwamba chama kitakachoingia madarakani baada ya CCM kinatakiwa kuonyesha kwamba kitakuwa tayari kuponyesha makovu yanayojitokeza katika utawala huu na huko nyuma, kusahau yaliyopita na kusonga mbele.

Kuijua Tanzania

Maalim Seif alikuwa mmoja wa viongozi vijana waliokuwa vipenzi vya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Kama ilivyokuwa ada wakati huo, Mwalimu aliwafunza vijana wake mambo muhimu kuhusu nchi yetu.

Hii ndiyo kusema kwamba hakuna jambo muhimu la Tanzania na Watanzania ambalo Maalim halifahamu. Hakuna mkanganyiko kichwani kwake kuhusu Sera yetu ya Mambo ya Nje, maadui na marafiki zetu wala wapi hasa wazee wetu walitaka nchi yetu iende.

Tangu ACT Wazalendo ianzishwe, Zitto amekuwa akitoa matamko kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu nchi yetu ambayo serikali imekuwa haiyafanyi ipasavyo au imeanza kuyaepa kwa sababu zisizo na mashiko.

Muunganiko wa Maalim na Zitto unamaanisha kuwa na chama na watu ambao watarejesha heshima ya Tanzania na Zanzibar ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.

Uchumi

Maalim Seif ni mtu anayeamini kwamba siasa za nchi zinatakiwa kutumikia uchumi wa nchi na si vinginevyo. Anaamini kwamba Zanzibar inaweza kupiga hatua kubwa kiuchumi na kuwa kama kama visiwa vingine kama Mauritius na Shelisheli au pengine nchi kama Dubai endapo uchumi na mifumo yake itafuatwa.

Na hili lilijidhihiri wakati alipokuwa Makamu wa Rais wa SUK. Wakati anaanza kazi, bei ya zao muhimu zaidi la kiuchumi Zanzibar la karafuu ilikuwa shilingi 3,000. Wakati anamaliza muda wake, bei ilishafika hadi shilingi 20,000 kwa kilo.

Tafakari, kama wakulima wa korosho walifikia hatua ya kunywesha mbuzi soda na bia kwa bei ya korosho kupanda kutoka shilingi elfu moja mpaka elfu nne kwa kila, hawa waliotoka 3,000 mpaka 20,000 walikuwa na hali gani?

Maono haya haya ya uchumi ndiyo ambayo anayo Zitto kuhusu Tanzania. Kwa takribani miaka 10 sasa, hakuna mbunge wa Tanzania ambaye amejishughulisha kutoa hoja nzito za kiuchumi kumzidi Zitto.

Hata kabla ya kuingia madarakani, Zitto tayari anaitengenezea serikali mabilioni ya shilingi kwa sababu ya mapendekezo yake bungeni ya Kodi ya Ongezeko la Mtaji (Capital Gain Tax).

Ni Zitto huyohuyo ambaye bado anaikumbusha serikali kuhusu miradi mikubwa kama ya Mchuchuma na Liganga na akisisitiza pia kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wa taifa letu.

Muungano wa Maalim na Zitto unamaanisha kuunganishwa kwa wanasiasa wawili mashuhuri ambao kwa dhati kabisa wanaamini kuwa uchumi ndiyo kila kitu.

Hili ni la muhimu kwa sababu nchi yetu ni masikini na wanahitajika watu wenye kuamini kwanza katika uchumi kuliko siasa ili kuitoa nchi yetu hapa ilipo.

Nyota

Siasa ni nyota. Tafiti zote ambazo zimewahi kufanyika Tanzania Bara katika muktadha wa kisiasa zimekuwa zikimtaja Zitto kama mwanasiasa kijana maarufu zaidi kuliko wengine.

Hakuna shaka kwamba kwa Zanzibar, hakuna aliye maarufu na kipenzi cha wengi kama ilivyo kwa Maalim Seif.

Muunganiko wa Maalim na Zitto ni muunganiko wa kisiasa wa nyota wawili wa Zanzibar na Bara. Kwa washabiki wa mchezo wa soka, wangesema hawa wawili sasa wanakwenda kutengeneza “Real Madrid” ya vyama vya kisiasa hapa kwetu.

Ama kweli, hakuna kama Maalim Seif na Zitto katika siasa za nchi yetu.

Dr. Goodluck Kateti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halo Lipumba atakuwa anachekelea meno thelathini na nje yote mbili,

Kila uzi uliobeza harakati za Lipumba hapa JF alipata wafuasi wengi tena kwa ushabiki, bila kufuata hoja ya Lipumba ni nini na anasimamia nini,

Nilishajifanyiaga uchunguzi kwamba kwa Tanzania ni ngumu watu kufuata utaratibu wa kujua hatua mbali mbali na maana yake,

Wengi walichukizwa na tendo la Lipumba kuondoka akamnanga Lowassa kwamba hawezi kumnadi kisa mchafu,

Hiyo ilipelekea chuki si kwa Lipumba tu bali kwa yeyote aliyeonekana kuwa against Mafuriko ya mwaka 2015,

Hivo wafuasi wengi wa Chadema na Ukawa ambao ukweli huu ukiusema unaambulia kupata maadui JF na kutukanwa, wakaanza kuwakashfu wote waliojitenga na harakati zao, hata kama wangekuwa na point wasingesikilizwa ila Matusi na Kejeli,

Mi kwa kumsikiliza kwa Makini Lipumba niligundua kwamba jamaa ni kichwa sana timing yake anaifanyia ambapo Chadema, CuF na wengine wengi hawagundui ni nini kipo nyuma na sarakasi hizi,

Mbaya zaid hata waliyekuwa na mahaba naye , kayahamishia ya kwake kwa Magufuli,

CUF NGANGARIII VIJANA NGANGARIII NIMEKUMBUKA MSEMO HUU
 
Ndoa ya Mashaka,Maalim Seif amepotea njia.
Zitto ndio mshindi,lakini wakiamka waliolala fofo patachimbika.
 
Mkuu LIPUMBAV NI KICHWA KWENYE NADHARIA ZA UCHUMI ..SIO KWENYE SIO! CCM WALIONA FURSA KUPITIA POVU LAKE NA WAMEITUMIA !
 
Mbowe atakuwa muathirika wa kwanza wa muungano huu. 1 atapoteza nafasi KUB mbunge lijalalo. 2. Credibility ya uongozi wake iko mashakani kwanini Member mwandamizi wa UKawa achague chama cha Zito na sio CDM inaonesha wazi kuwa Maalim ana mashaka na uongozi na muelekeo wa CDM kwa hiyo kawatosa kiana. Obviously CUF Zanzibar itakoma hii haina ubishi na muda si mrefu Lipumba atabaki na majengo kama Mrema. CDM umaarufu utapungua sana wasipobadili muelekeo huenda nayo ikawa kama NCCR, Mbunge lijalo ACT itakuwa chama kikuu cha upizani na Zitto KUB
 
Time will tell

Sent using Jamii Forums mobile app
Act ilianzishwa chini ya nguvu ya urafiki wa zito na kikwete,kwa mpango mahususi kabisa wa kikwete kuivunja nguvu ya chadema,maana aliamini itachukua nchi.
Pia zito alilifahamu hilo,na kwakuwa alitoka chadema kwa kashfa ya uzaliti, akazigawa kura za wapinzani kwa kuanzia Act.
Hofu yangu ni kwamba,maalim sheif asije akadanganywa na zito kumbe anamkakati sirini.

Dua la kuku hili!
 
Ntakua wa mwisho kuamini kama kitendo cha Maalim seif kuhamia ACT hakina baraka za CDM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo nikuwa ACT ni tawi lingine la LUMUMBA,wasioelewa waelewe na soon Maalim atashtuka wakati asubuhi ishafika
Hilo lililkuwa wazi sana wakati ACT inaanzishwa, na hata wakati wa uchaguzi wa 2015, walibeba maslahi ya CCM waziwazi, wakiishambulia UKAWA. Na pia pale Magufuli alipotinga Bungeni kutoa hotuba yake, UKAWA walitoka bungeni hasa wakipinga uwepo wa rais wa Zanzibar ambaye alichaguliwa kwa uchaguzi feki baada ya ule halali kufutwa kwa kumtumia Jecha, Zitto alibaki bungeni kumuunga mkono Magufuli, naye alimsifiia. Lakini inaonekana Zitto hakupata alichokitafuta, na pengine hakupata hata fedha alizoahidiwa kwa kazi yake ya kuiponda UKAWA, maana tulimsikia akidaiwa madeni kibao. Hapa kati tumemuona Zitto akibadili mwelekeo.

Kimsingi Zitto hajaficha nia yake ya kugombea urais muda mrefu sana tokea akiwa CHADEMA. alitangaza nia hii siku ile ile ambayo CHADEMA walizindua kampeni zao mwaka 2010 Slaa akiwa mgombea. hiyo ilionesha kwamba Zitto hakuwa na wenzake, alilkuwa anaangalia interest zake binafsi. Hilo la Kutamani urais amelirejea tena hivi karibuni.

lakini hapa wamekutana watu wawili ambao wana sifa ya kila mmoja kuwa makini na interest zake. Maalim Seif siyo mjinga, Zitto pia siyo mbumbumbu. Je, Zitto amekuwa sasa na hekima ya kutambua kwamba ni bora kutegemeana kuliko kugombana? kwamba mpinzani mmoja hawezi kupambana na CCM? kwamba huwezi kuishinda CCM kwa kupokea peremende kutoka huko huko? haya tuache Historia itujibie
 
Mbowe atakuwa muathirika wa kwanza wa muungano huu. 1 atapoteza nafasi KUB mbunge lijalalo. 2. Credibility ya uongozi wake iko mashakani kwanini Member mwandamizi wa UKawa achague chama cha Zito na sio CDM inaonesha wazi kuwa Maalim ana mashaka na uongozi na muelekeo wa CDM kwa hiyo kawatosa kiana. Obviously CUF Zanzibar itakoma hii haina ubishi na muda si mrefu Lipumba atabaki na majengo kama Mrema. CDM umaarufu utapungua sana wasipobadili muelekeo huenda nayo ikawa kama NCCR, Mbunge lijalo ACT itakuwa chama kikuu cha upizani na Zitto KUB
Kama CHADEMA na ACT na wapinzani wengine hawajatambua tu kwamba UMOJA WAO ndiyo silaha namba moja katika kukabiliana na CCM, kwamba CCM imetumia fedha nyingi na gharama nyingine nyingi kuharibu UKAWA, kwa kuivuruga kabisa CUF na kuidhoofisha CHADEMA - japo kama wamefaulu au la hilo bado linahitaji ushahidi zaidi. kwa staili ya Magufuli naweza kuamini kwamba wapinzani bado wana nguvu sana tu.

CCM inajua kwamba wapinzani wakishirikiana, mambo ni magumu zaidi kwao. kwa hiyo ACT mpya haina njia mbadala isipokuwa kushirikiana na CHADEMA, kwa kuachiana majimbo ambapo mmoja ana nguvu zaidi. tunajua hilo siyo rahisi, lakini wanaweza kulifanya katika maeneo mengi tu. kama hawatafanya hivyo, wote wataumia na CCM itasonga mbele kidedea, na kuwaacha wakifa kifo cha mende, miguu juu.

Watanzania wapo tayari kwa mabadiliko, wanachohitaji ni taasisi ambazo zipo tayari kuwaongoza. kama watashindwa kushirikiana, wakaamini kwamba mmoja anaweza kufanya peke yake, hiyo ni bahati mbaya sana
 
Je mkigoma yupo tayari kushirikiana na wengine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Act ilianzishwa chini ya nguvu ya urafiki wa zito na kikwete,kwa mpango mahususi kabisa wa kikwete kuivunja nguvu ya chadema,maana aliamini itachukua nchi.
Pia zito alilifahamu hilo,na kwakuwa alitoka chadema kwa kashfa ya uzaliti, akazigawa kura za wapinzani kwa kuanzia Act.
Hofu yangu ni kwamba,maalim sheif asije akadanganywa na zito kumbe anamkakati sirini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kura elfu 90 ilizopata Act sioni sababu kama unaweza kuita aligawa kura.
 
Back
Top Bottom