Teamo
JF-Expert Member
- Jan 9, 2009
- 12,272
- 1,035
HONGERA SANA DK.wapendwa wanaJF na watanzania wenzangu wote,
nichukue fursa hii kutoa pole zangu za dhati kwa watanzania wote kwa msiba mkubwa uliolikumba taifa kutokana na mbinu dhaifu, zilizopotoka na mbaya za ulinzi zilizotumiwa na jeshi letu la polisi kwa maelelkezo ya viongozi wao na kusababisha maafa ya raia wema mkoani Arusha tarehe 5 January 2011 wakati wakitekeleza kwa vitendo haki yao ya msingi ya kukutana na kuandamana kwa mujibu wa katiba.
binafsi sikuwepo nchini wakati hayo yakiokea na nilifuatilia tukio zima kupitia mitandao ya internet. niseme tu kuwa najua hivi sasa marehemu wamekwishaagwa na kuzikwa huku wakipewa heshima wanayostahili na chama cha demokrasiaa maendeleo CHADEMA na wakazi wa Arusha na vitongoji vyake na hata miji jirani. ila nimesikitishwa sana na kutojitokeza kwa kiongozi yoyote wa serikali na wa chama cha mapinduzi kushiriki waziwazi kwenye msiba huo. kuna wakati inabidi hata mchawi mwenyewe kuhudhuria msiba kwani ni katika matukio kama hayo dhamira ya kweli ya umoja na undugu hudhirika.
pia nimeshangazwa sana na kitendo cha waziri mkuu kushindwa kutoa tamko lolote la serikali hadi wakati huu, si kwa uchaguzi wa meya wala wa machafuko yaliyosababisha umwagaji wa damu zisizo na hatia. halikadhalika sijasikia kauli thabiti ya wahusika kukemea na kukosoa jeshi la polisi kwa mashambulizi dhidi ya raia kwenye maandamano ya amani kwa kutumia risasi za moto. yote haya kwangu yanadhihirisha udhaifu wa uongozi na ulegevu katika kuchukua hatua madhubuti pale zinapohitajika.
nakumbuka wakati IGP mstaafu Omary Mahita aliposhutumu wabunge kujipendelea kwa mishahara na posho kubwa huku askari wake wakiwa an maissha na zana duni, haraka haraka aliomba radhi baada ya kubanwa na kamati ya bunge iliyokuwa chini ya mh Simpasa. binafsi nilichukizwa kuona askari akiomba radhi mwanasiasa, lakini kwa hili la arusha naamini itakuwa heshima viongozi wa jeshi hasa IGP mwenyewe akiwaomba radhi wanachi wote wa Tanzania kwa jeshi lake kushindwa kulinda usalama na badala yake kushambulia hata pale palipokuwa hakuna tishio lolote la kiusalama. hata kama ni kwa kupotoshwa na taarifa za kiintelijensia, bado anapaswa si tu kuwachukulia hatua waliompotosha, bali pia kuwajibika kwa kutoa maagizo yaliyopelekea maafa kwa raia wema na uharibifu wa mali.
kumhusu waziri nahodha, mie binafsi sijapata kufurahishwa na uongozi wake tangu alipokuwa waziri kiongozi huko zanzibar. ni kwamba sijajua vigezo vilivyotumika kumweka hapo alipo, lakini kwa hili la arusha na lile la zanziba wakati wote akiwa madarakani na kuhusika moja kwa moja na matukuio yote mawili, naye anapaswa si tu kuwajibika , bali kjichunguza kama kweli anaweza kuwa kongozi wa dhamana ya kiwango alichonacho na bado akawa ni wa kutumainiwa. tathmini hiyo yafaa pia kufanywa na rais kikwete na iwe ni dira ya kumuongoza katika kuteua wasidizi wake kwa siku zijazo.
mwisho niupongeze uongozi wa CHADEMA kwa kutoyumba katika kutetea kile wanachoamini na kuwapa heshima waliyostahili ndugu zetu wote waliotutoka. ni changamoto kama hizi ndio zimebadili sehemu nyingine za dunia na kuwa na demokrasia za kupigiwa mfano. aidha chama cha mapinduzi nacha chapaswa kujitafakari namna kinavyoendesha siasa zake hasa miongoni mwa watu wa tabaka za chini. nafikiri ni wakati muafaka sasa wa CCM kujihoji pia kama bado inamhitaji luteni makamba kuendelea kuwa katibu mkuu wake. matatizo kama haya yalihitaji umakini wa kiuongozo ili kuayepuka na hata watu wadogo kinafasi na kiwadhifa kama mary chatanda leo wasingekuwa wanjulikana kiasi hiki. kule kushindwa kutokea kwenye msiba, kunadhihirisha kuwa CCM na serikali yake wamewaachia CHADEMA msiba wao. hili ni kosa na hata kama hawataelewa leo, wataelewa kesho.
nimalizie tena kwa kutoa pole kwa wafiwa na majeruhi wote na kumuuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. amina
walau umetofautiana na mnaemwita ''katibu''