Museveni alarmed by human capital flight

Sina la kuongezea. Umewekewa statistics na uzioni! Nchi yenye kipato cha US$ 288 bado tunadai ni tajiri? Haya mimi na wenzangu kama mimi tukichukua stahili yangu ya US$ 24,000 kwa mwaka, ambao si wa kukufuru, kutabaki nini? Nani alikuambia nataka kuishi maisha ya shida au ninaishi maisha ya shida? Ninachokataa ni hii tabia ya kusimplify mambo. Tukiuza magari, wote tutapata neema? Tunamdanganya nani? Tatizo ni kubwa zaidi. Pamoja na kubanana mbavu inatubidi wote taufanye kazi ya ziada kujikomboa. Na haitatokea kesho. Na nyinyi mnaokaa nje sio panacea. Msome Kitila Mkumbo na umuelewe.

Pato linaonekana dogo kutokana na mafisadi na wizi wanaoiba mapesa chungu nzima na rasilimali zetu zinazoporwa mchana kweupe. Statistics za kutupora, wizi na ufisadi mbona hujaziweka, je unajua kama ni kubwa!? Si umesema hutaki kulipwa mshahara wa kufuru, nikakuuliza mshahara wa kufuru ndio upi? hadi sasa umeshindwa kujibu.

Ndio nyinyi mkipata uongozi mnasema Watanzania hawastahili mishahara mikubwa maana wataishia kuoa wake chungu nzima, kuwa na nyumba ndogo na ulevi. Nani kasema tuuze magari? :confused: uwe unasoma kabla hujajibu siyo kukurupuka tu! Nimesema tunaweza kupunguza gharama kubwa za uendeshaji kama watakaostahili kuwa na magari yanayohudumiwa na serikali ni watu wachache tu wengine wote wajitegemee wenyewe, kupunguza ukubwa wa sirikali na kupunguza safari za nje ya nchi na idadi ya wasafiri katika safari hizi hii itashusha kwa kiasi kikubwa gharama hizi na savings zinaweza kuhamishiwa sehemu nyingine.

Sina haja ya kumsoma yeyote, wasomi Watanzania hawasikilizwi wako tayari kabisa kuchangia maendeleo ya nchi yao lakini maoni yao miaka nenda miaka rudi yamekuwa yanatupwa kapuni matokeo yake wamegundua kwamba kuna nchi ambazo zinathamini mchango wao na elimu yao na wakati huo huo wanalipwa vizuri.

Nyie kaeni na ngonjera yenu ya tangu mwaka wa 47 kwamba "Tanzania ni nchi maskini" wakati tunaona viongozi na familia zao wanakuwa mabilionea kila kukicha.
 
Fundi Mchundo

Sina haja ya kushinda kama unavyotaka. Hivi unafahamu kwamba geologists miaka ya 1960's walikuwa wanasoma baada ya kupata first degree? Vile vile Geotechnics kuna topics ambazo siku hizi wanasoma kwenye first degree lakini zilikuwa so advanced wakati ule na hakukuwa na programmes kwenye computer kufanya baadhi ya calculations. Kitu ambacho unashindwa kuelewa ni umbumbumbu ambao viongozi wetu wanauendekeza.

Ninarudia ukienda leo hii Bulyankulu wanaofanya kazi wataalam wa kitanzania wanalipwa pesa ndogo kulinganisha na wale wa nje kisa wao wana ngozi nyeusi rejea malalamiko yao kwenye mgomo. Tatizo sio kuwa na uwezo ni ubaguzi wa kipumbavu ambao serikali inaufumbia macho.

Kuhusu hiyo budget support ndio nasema hatuihitaji kwani nchi kama Kenya wameondokana nayo na sisi tangu pale WB au IMF whoever suggested it and tried that system ndio tumeikumbatia lakini haina faida kwa sababu hiyo misaada haiwafikii walengwa inatafunwa na wajanja wachache.

Export zinazoweza kuboreshwa ni pamoja na kuuza nyama ya ng'ombe EU, kuongeza ubora wa packing katika matunda yote yanayooza kila mwaka na kuuza EU kwa sababu wana shida ya matunda, kufufua zao la Zabibu kule Dodoma na kuuza kwa fujo. Kuongeza ulimaji wa mazao ya chakula na kuuza popote pale duniani wanakohitaji, kuongeza airport charges kwa wageni hadi kuwa $50 kwani hii ya $20 ni ya tangu miaka ya 1980. Kuweka kipaumbele kwenye kilimo matrekta ya ukakika yanunuliwe badala ya mashangingi, kukuza utalii, kuuza madini as finished products sio kuuza mchanga. Kukuza utumiaji wa gesi ambayo tunayo nyingi ya kutosha n.k. List ni ndefu sana...... vile vile lazima uzingatie kuwa na civil servant ya wafanyakazi wachache na wanaolipwa vizuri, kufanya computerization ya hali ya juu kwenye idara zote za serikali.

Huna sababu ya kunizulia mambo ambayo mimi sikuyasema.
 
Nitawajibu haraka haraka. Dada yangu hayo magari baada ya kuyapunguza tuyafanye nini? Tuyafungie MT depot? Mtu tajiri wa pili duniani anatoka Mexico, je hii ina maana kuwa Mexico ni tajiri. Kuweko na hivyo vitajiri uchwara haiondoi ukweli kuwa nchi yetu ni masikini. Wapingeni, wafungeni lakini bila kuukubali umasikini uliokubuhu na kuufanyia tutakuwa tunabadilisha mafisadi kama jirani zetu walivyofanya.
Nae Mh. Dua.
Zilikuwa advanced wakati ule na hakukuwa na computer za Kufanya baadhi ya calculations? Sasa walifundishwa vipi?

Sikatai kuwa ubaguzi upo na inawezekana kuwa hao ndugu zetu wanapunjwa kutokana na rangi zao. Lakini vilevile inawezekana kabisa kwamba criteria wanazotumia wenzetu haziko based kwenye karatasi. Tuweke sheria kama wenzetu ya kufanya ubaguzi wa rangi kuwa ni kosa ili unapotokea sheria ifuate mkondo.
Unafuatilia mazungumzo yaliyokuwa ya Doha. Kuuza nyama, matunda EU si rahisi kama unavyodhani. Unda kwenye mvinyo utapambana na wakulima wa Champagne, Porto ma kadhalika. Hayo matrekta tuwape bure hao wakulima ambao jembe la ng'ombe linawashinda. hayo mafuta, vipuri na maintenance ya kawaida atagharimia nani? haya, tunapata watalii milioni moja, tunapata $ 30 milioni. Hii itatuondoa kwenye umasikini? badala yake si itaongeza kero pale uwanjani na kuwafanya waende kwa washindani wetu?
Hiyo gesi ya kutosha iko wapi?
Civil servant ya wafanyakazi?!!! I rest my case.
Naenda kupumzika kama nilivyoshauriwa mapema.
 
Fundi Mchundo katika members wa hili Jamvi kwa kweli I salute you! umeingia katika ligi ya wachache ambao wanaangalia ukweli bila makengeza. I wish tungekuwa wengi zaidi. Hatuwezi kuendelea kwa finger pointing tuu! kwamba fulani mbaya, fulani ni fisadi nk.. we all know this, we dont need to tell each other! Swala ni kipi kifanyike? we need to offer alternative! Wewe jiulize mtu analalamika kwamba hali ni mbaya, viongozi ni wabadhirifu na uchafu mwingineo, Something I wholly agree with! lakini kipi tunafanya kubadili mambo?? usitegemee watu waiendeleze nchi yako on your behalf! wewe ni Mtanzania na Tanzania itajengwa na watanzania/wewe, na kama wewe ulivyo na hamu kuvaa vizuri, kutembelea SUVs, kuwa na pesa nyingi kwenye account, so is a normal politician in bongo, MP in Dodoma nk! Harafu leo tunalalamika ooohh, USA inadominate dunia, ni wababe, lakini look how every citizen anavyoiweka mbele inchi yake! kuna vitu kama Iraq, ME, Nk will never change whether its a democrat or a Republican! WE SHOULD GET LIFE AND LEARN!

Kama huridhiki na wewe njoo kwenye uwanja wa mapambano uingie. Haiwezekani tupige kelele tukiwa nje ya geti (JK alishasema kelele...hazimzuii mwenye nyumba kulala). Lets learn at least from ZITTO KABWE is one of the young men I admire! (though we all cant be politicians, but lets join the struggle in what we can deliver best!)

Hakuna anayelazimika kurudi nyumbani (after all BY NATURE binadamu wote ni selfish) lakini watanzania wenzangu tufike point tujiulize, sisi tunafanya nini katika kuibadilisha hii hali nyumbani kwetu? angalia US wagombea wanavyokelembeshwa kwa kuulizwa wataifanyia nini nchi yao, sisi tunashangilia na hata kama wengine hatujawa raia..tumeshachukua side nani ashinde, huyo huyo ukimuuliza kuhusu Tanzania, atakwambia imejaa ufisadi, sasa jamani, Ufisadi ni kweli upo, tufanye nini kuuondoa? haitoshi kulalamika tuu. As well said by Kitila, hiyo USA unayotembelea leo lane nane za bara bara, ilijengwa na waamerika wenye Moyo! HATA KAMA HAWAKUFAIDI, lakini waliwaachia vizazi vyao something to be proud of!

Lazima tujue kwamba maendeleo ni kujitoa mhanga. Ndugu Fundi hapo juu ametanabaisha yote sina haja ya kurudia. Tunaongea hapa kwenye forum (something which is good) lakini zaidi ya hapo ni nini? jamani umaskini wa Tanzania unatisha, usitegemee kwamba kwa sababu umesoma Harvard, Oxford nk unaweza kupata kazi wall street, utegemee mshahara huo huo ukija bongo , after all watu wa Kasulu na Kibondo wanakuhitaji zaidi ya Wall Street!

Mi kwa kweli, nasema hivi watanzania tumejaa siasa na maneno mengi, just like any humans tunapenda kuwa critical bila kuangalia the other side of the coin! Hiyo Kibongo, Kasulu, Mpanda, Likwenbe will NEVER be good if we are not prepared to go and invest our talents and abilities. Sasa leo mtu akipangiwa kazi Kibondo anaona ameonewa! nani aende sasa? akienda mwenye diploma ya chuo cha Mipango dodoma akaboronga, wote tunakuwa critical! mwenye elimu ya UCLA ambaye angeweza kufanya kazi kwa ustadi, hataki kwenda! !!! Otherwise tuamue kuendelea kulalamika tuuuuuu, wakati nchi yetu inateketea. THE BUCK STOPS WITH ALL OF US not just JK, EL, and their cabinet!

Tujiulize humu, ni wangapi maprofesa na madokta mko huko ulaya for more than ten+ years? jibu a haraka haraka ni maslahi mazuri! But deep down do you really think thats enough? harafu ujiulize wasomi wetu UD na kwingineko tunavyowaponda wakiamua kutafuta fani nyingine!

Weekend njema waungwana. Ngoja niwahi kabla ya umeme haujakatika!
 
Naenda kupumzika kama nilivyoshauriwa mapema
.

Zilikuwa advanced ......................vipi?

Umeamua kuzua wapi nimesema hivyo?

Angalia SA, Angola wanavyouza nyama pamoja na matunda EU, sisi ni member wa SADC sasa kwa nini tusitumie mbinu za wenzetu na sisi tukaweza kufanya hivyo? Tatizo letu kubwa lilikuwa la packing. Unasema tuwape matrekta bure akina nani? Kwani mashangingi tunapata bure? Unashindwa kufikiria kama tunaweza kuwa na idadi kubwa ya mashangingi hivyo kwa nini tusiwe na matrekta instead? Naona hata basic economics inaanza kukupiga chenga nimekupa mfano airport tax ya $20 ni tangu 1980's haijabadilishwa hata katika mazingira ya inflation tu ilikuwa tuongeze na mimi nikasema at least $50 kwa sasa, haba na haba hujaza kibaba.

Nimesema civil servant waajiriwe wachache ambao ni competent na kuboresha computerization kuliko kuwa na rundo la wafanyakazi ambao wanalipwa vibaya na ukienda ofisini hawapo muda wote.

Hivi kama hufahamu tuna gas nyingi tu Tanzania kutoka songo songo hata kule mtwara Mnazi bay na hatujaweza kuweka mikakati ya kuitumia yote, sasa kama hilo hufahamu sijui nikusidie vipi? Hata habari za juzi juzi tu kule mkuranga nako gas ipo. Nilisema mwanzo usikurupuke soma na elewa basis ya kinachoandikwa kabla ya kurukia keyboard.
 
Fundi Mchundo katika members wa hili Jamvi kwa kweli I salute you! umeingia katika ligi ya wachache ambao wanaangalia ukweli bila makengeza. I wish tungekuwa wengi zaidi. Hatuwezi kuendelea kwa finger pointing tuu! kwamba fulani mbaya, fulani ni fisadi nk.. we all know this, we dont need to tell each other! Swala ni kipi kifanyike? we need to offer alternative! Wewe jiulize mtu analalamika kwamba hali ni mbaya, viongozi ni wabadhirifu na uchafu mwingineo, Something I wholly agree with! lakini kipi tunafanya kubadili mambo?? usitegemee watu waiendeleze nchi yako on your behalf! wewe ni Mtanzania na Tanzania itajengwa na watanzania/wewe, na kama wewe ulivyo na hamu kuvaa vizuri, kutembelea SUVs, kuwa na pesa nyingi kwenye account, so is a normal politician in bongo, MP in Dodoma nk! Harafu leo tunalalamika ooohh, USA inadominate dunia, ni wababe, lakini look how every citizen anavyoiweka mbele inchi yake! kuna vitu kama Iraq, ME, Nk will never change whether its a democrat or a Republican! WE SHOULD GET LIFE AND LEARN!

Kama huridhiki na wewe njoo kwenye uwanja wa mapambano uingie. Haiwezekani tupige kelele tukiwa nje ya geti (JK alishasema kelele...hazimzuii mwenye nyumba kulala). Lets learn at least from ZITTO KABWE is one of the young men I admire! (though we all cant be politicians, but lets join the struggle in what we can deliver best!)

Hakuna anayelazimika kurudi nyumbani (after all BY NATURE binadamu wote ni selfish) lakini watanzania wenzangu tufike point tujiulize, sisi tunafanya nini katika kuibadilisha hii hali nyumbani kwetu? angalia US wagombea wanavyokelembeshwa kwa kuulizwa wataifanyia nini nchi yao, sisi tunashangilia na hata kama wengine hatujawa raia..tumeshachukua side nani ashinde, huyo huyo ukimuuliza kuhusu Tanzania, atakwambia imejaa ufisadi, sasa jamani, Ufisadi ni kweli upo, tufanye nini kuuondoa? haitoshi kulalamika tuu. As well said by Kitila, hiyo USA unayotembelea leo lane nane za bara bara, ilijengwa na waamerika wenye Moyo! HATA KAMA HAWAKUFAIDI, lakini waliwaachia vizazi vyao something to be proud of!

Lazima tujue kwamba maendeleo ni kujitoa mhanga. Ndugu Fundi hapo juu ametanabaisha yote sina haja ya kurudia. Tunaongea hapa kwenye forum (something which is good) lakini zaidi ya hapo ni nini? jamani umaskini wa Tanzania unatisha, usitegemee kwamba kwa sababu umesoma Harvard, Oxford nk unaweza kupata kazi wall street, utegemee mshahara huo huo ukija bongo , after all watu wa Kasulu na Kibondo wanakuhitaji zaidi ya Wall Street!

Mi kwa kweli, nasema hivi watanzania tumejaa siasa na maneno mengi, just like any humans tunapenda kuwa critical bila kuangalia the other side of the coin! Hiyo Kibongo, Kasulu, Mpanda, Likwenbe will NEVER be good if we are not prepared to go and invest our talents and abilities. Sasa leo mtu akipangiwa kazi Kibondo anaona ameonewa! nani aende sasa? akienda mwenye diploma ya chuo cha Mipango dodoma akaboronga, wote tunakuwa critical! mwenye elimu ya UCLA ambaye angeweza kufanya kazi kwa ustadi, hataki kwenda! !!! Otherwise tuamue kuendelea kulalamika tuuuuuu, wakati nchi yetu inateketea. THE BUCK STOPS WITH ALL OF US not just JK, EL, and their cabinet!

Tujiulize humu, ni wangapi maprofesa na madokta mko huko ulaya for more than ten+ years? jibu a haraka haraka ni maslahi mazuri! But deep down do you really think thats enough? harafu ujiulize wasomi wetu UD na kwingineko tunavyowaponda wakiamua kutafuta fani nyingine!

Weekend njema waungwana. Ngoja niwahi kabla ya umeme haujakatika!

Hivi hatujui kweli nini cha kufanya ili kupambana na ufisadi, wala rushwa,wanaosaini mikataba mibovu, viongozi wanaotumia nyadhifa zao kujitajirisha!? :confused:
Baada ya miaka 46 ya uhuru kama bado hatujui kupambana na uozo huo, basi bado tuna safari ndefuuuuu sana! Labda tuite expatriates (Wazungu toka nchi za magaharibi) waje kutusaidia ni vipi tupambane na uuzo huo uliokithiri Tanzania. Vichwa vyetu ni vizito mno kufikiri inabidi tusaidiwe na wazungu. Duh!
 
Nitawajibu haraka haraka. Dada yangu hayo magari baada ya kuyapunguza tuyafanye nini? Tuyafungie MT depot? Mtu tajiri wa pili duniani anatoka Mexico, je hii ina maana kuwa Mexico ni tajiri. Kuweko na hivyo vitajiri uchwara haiondoi ukweli kuwa nchi yetu ni masikini. Wapingeni, wafungeni lakini bila kuukubali umasikini uliokubuhu na kuufanyia tutakuwa tunabadilisha mafisadi kama jirani zetu walivyofanya.
Nae Mh. Dua.
Zilikuwa advanced wakati ule na hakukuwa na computer za Kufanya baadhi ya calculations? Sasa walifundishwa vipi?

Sikatai kuwa ubaguzi upo na inawezekana kuwa hao ndugu zetu wanapunjwa kutokana na rangi zao. Lakini vilevile inawezekana kabisa kwamba criteria wanazotumia wenzetu haziko based kwenye karatasi. Tuweke sheria kama wenzetu ya kufanya ubaguzi wa rangi kuwa ni kosa ili unapotokea sheria ifuate mkondo.
Unafuatilia mazungumzo yaliyokuwa ya Doha. Kuuza nyama, matunda EU si rahisi kama unavyodhani. Unda kwenye mvinyo utapambana na wakulima wa Champagne, Porto ma kadhalika. Hayo matrekta tuwape bure hao wakulima ambao jembe la ng'ombe linawashinda. hayo mafuta, vipuri na maintenance ya kawaida atagharimia nani? haya, tunapata watalii milioni moja, tunapata $ 30 milioni. Hii itatuondoa kwenye umasikini? badala yake si itaongeza kero pale uwanjani na kuwafanya waende kwa washindani wetu?
Hiyo gesi ya kutosha iko wapi?
Civil servant ya wafanyakazi?!!! I rest my case.
Naenda kupumzika kama nilivyoshauriwa mapema.

Usipindishe mambo bwana! Hakuna mtu aliyesema Watanzania wasiwe mabilionea! Mbona Mengi amekuwa Tajiri siku nyingi tu na hakuna Mtanzania anayepigia kelele utajiri wake!? Kwa sababu utajiri wake hakudhulumu mtu yeyote umepatikana kwa jasho lake na kwa njia za halali.

Tunachokataa ni kuona Viongozi wanawadhulumu Watanzania misaada, mikopo tunayopata toka nchi tajiri, kupindisha maadili ya uongozi ili kujitajirisha na kusaini mikataba mibovu ya rasilimali zetu ambayo haina manufaa kwa Tanzania wakati wao wakiwa mashareholders katika makampuni hayo ya kigeni. Kwa mara nyingine Tanzania sio MASKINI ni upumbavu tu wa viongozi wetu ambao hawana sera na wameweka mbele maslahi yao badala ya Taifa. Tulikuwa maskini kabla hatujawakaribisha 'wachukuaji' waje kuchukua dhahabu yetu, wakati makampuni yao na shareholders wao wanafaidika, Tanzania inaendelea kuwa maskini. Leo hata yakigunduliwa mafuta mengi kiasi gani Tanzania itaendelea kuwa maskini kwa sababu wanaosaini mikataba hiyo hawajali maslahi ya Tanzania bali matumbo yao. Si unaona Nigeria wana mafuta kibao, lakini mamilioni ya wananchi wa nchi hiyo wanaishi maisha ya dhiki kubwa. Hivyo ndivyo itavyokuwa kwa Tanzania. Mpaka hapo viongozi watakapoweka ubinafsi wa kujitajirisha pembeni na kuhakikisha rasilimali za Tanzania zinawanufaisha Watanzania, basi huo wimbo wenu wa 'Tanzania maskini' utaendelea kwa miaka chungu nzima. Barrick faida yao kwa mwaka 2004 ilikuwa $248,000,000 mwaka jana iliongezeka na kufikia $1,506,000,000 kutokana na ongezeko kubwa la bei ya dhahabu katika soko la dunia. Tanzania imenufaika vipi na ongezeko hilo la bei ya dhahabu katika bei ya dunia!? Haikumbulia chochote bado tunaendelea kuambulia mrahaba wa 3%! Tutaachaje kuendelea kuwa maskini!
 
Angalia SA, Angola wanavyouza nyama pamoja na matunda EU, sisi ni member wa SADC sasa kwa nini tusitumie mbinu za wenzetu na sisi tukaweza kufanya hivyo? Tatizo letu kubwa lilikuwa la packing. Unasema tuwape matrekta bure akina nani? Kwani mashangingi tunapata bure? Unashindwa kufikiria kama tunaweza kuwa na idadi kubwa ya mashangingi hivyo kwa nini tusiwe na matrekta instead? Naona hata basic economics inaanza kukupiga chenga nimekupa mfano airport tax ya $20 ni tangu 1980's haijabadilishwa hata katika mazingira ya inflation tu ilikuwa tuongeze na mimi nikasema at least $50 kwa sasa, haba na haba hujaza kibaba.

Nimesema civil servant waajiriwe wachache ambao ni competent na kuboresha computerization kuliko kuwa na rundo la wafanyakazi ambao wanalipwa vibaya na ukienda ofisini hawapo muda wote.

Hivi kama hufahamu tuna gas nyingi tu Tanzania kutoka songo songo hata kule mtwara Mnazi bay na hatujaweza kuweka mikakati ya kuitumia yote, sasa kama hilo hufahamu sijui nikusidie vipi? Hata habari za juzi juzi tu kule mkuranga nako gas ipo. Nilisema mwanzo usikurupuke soma na elewa basis ya kinachoandikwa kabla ya kurukia keyboard.[/QUOTE]

Fundi Mchundo

Sina haja ya kushinda kama unavyotaka. Hivi unafahamu kwamba geologists miaka ya 1960's walikuwa wanasoma baada ya kupata first degree? Vile vile Geotechnics kuna topics ambazo siku hizi wanasoma kwenye first degree lakini zilikuwa so advanced wakati ule na hakukuwa na programmes kwenye computer kufanya baadhi ya calculations. Kitu ambacho unashindwa kuelewa ni umbumbumbu ambao viongozi wetu wanauendekeza.

Kwa hiyo miaka ya sitini walikuwa wanachukua digrii ya kwanza halafu wanaenda Dodoma kusomea geology, hiyo miaka ya sitini? Unaamini kweli hiyo?
Hii ndiyo sentensi uliyoikana!Aha,kumbe ulisema programmes za kwenye computer! Samahani Mkuu kwa kusingizia. Lakini kama hizo calculations zilikuwa so advanced kwa nini walizifundisha? Walimu waliwapa na waliposhindwa waliwaambia wasiwe na wasiwasi, programme zinakuja? Sijaelewa umbumbu unaoendekezwa na viongozi wetu katika hili. Kutokuwa na programme za computer advanced miaka ya sitini? Au kutowatumia hao mageologists wa miaka ile wenye digrii ya kwanza? Au kutowatumia hao Civil Engineers waliochukua elective ya Geo-technics?

Ninarudia ukienda leo hii Bulyankulu wanaofanya kazi wataalam wa kitanzania wanalipwa pesa ndogo kulinganisha na wale wa nje kisa wao wana ngozi nyeusi rejea malalamiko yao kwenye mgomo. Tatizo sio kuwa na uwezo ni ubaguzi wa kipumbavu ambao serikali inaufumbia macho.

Katika soko huria, unaomba kazi na kabla ya kuingia mkatba mnakubaliana mshahara na marupurupu na haki zako nyingine. Kama mshahara anaoku"offer" mwajiri unaona ni mbuzi unakataa kusaini mkataba na unajiondokea. Ukisaini mkataba na ukakuta kuna mtu ambae kiuwezo unaona unamshinda na alipwa zaidi, unamweleza mwajiri wako. Mkishindwa kuelewana, unaacha kazi! Mathlani, umeajiriwa Microsoft halafu ukagundua kuwa Bill Gates ni kilaza hata digrii hana, na wewe una Ph.D ya nguvu,una haki ya kwenda kwa bosi na kulalamika. Wakikataa kukupandisha kumzidi Bw. Gates au kumshusha ili umzidi, unajiondokea na stock options zao unawatupia usoni.

Kuhusu hiyo budget support ndio nasema hatuihitaji kwani nchi kama Kenya wameondokana nayo na sisi tangu pale WB au IMF whoever suggested it and tried that system ndio tumeikumbatia lakini haina faida kwa sababu hiyo misaada haiwafikii walengwa inatafunwa na wajanja wachache.

Kwa vile wajanja wachache wanatafuna budget support tunasema hatuihitaji badala ya kuwachukulia hatua. Hivi kweli tumefikia mahali pa kuionea wivu Kenya? Mnyonge mwenzetu! Wale mabwana walikataa budget support kwa vile hawakutaka kuulizwa kulikoni katika ulaji wao. Hamna cha uzalendo. Tusimtupe mtoto na maji yake!

Export zinazoweza kuboreshwa ni pamoja na kuuza nyama ya ng'ombe EU, kuongeza ubora wa packing katika matunda yote yanayooza kila mwaka na kuuza EU kwa sababu wana shida ya matunda, kufufua zao la Zabibu kule Dodoma na kuuza kwa fujo. Kuongeza ulimaji wa mazao ya chakula na kuuza popote pale duniani wanakohitaji, kuongeza airport charges kwa wageni hadi kuwa $50 kwani hii ya $20 ni ya tangu miaka ya 1980. Kuweka kipaumbele kwenye kilimo matrekta ya ukakika yanunuliwe badala ya mashangingi, kukuza utalii, kuuza madini as finished products sio kuuza mchanga. Kukuza utumiaji wa gesi ambayo tunayo nyingi ya kutosha n.k. List ni ndefu sana...... vile vile lazima uzingatie kuwa na civil servant ya wafanyakazi wachache na wanaolipwa vizuri, kufanya computerization ya hali ya juu kwenye idara zote za serikali.

Nimejaribu kukueleza kuwa kuuza E.U sio kama sokoni. Kuna kitu kinaitwa Tariffs. Kuna kitu kinaitwa standards ambazo zinatumiwa vizuri kutuzia kuingia kwenye soko lao. Ndiyo maana waheshimiwa hawajaweza kuelewana kwenye mzunguko wa Doha.S.Africa na Angola wanauza nyama ya ng'ombe E.U? Mimi nilidhani Botswana ndio wauzaji wakubwa wa nyama ya ng'ombe.Lakini si unakumbuka Tanganyika packers ilivyotushinda. Na aliyekuambia E.U wana shida ya matunda nani? Machungwa etc yanatoka Spain,Egypt,Israel Ecuador wanamwaga ndizi etc. hata hizo tariff wakizitoa, tutauweza ushindani wa latin amerika, afrika kusini na nchi za mediterranean? Vile vile mvinyo. Unaamini napo kuwa tulima zabibu, halafu tukamwage Dodoma wine ulaya? Unajua soko hili lilivyo competitive? Unaujua ugomvi unaoendelea kati ya Afrika Kusini na E.U kuhusu mvinyo? Unajua wakulima wachampagne walivyo wakali kuhusu zao lao? Unajua wareno wanavyong'aka kuhusu port? Halafu kuna waAustralia, waArgentina na wenzetu wa Napa valley? Leo unaamini utawapelekea Dodoma wine bwelele?
Finished madini? Utashindana na wadachi? Unadhani mhindi yuko tayari kunua heleni zako za dhahabu? jiulize kwa nini viwanda vya korosho vilikufa?
hayo matrekta tukishayanunua badala ya mashangingi tutayafanyia nini? Kwa maneno mengine tutayafikishaje huko shambani? Tuwape bure wakulima wetu, tuwakopeshe au tuwauzie? Hawa ni wale hata pampu za Tanira ziliwashinda kuhudumia?

Gesi tunayo kweli lakini si nyingi kama unavyodhani. Pamoja na hayo, tuifanyie nini? Tuzalishe umeme ambao nasikia wenzangu wa Mtwara na Lindi hawawezi kuutumia? Tuusambaze kwenye majumba kama wenzetu wa ulaya wanavyofanya? Viwanda vingapi vinauwezo wa kutumia gesi yetu. Au tuzalishe mbolea ambayo soko la dunia limejaa? Zaidi ya hapo inapingwa na wanamazingira kwa kupunguza rutuba katika ardhi.

Haya ndugu yangu msomi, civil servant ya wafanyakazi wachache maana yake nini? Kwa upeo wangu mdogo, nadhani unamaanisha civil service ya watu wachache. Kama tena nimekuharibia mpangilio wa sentensi yako uniwie radhi. Hao civil servant surplus ambao sasa hivi wanafukuza chawa maofisini wakipunguzwa waende wapi? Kwa bahati mbaya si ofisi zote za serikali ziko Dar es salaam. Hizo za Kasulu, Manda, Mbaba Bay na zenyewe tuzicomputerise? Wakati hata umeme wa hakika hamna?

Mimi ninachokisema ni hiki tuu. Nchi yetu masikini sana ingawa ina potential. Ni sisi kwa kujituma ndio tunaweza kujitoa kwenye haya matatizo. Safari itakuwa ndefu na ngumu, tutakatishwa tamaa na wenzetu wenye uchu wa utajiri wa haraka haraka na wasio na uchungu wa nchi yao, hatuna mjomba uko nje ambae atatukomboa sisi ila tukijitahidi tutafika. Lakini si kesho. Tuwekeza kwenye elimu itakayomuempower mwananchi, tukabili matatizo yaliyo ndani ya uwezo wetu ( kupunguza vifo vya wakina mama wazazi,watoto wadogo,maji safi vijijini n.k) tuwatumie kikamilifu wataalamu wetu walio nchini na nje ya nchi, tujifunze kutokana na makosa tunayoyafanya badala ya kutafuta visingizio, tufungie kazi ubadhirifu wa aina yeyote ( ikiwa pamoja na kujipangia mishahara tusioyostahili, kutumia magari ya kifahari, kusafiri kifahari-si kila mtumishi wa umma lazima asafiri First class,tupunguze matumizi ya nishati katika maofisi yetu), tujifunze kwa waliotutangulie, turejeshe kiburi cha utaifa,tuishi kulingana na kipato chetu haswa haswa wale walio katika nafasi za uongozi,tuwekeze katika elimu,tutumie rasilimali yetu ya lugha ya Kiswahili ( tuwe kitivyo cha sinema, uandishi n.k za kiswahili), tuenzi mazingira yetituwekeze katika elimu, tuwekeze katika elimu, tuondoe usiri katika shughuli za serikali ikiwa ni pamoja na mikataba yote, tuwe wakweli na wazi katika shughuli zetu. Wengine wanaweza kuongezea.

Lakini kwako wewe Mheshimiwa Dua na Bubu, sidhani kama tutakuja kukubaliana. Naomba kiutuuzima na hasa ukilinganisha ugeni wangu na kutobahatika kwenda shule kama wenzangu,tukubali kutofautiana na tuendelee na hoja nyingine.
Huna sababu ya kunizulia mambo ambayo mimi sikuyasema.
 
Samahani , kwenye post ya hapo. Mimi ni technologically challenged kama mnavyoweza kujionea wenyewe. Kama Mh. Dua alivyonifahamisha...hata basic economics ( nisajawahi kulisoma hilo somo!) imeanza kunipiga chenga!
 
Mambo mengi tu hapa yako ni longo longo na politik kibao so dont worry kuomba msamaha maana umeshajulikana longo longo zako na maelezo mengi yanayotosha kuandika vitabu vya watoto
 
Yaani watu mna-analyse maneno ya mtu ambaye ni raisi mmoja tajiri (if not wealthiest) kutoka afrika.
 
Watu wanaojiita wasomi ndio wanaimaliza nchi,kuelimika ni tofauti na ku hudhuria madarasa kidato cha kwanza hadi shahada ya juu ya udaktari.
Mtu aliye ELIMIKA hawezi kusema sirudi kwa sababu TZ INALIPA Mishara ya laki tatu ,duu hapa inabidi ni uhoji usomi wako.

Umeenda shule kuelimika ili ukishakwisha elimika uje utumie uelevu wako ulioupata ili U CREATE mazingira hatimaye kuwatengenezea ajira watu ambao kwa namna moja au nyingine hawakupata kuelimika. Sasa napatwa na mshangao nanikibaki nimeduaa kuona mtu mwenye MASTERS akitaka kugombania ajira na watu waliomaliza FORM FOUR hii ni ajabu.

Nyie wasomi kama kweli mmeelimika mazingira ya Tz bado ni muafaka kuutumia usomi wenu kujinufaisha pia jamii kwa ujumla,
kama wasomi nao wanategemea kuja kuajiriwa na serikali sasa kuna haja gani ya watu kusoma hadi ELIMU YA JUU ambapo serikali inatumia fedha nyingi .
KAMA ENGINEER anataka kufanya kazi ya TECHNICIAN sasa kuna haja gani watu kuwa ma ENGINEER??
Kawaida ya mbabaishaji lazima apate kisingizio all in all
TANZANIA ni masikini kwa sababu wasomi wa TANZANIA wana uwalakini ktk usomi wao, wameshindwa kabisa kutumia usomi wao kugeuza malighafi waliojaliwa na Mungu kuwa na manufaa.

Kila kitu watanzania Mungu katupa ila kwa vile wote hatujaelimika tunashindwa kubadirisha SIGNAL AMBAZO ZIPO KWENYE TIME DOMAIN NA KUWA KTK FREQUENCY DOMAIN ili tupate spectrum zilizomo.
 
Mambo mengi tu hapa yako ni longo longo na politik kibao so dont worry kuomba msamaha maana umeshajulikana longo longo zako na maelezo mengi yanayotosha kuandika vitabu vya watoto

hivi kweli unaamini unapoitwa Senior Expert Member kweli ushakuwa mtaalam? Unanikumbusha mmarekani mwenzio aliyekuja akijibu"You can runbut you can not hide" kila akiulizwa jambo na wenzangu mkampa turufu akawaingiza mkenge! Jibu hoja, usipersonalise mambo! if you can't stand the heat get out of the kitchen-kwa lugha yenu. Mmezidi kutubabaisha ati kwa vile unavuta hewa moja na George Bush ndio umekuwa mtaalam!!! Get out of my face!
 
Hii thread niko 50/50.Lakini tatizo ile mtu kabukua na mishahada yake alafu akaanze kuandamana kuomba ongezeko la elfu 2 ili apate laki 1 na nusu ndio huwa tatizo.

Inafikia wakati mwingine uzalendo unakwisha ukiangalia hili sana.
 
Watu wanaojiita wasomi ndio wanaimaliza nchi,kuelimika ni tofauti na ku hudhuria madarasa kidato cha kwanza hadi shahada ya juu ya udaktari.
Mtu aliye ELIMIKA hawezi kusema sirudi kwa sababu TZ INALIPA Mishara ya laki tatu ,duu hapa inabidi ni uhoji usomi wako.

Umeenda shule kuelimika ili ukishakwisha elimika uje utumie uelevu wako ulioupata ili U CREATE mazingira hatimaye kuwatengenezea ajira watu ambao kwa namna moja au nyingine hawakupata kuelimika. Sasa napatwa na mshangao nanikibaki nimeduaa kuona mtu mwenye MASTERS akitaka kugombania ajira na watu waliomaliza FORM FOUR hii ni ajabu.

Nyie wasomi kama kweli mmeelimika mazingira ya Tz bado ni muafaka kuutumia usomi wenu kujinufaisha pia jamii kwa ujumla,
kama wasomi nao wanategemea kuja kuajiriwa na serikali sasa kuna haja gani ya watu kusoma hadi ELIMU YA JUU ambapo serikali inatumia fedha nyingi .
KAMA ENGINEER anataka kufanya kazi ya TECHNICIAN sasa kuna haja gani watu kuwa ma ENGINEER??
Kawaida ya mbabaishaji lazima apate kisingizio all in all
TANZANIA ni masikini kwa sababu wasomi wa TANZANIA wana uwalakini ktk usomi wao, wameshindwa kabisa kutumia usomi wao kugeuza malighafi waliojaliwa na Mungu kuwa na manufaa.

Kila kitu watanzania Mungu katupa ila kwa vile wote hatujaelimika tunashindwa kubadirisha SIGNAL AMBAZO ZIPO KWENYE TIME DOMAIN NA KUWA KTK FREQUENCY DOMAIN ili tupate spectrum zilizomo.

Watu wamepiga kelele dhidi ya kashfa mbali mbali za Mkapa kuhusiana na rada na kufanya biashara akiwa Ikulu, mkuu wa kazi akasema,"Mwacheni mzee wetu astaafu kwa amani." anaendelea kupeta na pesa zake za wizi, rada na rushwa. Wa kulaumiwa ni wasomi!

BOT kumetokea upotevu wa $250 millioni watu wamepiga kelele kimya, mkuu wa kazi akakaa kimya kana kwamba kila kitu kilikuwa ni shwari kabisa. Na Balali akasema, "Ugavana wa BOT sijiuzulu ng'o." Mpaka IMF na WB walipotia sauti zao ndio uchunguzi ukaanza! Wakulaumiwa ni wasomi!

Kulipotokea matatizo ya umeme, viongozi wa juu wakatangaza tenda ya kutafuta supplier wa umeme wakati ule wa kipindi kigumu kwa Watanzania. Ikaonekana Richmond ndio kampuni ambayo ingestahili kupewa mkataba ule pamoja na kuwa hawakuwa na uzoefu wowote katika mambo ya umeme! na kujifanya ni kampuni toka Marekani. Wakalipwa $172 millioni bila kufanya chochote kile! na nchi bado ikawa gizani. Watu wakapiga kelele na wabunge wakahoji kuhusiana na mkataba huo, lakini Waziri mkuu akaongea na wabunge wa CCM na kuwataka wasihoji mkataba ule kwa kuwa sasa umeme umesharudi na wabunge wakasikiliza wito wa Mkuu na kunyamaza KIMYA! Wa kulaumiwa si wengine bali ni WASOMI!

Mdosi aliyejipatia $12,000,000 za pesa za walipa kodi katika deal ya rada, ambayo Mkapa pamoja na kelele mbali mbali ndani na nje ya nchi aling'ang'ania kuinunua rada hiyo na Mramba kudai,"hata majani tutakula lakini rada ni lazima inunuliwe." alikuwa yupo nchini. Kilichohitajika kufanywa ni kumtia ndani mpaka hapo uchunguzi utakapomalizika ili kumfungulia mashtaka kama kuna ushahidi wa kutosha dhidi yake, wakamwacha huru mpaka kaingia mitini! wa kulaumiwa si wengine bali WASOMI!

Mikataba ikapigiwa kelele haina manufaa kwa nchi, na mkuu wa kazi akaahidi wakati wa kampeni yake kuiangalia upya ili kuhakikisha Tanzania inanufaika, pia akaahidi wakati wa kampeni 2005 kwamba hautasainiwa mkataba mwingine wowote wa madini mpaka hapo kazi ya kuiangalia mikataba ya zamani itakapomalizika na marekebisho kufanywa. Bado wakatumia siri kubwa kwenda kusaini Buzwagi nje ya nchi, na kipengele muhimu kukibadilisha bila ya kuomba maoni ya waliokiweka kipengele hicho! wa kulaumiwa ni nani WASOMI!

Waache waende zao kwenye nchi ambako wanaonekana ni watu wa maana, maoni yao kusikilizwa na kutolaumiwa kwa mabaya yanayofanywa na wengine katika kuiangamiza nchi, kupewa vitendea kazi na mishahara na marupurupu mazuri. Ama kweli WASOMI ndio wanaoipeleka pabaya Tanzania! Mimi nilidhani ni wanasiasa, mafisadi, wala rushwa, viongozi wenye uroho wa kujilimbikizia mali kumbe nilikuwa nakosea sana!
 
Watu hawataki kuangalia negative impact ya kuwalipa wafanyakazi mishahara midogo ambayo haiendani na hali halisi ya maisha. Wanachoangalia ni kwamba mtu akilipwa $1,500 kwa mwezi ni pesa nyingi sana hizo, huyu atafaidi sana si mwenzetu tena huyu!

Ukweli ni kwamba, Mtanzania huyu akilipwa pesa nzuri kama hiyo, anachapa kazi mtindo mmoja hana wasiwasi na pesa anajua ana pesa ya kutosha kabisa kuishi vizuri na wakati huo huo kuinvest katika uchumi wa Tanzania ambapo itasaidia kucreate kazi nyingine, kwa maneno mengine productivity yake itakuwa kubwa. Matokeo yake mshahara wa $1,500 kwa mtanzania mmoja unaweza kabisa kucreate kazi nyingine mbili au tatu. Watu wanapokuwa na purchasing power kubwa demand ya vitu na huduma mbali mbali inaongezeka hivyo kuusaidia uchumi kwa namna moja au nyingine na kama purchasing power yao ni ndogo demand inadumaa au hata kupungua matokeo yake uchumi nao unadumaa au hata kupungua na hii inakuwa ni vicious cycle inaendelea mwaka hadi mwaka. Lakini bado kuna wenzetu wanaona kumlipa mtanzania msomi mshahara wa $1,500 ni pesa ya kufuru hawaangalii upande mwingine wa sarafu kwamba Tanzania itanufaika vipi kwa kuwa na wananchi wengi wenye purchasing power kubwa!
:(
 
Watu wamepiga kelele dhidi ya kashfa mbali mbali za Mkapa kuhusiana na rada na kufanya biashara akiwa Ikulu, mkuu wa kazi akasema,"Mwacheni mzee wetu astaafu kwa amani." anaendelea kupeta na pesa zake za wizi, rada na rushwa. Wa kulaumiwa ni wasomi!

BOT kumetokea upotevu wa $250 millioni watu wamepiga kelele kimya, mkuu wa kazi akakaa kimya kana kwamba kila kitu kilikuwa ni shwari kabisa. Na Balali akasema, "Ugavana wa BOT sijiuzulu ng'o." Mpaka IMF na WB walipotia sauti zao ndio uchunguzi ukaanza! Wakulaumiwa ni wasomi!

Kulipotokea matatizo ya umeme, viongozi wa juu wakatangaza tenda ya kutafuta supplier wa umeme wakati ule wa kipindi kigumu kwa Watanzania. Ikaonekana Richmond ndio kampuni ambayo ingestahili kupewa mkataba ule pamoja na kuwa hawakuwa na uzoefu wowote katika mambo ya umeme! na kujifanya ni kampuni toka Marekani. Wakalipwa $172 millioni bila kufanya chochote kile! na nchi bado ikawa gizani. Watu wakapiga kelele na wabunge wakahoji kuhusiana na mkataba huo, lakini Waziri mkuu akaongea na wabunge wa CCM na kuwataka wasihoji mkataba ule kwa kuwa sasa umeme umesharudi na wabunge wakasikiliza wito wa Mkuu na kunyamaza KIMYA! Wa kulaumiwa si wengine bali ni WASOMI!

Mdosi aliyejipatia $12,000,000 za pesa za walipa kodi katika deal ya rada, ambayo Mkapa pamoja na kelele mbali mbali ndani na nje ya nchi aling'ang'ania kuinunua rada hiyo na Mramba kudai,"hata majani tutakula lakini rada ni lazima inunuliwe." alikuwa yupo nchini. Kilichohitajika kufanywa ni kumtia ndani mpaka hapo uchunguzi utakapomalizika ili kumfungulia mashtaka kama kuna ushahidi wa kutosha dhidi yake, wakamwacha huru mpaka kaingia mitini! wa kulaumiwa si wengine bali WASOMI!

Mikataba ikapigiwa kelele haina manufaa kwa nchi, na mkuu wa kazi akaahidi wakati wa kampeni yake kuiangalia upya ili kuhakikisha Tanzania inanufaika, pia akaahidi wakati wa kampeni 2005 kwamba hautasainiwa mkataba mwingine wowote wa madini mpaka hapo kazi ya kuiangalia mikataba ya zamani itakapomalizika na marekebisho kufanywa. Bado wakatumia siri kubwa kwenda kusaini Buzwagi nje ya nchi, na kipengele muhimu kukibadilisha bila ya kuomba maoni ya waliokiweka kipengele hicho! wa kulaumiwa ni nani WASOMI!

Waache waende zao kwenye nchi ambako wanaonekana ni watu wa maana, maoni yao kusikilizwa na kutolaumiwa kwa mabaya yanayofanywa na wengine katika kuiangamiza nchi, kupewa vitendea kazi na mishahara na marupurupu mazuri. Ama kweli WASOMI ndio wanaoipeleka pabaya Tanzania! Mimi nilidhani ni wanasiasa, mafisadi, wala rushwa, viongozi wenye uroho wa kujilimbikizia mali kumbe nilikuwa nakosea sana!

Bubu unauaaaaaa.....ndo maana nasema huyo raisi anayeongelewa, yaani ni kama anasanifu watu. Kwani yeye hakujua yote haya mpaka leo na kajitajirisha mpaka mmoja wa maraisi tajiri afrika. Its a joke.
Mkuu mimi wakati nasoma university....kijana wake huyu alikuwa anakuja kusumbua huko chuo. Yaani unakaa unajiuliza what the hell is wrong with Africa. The guy is taking the p.iss.

Kama mwafrika wa kike alivyosema.....too much longolongo. Hata speech yake ni longolongo tu, angekuwa na nia ya kufanya mabadiliko angekuwa ameshaanza miaka yote aliyokuwa kwenye cheo chake. A lot of times, african leaders just talk so as to say the obvious thing that sound right, but their own way of running things or way of life, contradicts what they say.
 
Watu wamepiga kelele dhidi ya kashfa mbali mbali za Mkapa kuhusiana na rada na kufanya biashara akiwa Ikulu, mkuu wa kazi akasema,"Mwacheni mzee wetu astaafu kwa amani." anaendelea kupeta na pesa zake za wizi, rada na rushwa. Wa kulaumiwa ni wasomi!

BOT kumetokea upotevu wa $250 millioni watu wamepiga kelele kimya, mkuu wa kazi akakaa kimya kana kwamba kila kitu kilikuwa ni shwari kabisa. Na Balali akasema, "Ugavana wa BOT sijiuzulu ng'o." Mpaka IMF na WB walipotia sauti zao ndio uchunguzi ukaanza! Wakulaumiwa ni wasomi!

Kulipotokea matatizo ya umeme, viongozi wa juu wakatangaza tenda ya kutafuta supplier wa umeme wakati ule wa kipindi kigumu kwa Watanzania. Ikaonekana Richmond ndio kampuni ambayo ingestahili kupewa mkataba ule pamoja na kuwa hawakuwa na uzoefu wowote katika mambo ya umeme! na kujifanya ni kampuni toka Marekani. Wakalipwa $172 millioni bila kufanya chochote kile! na nchi bado ikawa gizani. Watu wakapiga kelele na wabunge wakahoji kuhusiana na mkataba huo, lakini Waziri mkuu akaongea na wabunge wa CCM na kuwataka wasihoji mkataba ule kwa kuwa sasa umeme umesharudi na wabunge wakasikiliza wito wa Mkuu na kunyamaza KIMYA! Wa kulaumiwa si wengine bali ni WASOMI!

Mdosi aliyejipatia $12,000,000 za pesa za walipa kodi katika deal ya rada, ambayo Mkapa pamoja na kelele mbali mbali ndani na nje ya nchi aling'ang'ania kuinunua rada hiyo na Mramba kudai,"hata majani tutakula lakini rada ni lazima inunuliwe." alikuwa yupo nchini. Kilichohitajika kufanywa ni kumtia ndani mpaka hapo uchunguzi utakapomalizika ili kumfungulia mashtaka kama kuna ushahidi wa kutosha dhidi yake, wakamwacha huru mpaka kaingia mitini! wa kulaumiwa si wengine bali WASOMI!

Mikataba ikapigiwa kelele haina manufaa kwa nchi, na mkuu wa kazi akaahidi wakati wa kampeni yake kuiangalia upya ili kuhakikisha Tanzania inanufaika, pia akaahidi wakati wa kampeni 2005 kwamba hautasainiwa mkataba mwingine wowote wa madini mpaka hapo kazi ya kuiangalia mikataba ya zamani itakapomalizika na marekebisho kufanywa. Bado wakatumia siri kubwa kwenda kusaini Buzwagi nje ya nchi, na kipengele muhimu kukibadilisha bila ya kuomba maoni ya waliokiweka kipengele hicho! wa kulaumiwa ni nani WASOMI!

Waache waende zao kwenye nchi ambako wanaonekana ni watu wa maana, maoni yao kusikilizwa na kutolaumiwa kwa mabaya yanayofanywa na wengine katika kuiangamiza nchi, kupewa vitendea kazi na mishahara na marupurupu mazuri. Ama kweli WASOMI ndio wanaoipeleka pabaya Tanzania! Mimi nilidhani ni wanasiasa, mafisadi, wala rushwa, viongozi wenye uroho wa kujilimbikizia mali kumbe nilikuwa nakosea sana!

NARUDIA tena WASOMI ndio chanzo cha KUFUBAHA kwa uchumi wa TANZANIA
kwa ku prove hilo DR ndio aliyesaini mkataba wa BUZWAG
PROFESA ndiye aliye Saini mkataba wa TCCL.
VIOngozi karibu 80% wamesoma ulaya na marekani tena OXFORD na HAVARD hii ni sample ambayo tukiichukua ina toa tathimini nzima.

Achana na hiyo wasomi walio nje ya zizi wenyewe wakiita SYSTEM kazi yao ni kupiga mayowe wakiambiwa njooni na njia mbadala vichwa chini.
MAFISADI hata leo wakiondoka yani TZ ikawa haina hata mfisadi mmoja kwa hali hii ya kupiga mayowe UCHUMI WETU utaendelea kudidimia tena kwa mwendo wa ajabu.

KUMBUKA kipindi cha Nyerere mafisadi walikuwa wachache mno na kiongozi yule kwa swala la kujirimbikizia mali kila mmoja anajua mbona umasikini haukuondoka????.
UMASIKINI wa TZ sio wa ufisadi ,kwa mtazamo mwepesi utasema hivo
bali umasikini wetu ni UDHAIFU WA FIKRA NA MTAZAMO KWA WATANZANIA WOTE. Hii inatokana na kuelimika kwetu kuwa TETE.

Utasikia mtanzania anasema mimi sirudi kwa sababu ya PESA na akisahau kabisa MATUNDA ya wana ulaya na wamarekani yanatokana na mitazamo mirefu ya AKINA dr LIVINGSTONE aliyefia bagamoyo akitembea kwa mguu kwa ajiri ya kizazi chake cha leo.VASCO DAGAMA kapanda mashua na akajitoa kwa ajiri ya watu wa leo ambako yeye hakufaidika.
MIMI SIWASIFII ila angalia ktk wazungu unaokutana kwenye daladala utakuta anajisomea yani kati ya watatu lazima mmoja atakuwa na anajisomea SWALI je waTZ WANGAPI UMEKUTANA NAO WAKIJISOMEA.

I ngia ktk nyumba ya mzungu utakuta kabati la vitabu TENA SEBULENI ila UKIINGIA KWA mswahili utakutana na makabati ya vyombo na mi jokofu.
kUITWA dr AU prof HAKUNA MAANA JAMAA YULE KAELIMIKA ,ANGAlia mavituz ya mtoto wa darasa la SABA SHABAN ROBERT Utalinganisha na msomi yupi??.
Wasomi kama wangekuwepo TZ huo ufisadi usingekuwepo, na nina imani ULISOMA kitabu cha kusadikika KALAMA MSOMI pekee aliye fanya mapinduzi ya kimufumo pia kiuchumi ktk nchi ya KUSADIKIKA nchi iliyokuwa inaendeshwa kibabe na kifedhuli ije iwe TZ, kifupi
TZ HAKUNA WASOMI.
msomi ni mtetea haki kwa gharama ya aina yoyote ile ,hawo wanaojiita wasomi ni MAFISADI WA ELIMU wakitafuta sifa ktk jamii.
Kubali ukweli ili ujue tatizo ulilonalo na usake mwarobaini wake.
 
Back
Top Bottom