- Thread starter
- #121
Pole sana mleta mada!!! Kuanzia leo acha kumlea mume huyo!!!!!!!!!!!!!!!!!! Ulianza kumlea pale uliporuhusu kugawana majukumu 50%!!!! Sijajua wewe ni imani gani ila kwa wakristu imeandikwa kuwa mke ni msaidizi wako na kuwa unatakiwa kumtunza. Bi mkubwa wa Lara 1 alikuwa sahihi kabisa na wanawake wote mnatakiwa mjifunze hili. Wale wanaume ambao wanataka kulelewa huwa wanataka wake au wapenzi wao wawe ni financier, Ninaamini kuwa nikiwa kama mwanaume heshima yangu inapanda pale ninapokuwa na uwezo na jukumu la kuilisha familia yangu na mke anachangia tu. Tena niwaambie kuwa kama mke wako anaona unajituma kuangalia familia vizuri huwa inampa motivation sana ya yeye kuchangia ili kuonesha upendo wake. Cha msingi kama mke anafanya kazi kuna majukumu madogomadogo kama mishahara ya watumishi, vitu vidogovidogo vya watoto n.k. Ninakumbuka wakati tunasomesha, kulikuwa hakuna hizi shule zenu za hela nyingi, shule za serikali tulikuwa tunalipa 750,au 1,500 hivi mara ya mwisho ila uniform na pocket money na mambo mengine ilikuwa juu ya mzazi. Mwenzangu kuna wakati kabisa ananiambia kuwa analipa ada na si kwa kuwa nilimlazimisha ila kwa kuwa alikuwa ana appreciate matunzo yangu kwa familia. I tell you ninapotumika kwa familia yangu, najiona chief au king Fulani hivi na heshima inakuwepo full kuanzia kwa watoto hadi mama. Sasa wewe mwanaume goigoi unamwachia mke wako aheme mwishowe anachoka na sura haivutii kabisa mwisho wa siku unaanza kutafuta wa sura za kung'aa wakati ya mkeo uliharibu kwa kumpa kazi za mitulinga. Wanawake ni maua, na maua haya need handling with care!!! Extra care!!!! I wish you all the best, those who are still searching for their better half to get the rib of their ribs!!!! Usipoweza kufanya hivyo ndiyo yatajeuka ya huyu mzee Kalbandika wa huyu mleta mada. Pole sana dada yangu ila kuanzia sasa weka mikakati ya kumuwajibisha huyu mumeo. Akishasimama imara ndipo uanze kumsaidia kile kinachowezekana.
asante kwa ushauri mzuri, yaani nahisi nishazeeka hata kabla ya siku zangu...unajua hata hiyo 50% yenyewe tulikubaliana baada ya kuona ananiachia kila kitu, yaani hajishughulishi, nikaona bora tugawane ili ijulikane nani yuko responsible na nini ndio ikaja hiyo 50%, kwangu mimi ilikuwa ni ahueni...lkn na yenyewe hatimizi, sasa nikimuachia less say 90% ataweza?
niliposoma maoni yako umenifurahisha sana, yaani ww ni baba na uko proud na familia yako kwa unavyoihudumia..sisi wengine tulipata bahati mbaya tukakutana na vimeo, ndio tunahangaika huku jf saa izi...mi mwenyewe nakumbuka vile baba yangu alivyokuwa anatuhudumia kwa kila kitu mpaka mimi nimeolewa nakumbuka baba yangu alikuwa ananinipa hela ile miaka ya mwanzoni mwa ndoa(mpk nilikuwa naona aibu) na hajaacha mpk nilipopata kazi ndio akaacha kunipa hela..huyu baba yangu kwa sasa ni marehemu Mungu amlaze mahala pema kwa kweli niko proud sana na baba yangu.