MUAJI YA KINYAMA ARUSHA: Mwema, Nahodha na Kikwete Mjipime Kubakia Madarakani

ni vigumu sana kuwatenganisha viongozi wa dini na maouvu ya viongozi wa serikali. Atamfundisha vipi aliyeporwa kiwanja kwa mfano? Aliyelala njaa kwa ukosefu wa chakula wakati kuna watu wanafanya ubadhirifu, kama kuna voingozi wa dola wanaua raia mbele ya nyumba za ibada, ?

Kwa kifupi kwa mtu makini lazima afurahie kwamba viongozi wa dini wanayohaki ya kukemea, kuelekeza na kuonya ikiwa ni pamoja kuchukua.

Tutaendelea kudai polisi waliofyatua risasi kumwaga damu ya ndugu zetu wafikishwe kwenye mkondo wa sheria for murder case ili pia nao wawataje waliowatuma.

Hivyo mkwere, nahodha, igp -katili, na andnyenge wafukuzwe kwa nguvu ya umma-maanake wasipoachia tutaamini wazi mkulu ndiye alitaka kulipiza kisasi.


Nakubaliana na wewe kabisa katika hili!

Kwa kuwa SIASA inahusu jamii ya Tanzania; ustawi wetu mzuri na maendeleo yetu, na kwa upande mwingine MASUALA YA KIROHO vile vile yanahusu jamii hii ya Tanzania kwa ustawi wetu mzuri na maendeleo, yeyote anayejaribu kusema SIASA na DINI ni kama mbingu na ardhi kamwe si mkweli.

Hizi dira zote mbili za miongozo katika maendeleo na ustawi wa maisha ya binadamu ni nguvu mbili kubwa ambazo kwa kiasi kikubwa zaidi (i) hutegemeana, (ii) hukamilishana na vile vile (iii) hupingana katika (a) kasi gani mambo yaende, (b) kiwango gani cha ushirikishwaji, (c) uwajibikaji murua ulioje.

Hivyo, katika kutazama jinsi nguvu za SIASA na DINI zinavyofanya kazi katika maisha ya binadamu katika nyanja zote za kitamaduni, kisiasa na kiuchumi zote hushikwa na nguzo moja iitwayo HAKI.

Pindi uonapo kwamba Viongozi wa SIASA na wenzao wa DINI hawaelewani au kila kimoja ndani kwanda mwake basi ujue ama NGUZO MAMA (HAKI) imepindishwa mahala au haipo kabisa.

Lakini pale ambapo haki huonekana kujaa tele kwa furaha ya kila mshikadau basi MATUNDA MEMA ambayo jamii zima pamoja na wanasiasa na viongozi wa dini huvuna (1) AMANI, (2) UPENDO, (3) UMOJA na (4) UZALENDO wa Hiari katika taifa.

Hadi hapo ninamaanisha yeyote anayejaribu kudai kuwepo matunda haya manne bila ya kuchunguza Jamii yake na msimamo wa ile NGUZO MAMA - Haki ambayo ndio kiunganishi cha yote.

Tanzania serikali yetu hutambua jambo hili???
 
Back
Top Bottom