Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,174
Player ni fataki na hana taswira nyingine ingawaje huificha
Wasifu wake huvuma kwani vigezo vingi huvikamilisha bayana
Mabinti humpapatikia na tamaa yao huwa ndiyo suluba yao
Player ana makorokoro kibao na vijisenti havimpigi chenga kamwe
Player hana hasira na uvumilivu bila kikomo huwa ni rungu lake
Mustakabali wa Player ni kuvuna asichopanda!
Kwa kuelewa udhaifu wa mabinti yeye huwavuna kwa rungu lake
Shida zao wakimlilia yeye ni kimbelembele kuzitatua bila kalenda
Ingawaje hutuliza kero zao lakini moyo wake ni wa kwake pekee yake
Mabinti hupoteza maboya wakidhani Player anawahusudu kumbe la!.
Mwenyewe Player aelewa kawekeza mtaji wa nguvu na asubiria kivuno.
Mustakabali wa Player ni kuvuna asichopanda!
Player huficha msimamo wake ndani ya kichaka cha uanamalenga
Malenga malenga huwapumbaza nayo nao kumuwazawaza bila ukomo
Si usiku au mchana wao hujadili upendo wa Player bila ya kujua huo ni mtego
Player ajua fika tamaa ya mabinti ni kupendwa naye awahadaa kuwa anawapenda
Pia hachelei kuwakumbusha-kumbusha ya jinsi anavyoweweseka nao bila bureki!
Mustakabali wa Player ni kuvuna asichopanda!
Mtambue Player pale uonapo hataki mikwaruzano nawe unapombishia!
Mtambue Player pale ambapo penye udhia hukimbilia kuweka rupia!
Mtambue Player pale ambapo hudai malipo ya uwekezaji wake bila ya aibu!
Mtambue Player pale ambapo huhakikisha biashara yake huwa ni asubuhi tu!
Mtambue Player pale ambapo uonapo anavuma sana na kila binti anamsaka!
Mustakabali wa Player ni kuvuna asichopanda!