JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,316
- 5,479
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imetangaza kuwa upasuaji wa kutenganisha watoto waliokuwa wameungana umefanyika kwa mafanikio.
Watoto hao Rehema na Neema walikuwa wameungana kifuani na upasuaji huo umefanyika leo Julai Mosi, 2022 chini ya Wataalam wa Afya 31.
Awali, Mtaalam wa Magonjwa ya Watoto-Muhimbili, Dkt. Petronila Ngiloi alisema watoto hao walikuwa na muunganiko mkubwa wa Ini na kuna uwazi mkubwa katika Kitovu wanachotumia pamoja.
Pia soma > Watoto pacha walioungana kufanyiwa upasuaji Muhimbili, leo Julai 1, 2022