mume analala nje wiki nzima bila mawasiliano na mkewe

Mar 2, 2013
24
6
Habari za wakati huu,

Wapendwa kaka na dada zangu, ni mara ya kwanza ktk uwanja huu. wote salaamu!

nina rafiki yangu ameolewa na wamebahatikkuwa na mtoto mmoja. mume wake ni dereva daladala. wanaishi dsm mtongani, mume anaendesha daladala za gongolamboto. lakini siku zote hulala nje eti hawezirudi nyumbani kwa hofu ya kuchelewa kuamka asbh. so ktk wiki atarudi nyumbani cku moja. tena bila ya pesa, na atalala cku moja tu.

Hana huduma zote muhimu kwa mke na mtoto. mwanamke anajisaidia mwenyewe kwa kila kitu. tena imebidi achukuwe mtoto ampeleke kwa wazazi wake mwanamke ili aweze kutafuta riziki. mume hana msaada wowote kwake. sasa mwanamke amechukuwa maamuzi ya kutafuta chumba na kuishi mwenyewe, akaenda kueleza matatizo yake upande wa mume wake na uamuzi aliochukua.

Kikafanyika kikao na mume akiwepo mume akadai atajirekebisha akamuomba mkeme asiondoke. mke akamsamehe, lakini mume karudia tena tba yake ya mwanzo. sasa mke anaomba ushauri juu ya hili. natanguliza shukrani
 
kama anakuja once is enough lol,wewe huoni wanawake( sio wote) wana low sex drive....mie asipokuja ndio sahihi ananipunguzia mzigo atii................nakutania mwambie achunguze nini kinachomuweka huko nje,kama mnalala pamoja na anagopa kuchelewa kuamka, solution ni kununua simu ya alarm itakayomuasha au wewe mwenyewe chukua jukumu la kumuamsha
 
Issue nyingine ni nyepesi sana hazihitaji hata kuumiza ubongo. Hapo hakuna ndoa na jamaa anakuja kubadilisha tu mazingira. That's all.
 
kama issue ni kuchelewa kazini kwanini asipange nyumba ya kuishi na mkewe hukohuko,afu anarudi nyumbani mara moja kama mgao wa umeme mmmmmh hapo hakuna ndoa anauchosha tu mwili wake kumhudumia hata hiyo mara moja mara mia achukue talaka bado mapema. Wanaopenda kuolewa huku hawana mbele wala nyuma mnamsubilia husband aprovide nadhani funzo mmelipata hapa.
 
Pole, kuna asilimia kubwa sana ana nyumba ndogo mahali na ametekwa kweli kweli.

Ni aibu sana mtu aache familia mke na damu yake iteseke nam hiyo kwa kuendekeza tamaa, too bad
Baadhi yetu tunafanya yasiyotakikana kabisa.
 
Huyo mwanaume mbona hana msaada...aachane naye atafute maisha yake
 
Awe na msimamo kama aliamua kuondoka sasa ni wakati wa kufanya hivyo la kama anajisikilizia maumivu No Cmnt
 
pole mdada kwa yaliyokukuta, hii ni mitihani ambayo inatakiwa kuishinda.
 
uamuzi aliochukua mara
ya kwanza wa kupanga chumba ni mzuri
huyo mume ana hawara,na kwake anaenda
labda ili abadili viwalo bas,na kama hamtunzi kwa chochote
na anaishi basi ni dhahiri anaweza kujimudu na mtt wake!!mpe pole lol!!
hua anaomba msamaha wa kinafki huyo hana lolote!!
 
Kwanza nampongeza mwanamke kwa moyo wake wa uvumilivu aliouonyesha kwa kipindi chote alichokuwa na mumewe, ila ifike mahali mtu aseme "enough is enough" haiwezekan mtu akufanyie vitendo kama hivi, tena vitendo vya kujirudiarudia halafu uendeleza msamaha kila mara. Ifike mahali na mwanamme aone kwamba amekosea na ahitaji kujirekebisha kwa yale matendo mabaya anayo yafanya. Nasema mwanamama huyo anatakiwa a "go on" kwa kutafuta maisha yake mwenyewe na wala asiangalie nyuma tena kwani kukaa na huyo mwanaume anajiongezea matatizo tu.
 
Wanaume kama tumelogwa vile, anyway, ajishughulishe mwenyewe kuliko kujitafutia presha ya bule mwenzake anakula good time.
 
Kama huko aliko wamepanga anasshidwa nini kuhamia huko anakoamini anaweza kuamuka mapema na kuwahi kibaruani ili kuepuka kuvunja ndoa yake. Kama hilo haliwezekani basi hapo hakuna ndoa baina ya hao wawili, aidha pia anaposema anakuja mara moja moja tena bila pesa sasa anafanya nini, huoni hii ni second justification kwamba hiyo ndoa ilikwisha vunjika siku nyingi sana, na huyu ndugu yako anachukuliwa kama nyumba ndogo tu na si vinginevyo.

Mpe pole sana kwa kupoza ndoa yake, na mwambie achukue hatua zinazostahili ama kuirudisha ndoa yake hiyo na akishindwa akubali kuivunja rasmi.
 
Issue nyingine ni nyepesi sana hazihitaji hata kuumiza ubongo. Hapo hakuna ndoa na jamaa anakuja kubadilisha tu mazingira. That's all.

Uko sawa mkuu; kwa nyongeza huyo mwanamke inabidi atafute mume mwingine aachane na huyo dreva wa dalaldala.
Pia kuna uwezekano mkubwa labda huyo mwanamke naye anaweza akawa na vitabia ambavyo mumewe vinamkera. Wapo wanawake ambao ikitokea mwanaume akayumba kiuchumi wanabadilika sana na kuanza vimaneno vya kejeli; mara mwanaume gani, mara kutotoa unyumba na mengine mengi.
 
Mwenye macho haambiw tazama mwambie achape raba mjini hapa ...............kwan frm begin walianzaje na ss wanaendeleaje till kufikia kwny situation hyo
 
Habari za wakati huu,

Wapendwa kaka na dada zangu, ni mara ya kwanza ktk uwanja huu. wote salaamu!

nina rafiki yangu ameolewa na wamebahatikkuwa na mtoto mmoja. mume wake ni dereva daladala. wanaishi dsm mtongani, mume anaendesha daladala za gongolamboto. lakini siku zote hulala nje eti hawezirudi nyumbani kwa hofu ya kuchelewa kuamka asbh. so ktk wiki atarudi nyumbani cku moja. tena bila ya pesa, na atalala cku moja tu.

Hana huduma zote muhimu kwa mke na mtoto. mwanamke anajisaidia mwenyewe kwa kila kitu. tena imebidi achukuwe mtoto ampeleke kwa wazazi wake mwanamke ili aweze kutafuta riziki. mume hana msaada wowote kwake. sasa mwanamke amechukuwa maamuzi ya kutafuta chumba na kuishi mwenyewe, akaenda kueleza matatizo yake upande wa mume wake na uamuzi aliochukua.

Kikafanyika kikao na mume akiwepo mume akadai atajirekebisha akamuomba mkeme asiondoke. mke akamsamehe, lakini mume karudia tena tba yake ya mwanzo. sasa mke anaomba ushauri juu ya hili. natanguliza shukrani

Hii ni sinema nyingine ya vituko mitaani..
 
Yaani alipomsamehe alitegemea kaka wa watu ataacha kuogopa kushindwa kuamka? Sasa inamaanisha jamaa analala kwenye gari ama? Nna maswali kama 159 hivi!
Cc Boflo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom