YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,906
- 51,924
Musiba ajitosa ubunge Mwibara
MCHAKAMCHAKA wa uchaguzi Mkuu ujao, umeanza kuchukua sura mpya katika Jimbo la Mwibara Wilaya ya Bunda Mkoani Mara, baada ya Mwandishi wa habari na Mtangazaji mwandamizi wa Televisheni ya Channel Ten, Cyprian Musibaambaye ametangaza kugombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, kuonekana kukubalika zaidi jimboni humo.
Musiba ambaye ni kijana, wiki iliyopita alizuru katika jimbo hilo la Mwibara kwa lengo la kujitambulisha na kutangaza nia yake ya kugombea ubunge wa jimbo hilo, alipokelewa kifalme na watu wa wengi wa rika zote kila alipokuwa akienda kujitambulisha kwake.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wanachama wa CCM katika vijiji vya vya Karukekere, Chingurubila, Mugara, Mwiruruma, Sikiro, Igundu, Muranda na Buramba, Musiba alisema ameamua kugombea ubunge katika jimbo hilo, ili kuwakomboa wananchi kimaendeleo, kwani jimbo hilo lipo nyuma zaidi kimaendeleo huenda kuliko majimbo yote nchini.
Alisema, tangu nchi ipate Uhuru hadi sasa, wananchi wa Mwibara bado wanapata shida kubwa sana katika suala zima la maendeleo, kwani barabara zilizopo hazipitiki kirahisi, huduma za afya mbovu jambo ambalo inaonekana wananchi kutelekezwa.
Jimbo la Mwibara hivi sasa linawakilishwa na mbunge anayemaliza muda wake, John Kajege (CCM), ambaye amekuwa akilalamikiwa na wananchi wengi wa jimbo hilo kwa madai ya kushindwa kutekeleza ahadi alizowaahidi, hivyo anakabiliwa na hali ngumu zaidi.
Kutokana na hilo, Musiba ambaye anaonekana kukubalika kwa wananchi wa jimbo hilo kwa asilimia kubwa, alisema iwapo atateuliwa na chama chake kugombea nafasi hiyo na hatimaye kushinda atahakikisha anaboresha barabara, afya, elimu, huduma ya maji pamoja na kujenga ofisi za CCM kila tawi na Kata.
Lengo jingine ni pamoja kujenga ushawishi mkubwa kwa wafadhili na wawekezaji kujenga viwanda vya samaki Mwibara, huduma za kibenki kusogezwa pamoja na kuimarisha ushirikiano kati yake na wananchi wa rika zote jimboni humo.
“Tangu uhuru Mwibara haina hospitali ya jimbo, barabara mbovu, huduma za afya nazo mbovu, wananchi wanakunywa maji machafu wakati Ziwa tunalo ubavuni hapa! Nikiwa mbunge wenu matatizo yote haya nitayatatua kwa haraka sana”, alisema Musiba.
Katika ziara yake hiyo ya kujitambulisha, Musiba ambaye ni mzaliwa wa Iramba Mwibara alikumbana na adha mbali mbali ikiwa ni pamoja na kukwama mara kadhaa kwa gari lake alilokuwa akilitumia kutokana na barabara kuwa mbovu zisizopitika.
Mbali na Mtangazaji huyo wa Channel Ten, Musiba kutangaza kugombea ubunge wa Mwibara, watu wengine waliotangaza kugombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM ni pamoja na mbunge wa sasa anayemaliza muda wake, Kajege na Rubola Kange ambaye amewahi kugombea chaguzi tatu zilizopita mfululizo anashindwa.
Kulingana na hali hiyo, Tanzania Daima imeshuhudia siasa chafu jimboni Mwibara, kwani baadhi ya wagombea wa jimbo hilo (majina tunayo), wameanza kutembeza rushwa ya fedha kwa wananchi, kwa lengo la kuwashawishi wawachague.
Akizungumzia suala la afya jimboni humo, Musiba alisema wanawake wengi wakiwemo wajawazito na watoto wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya katika hospitali ya binafsi ya Mission, hivyo baadhi yao hupoteza maisha yao ovyo.
Aidha, aliwasihi wanaCCM wenzake kuwapima kwa sera wagombea wote wa ubunge jimboni humo, yupi mwenye sera nzuri na anayewafaa na yupi asiyewafaa kisha kuchagua kiongozi bora na siyo bora kiongozi.
SOURCE:https://musiba4mwibara.wordpress.com/2010/04/15/musiba-ajitosa-ubunge-mwibara/
MYTAKE: CCM wana haki zote kumjadili vikao vya CCM