gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,283
- 3,274
- Thread starter
- #41
Pesa inapopitiliza ni hatari sana,ni wengi sana wameweza kununuliwa ili tu wamtetee huyu mzee.Hizi kwenye histori ya nchi hiii ilishawahi kutokea kwa kiongozi kugawa pesa mamilioni kwa mamilioni kiholela akijifanya kusaidia kisa tu uraisi?Huwenda tunawezakosa kuthibitisha kwa ushahidi,lakini hata ushahidi wa mazingira tu wewe huuoni?Hivi umegawiwa sh ngapi na hata unalisaliti taifa lako?Au wewe unaitwa Fuledi mkuu?Wewe gimmy's una matatizo kichwani. Wakati ripoti ya Richmond ikisomwa bungeni Mwakyembe alituaminisha kwamba hakuisoma ripoti yote ili kunusuru amani ya nchi, huwezi hata kutafakari na kuhoji kwa nini hakuisoma yote? Sababu kubwa ni kuhusika moja kwa mija kwa JK.
Lowassa aliwaambia waliompa nafasi ya kujiangalia kwamba kuna waatu wanataka uwaziri mkuu wake kwa hiyo akaondoka wauchukue. EL ni mtu ambaye namwona kama shujaa na sugu wa kuhimili matusi na kejeli kutoka CCM. Amesisitiza mara nyingi kwamba yeyote mwenye ushahidi kwamba yeye ni fisadi aupeleke mahakamani. Na mara alipoachana na CCM aliweka bayana kilichotokea wakati wa mchakato mzima wa Richmond.
Nyie msiopenda kufikiri na kupambanua mambo hamkumbuki kwamba baada ya Richmond ilikuja Dowans ambayo kuna kitu serikali ilifanya na kujikuta inalipa faini kubwa mno. Mhusika mkubwa (yule aliyejivua gamba kwa kusema anachana na siasa uchwara) akauza mitambo hiyo kwa wamarekani kwa faida kuubwa tu. Hayo yote mnayajua???
Kinaachfanyika CCM sasa hivi ni kama kilichotokea serikalini, kutumbua vipele. Mijizi mikubwa hakuna anayeweza kuigusa akiwa ndani ya chama kibovu cha mafisadi.
Watamkaba na kumwambia kwamba hakupata urais kwa ridhaa ya wananchi (na hii si siri hata yeye anajua) na watamtahadharisha kukosa imani naye na pia watamkumbusha skandali zake nyingi za nyuma: nyumba za serikali zilivyouzwa, meli mbovu na wale samaki wa kichina. Na sasa hivi ameisha ingizwa mkenge na washauri wake kuzuia wawekezaji wenye mikataba halali wasipeleke mchanga nje. Hii ni hatari.
CCM ina wenyewe, ambao yeye si mmojawapo.