Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,942
- 6,860
Mishahara ya kufuru? Hiyo mnayogombea na waheshimiwa wabunge!Wewe ndugu yangu uliye nje nilieze mshahara gani na marupurupu ambao unaona utakuridhisha kurudi nyumbani? Ambao hiyo nchi yenye GDP/capita haifiki $300 kwa mwaka itaweza kukupa? Nani amesema anataka aimbiwe ngonjera? Kwangu mimi kuthaminiwa ni kupewa nafasi ya kufanya kazi kadri ya uwezo wangu bila kuingiliwa na mtu,ushauri wangu kuthaminiwa kama mtaalam, kupatiwa mazingira mazuri ya kufanyia kazi,kujua nikifanya kazi vyema nipanda hadi hapo nitakapostaili, n.k. Kwa kukazania mshahara peke yake hatutafika mbali.
Mheshmiwa Koba, huyo ndugu yako aliye planning officer huko mkoani angepewa mshahara mzuri, mazingira mzuri ya kufanya na kufanya kazi aliyoisomea sidhani kama angelalamika! Tunachofanya ni kumfrustrate mpaka nae ataona heri aende watakomthamini. Ninachosema serikali badala ya kutubembeleza sisi tulio nje iwaangalie hao walioko nyumbani kwanza.
Wako waliorudi kutokana na wito wa Rais Ali Hassan Mwinyi. Wengine walikuwa matapeli, wakagundulika na sasa hawapo tena kwenye ajira. Wengine nadhani mazingira yaliwashinda. Wengine waliorudi baadae ndio hao tunawasemea vibaya leo.
Kuna ndugu mmoja alizungumzia wananchi wanaotembea kwa mguu kutoka Kimara kwa vile hawana nauli! sasa kwa taarifa yako hawa ndio wenye bahati. Nenda huko vijijini ukaone maisha wanaoishi watanzania wenzako halafu uniambie kama hawa hawataona hiyo mishahara mnayogombeana si kufuru. Watu wanapata kichaa kwa shilingi 80,000 wakati sisi tunazungumzia ka laki 3! Ah, nimesahau, walikimbia umande!