Muafaka CCM na CUF, pande mbili za shilingi!

Nilikwisha kusema CUF hawatorudi katika mazungumzo hayo hata kwa bakora ,wameshatega na mtego umenasa na jinsi nchi ilivyochafuka ndio kabsaa hawakai mezani wala kwenye jamvi ,Ubabe wa CCM unaelkea ukingoni hizi alama zote zinazotutokelea zina maana na si dalili nzuri kwa chama tawala na kiongozi wao ,kama hawajui ndivyo au mwanzo wa kitu kinachoporomoka na kuanguka ,tusitegemee CCM itaanguka kama nazi lakini itaporomoka kaa mlima kwa luga ya kigeni wanaita landslide au mudslide ndio hivyo hivyo.
Nikirudi kwa Makamba yeye alitakiwa kujiuzulu palepale Butiama bila ya kuchelewa ili alinde heshima yake lakini sasa amekuwa kama mbao ya mkonge au bua ,tatizo ni kwa hawa wanaojiita CCM ni kuwa wengi wao hawajiamini na ubaya uliokuwemo ndani ya Chama chao ni tishio na wanahisi huenda wakadhurika au kupata shinikozo la damu ugonjwa maarufu kwa viongozi wa CCM.
 
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba ameomba kukutana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad wazungumze kuhusu hatima ya mwafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar.


Habari zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi waandamizi wa makao makuu ya CCM, jijini Dar es Salaam, zinaeleza kuwa Makamba ameomba suala hilo kupitia barua yake ya Aprili 25, mwaka huu, aliyomwandikia Maalim Seif.


Vilevile, Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Ismail Jussa, wamelithibitishia gazeti hili jana kuhusu chama chao kupokea barua hiyo na kusema kuwa, wamekwishaijibu tangu jana.


Hatua hiyo ya Makamba imefikiwa ikiwa ni siku mbili, baada ya kukaririwa na gazeti hili Jumanne wiki hii, akipinga kufanya mawasiliano yoyote mapya na CUF kuhusu mwafaka huo.


Katika barua hiyo, Makamba amemuomba Maalim Seif wakutane wazungumze ili wapate kuzikutanisha kamati za mazungumzo ya mwafaka za vyama vyao ili waendelee na mazungumzo hayo.


Kwa mujibu wa Jussa, barua hiyo ya Makamba iliandikwa Aprili 25, mwaka huu, lakini ikapokelewa na Katibu Mkuu wa CUF juzi.


Hata hivyo, Hamad na Jussa kwa nyakati tofauti jana, waliliambia gazeti hili kuwa, barua hiyo ilijibiwa jana kwa CUF kulikataa ombi hilo la Makamba.


''Ni kweli tumeipokea barua hiyo. Ni ya tarehe 25, lakini ilipokelewa jana (juzi). Haina chochote cha maana. Tumeijibu leo (jana),'' walisema.


Hamad alisema wamelikataa ombi hilo la Makamba kwa vile mazungumzo kuhusu mwafaka wa kisiasa Zanzibar, yalishaisha muda mrefu na walishafikia makubaliano mbalimbali kati yao na CCM, ikiwamo kuundwa kwa serikali shirikishi, maarufu kama ''Serikali ya Mseto,'' visiwani humo.


Alisema sababu nyingine ya kukataa ombi hilo la Makamba, inatokana na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kushindwa kutekeleza agizo lake alilolitoa mbele ya umma katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Aprili 4, mwaka huu, kwamba atamwagiza Makamba awaandikie CUF makubaliano waliyofikia katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC-CCM), uliofanyika Butiama, mkoani Mara, Machi 29-30, mwaka huu.


Hamad alisema pamoja na CUF kuiandikia barua CCM zaidi ya mara mbili kuomba makubaliano hayo, hadi sasa CCM hawajafanya hivyo.


Alisema sababu nyingine ya kukataa ombi la Makamba, inatokana na kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa katika ukumbi huo iliyoonyesha kutoheshimu na kuthamini mamlaka na maamuzi ya Makamba kama Katibu Mkuu wa chama.


Alisema katika mkutano huo wa Diamond Jubilee, Rais Kikwete alikaririwa akisema saini ya Makamba na Maalim Seif hazitoshi kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na kamati za mazungumzo ya mwafaka za vyama hivyo.


''Hivyo, sisi hatuwezi kukaa na mtu ambaye hana 'mandate' (mamlaka) kwa chama chake na asiyekuwa na uwezo wa kukwamua matatizo. Sisi Katibu Mkuu wetu ana 'mandate' katika chama na maamuzi yake tunayaheshimu na kuyathamini,'' alisema Hamad.


Jussa na Hamad walisema njia pekee iliyobaki hivi sasa, ni Rais Kikwete kuwakutanisha Maalim Seif na Rais Aman Abeid Karume, kama alivyofanya Kenya kwa kuwakutanisha Kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM), Raila Odinga na Rais Mwai Kibaki wa PNU, ili kuupatia ufumbuzi mgogoro uliopo visiwani humo.


Jumatatu wiki hii, Makamba aliliambia gazeti hili kuwa wanasubiri majibu kutoka CUF kuhusu suala hilo na kwamba, haoni sababu ya kujibu barua aliyoandikiwa na Maalim Seif kukataa kuendeleza mazungumzo yaliyoitishwa upya na CCM.


"Tulitoka Butiama, tukawaandikia barua kuwaomba turejee katika mazungumzo. Wao wakatuandikia kuwa hawataki. Sasa unataka niwajibu nini? Mimi ndiye nangoja majibu kutoka kwao," alisema Makamba kwa njia ya simu juzi.


Kauli hiyo ya Makamba, ilitolewa siku hiyo saa chache baada ya Hamad, kuliambia gazeti hili kuwa CCM hawajajibu barua yao.


Katika barua hiyo yenye Kumbumbuku namba CUF/AKM/CCM.II/2008/007 ya Aprili 14, 2008 iliyosambazwa kupitia mtandao wa intaneti, Maalim Seif alisema CUF haiko tayari kushirikiana na CCM kuwahadaa Watanzania kwa kuendeleza mazungumzo yasiyo na mwisho na yaliyokosa nia njema.


Nakala ya barua hiyo ya Maalim Seif, ilipelekwa pia kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Rais Amani Abeid Karume na Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba.


Wengine, ni Mwenyekiti Mwenza wa Mazungumzo ya Mwafaka kutoka CUF, Hamad Rashid Mohamed na Mwenyekiti Mwenza wa Mazungumzo hayo kutoka CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru.


Maalim Seif alisema pendekezo la kufanya kura ya maoni akiita kuwa ni kiini macho chenye lengo la kuchelewesha utiaji saini na utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa, halikubaliki kwa CUF.

Source: Gazeti Mwananchi


Zee la Shamba,
Habari hii source yake ni Raia Mwema la Jumatano iliyopita na sio Mwananchi ama unavyotaka tuamini. Unaweza kufanya mabadiriko ya source ya hiyo habari?
 
aslaam aleikum wanajamii.
kwanza ninafuraha kubwa kujiunga na jamboforum.
nakubaliana na rasnungwi kuhusu muuafaka wa Zanzibar mimi si mwanasiasa au mwanachama wa chama chochote.Isipokua mimi ni mpenda amani na rakha za kuishi kwa usalama katika dunia hii.Kwamtizamo wangu naona sisi Wazanzibar umefika wakati wakuungana sio kutengana.Muafaka ni kitu murua kwetu hasa tukizingatia kua sisi sote ni wamoja tusijaribu kutumia siasa za kututenganisha ila tutumie siasa za kutuweka pamoja .hii ndio njia pekee ya kufuata.tusiwe na siasa mbovu zilizopitwa na wakati.Muuafaka utatuletea mambo mazuri na kutupa fikira za kutatua matatizo yetu tutakua na uwezo wa kuongoza nchi yetu bila purukushani zozote.
Wazanzibari wenzangu lazime tujue kua Zanzibar ni kama jahazi ndogo kama inaanza kuvuja tushirikiane kuikalafati tuendelee na safari yetu.tukigawana mbao hatufiki tutazama tuu
 
Assalaam wanajamii hebu tuliangalie suala la Zanzibar pasi na ushabiki,chuki na mapenzi yetu binafsi.uwapi uhalali wa mapinduzi ikiwa kwa maneno ya John Okello wazanzibari walioshiriki walikuwa nane(8).Hivyo ile ilikuwa ni GENOCIDE na ukweli wake aliujua Mwalimu na Bwana Karume.Serikali kuendelea na sherehe za mapinduzi kila mwaka ni sawa na kurejesha kumbukumbu za mauaji ya 1964 na kwa sababu hiyo CUF wasahau kama kutakuwa na serikali ya mseto kwa sasa.Hisia na chuki za mauaji ya 1964 zitachukua muda mrefu kusahaulika kwa kuwa ziliwagusa wazanzibari wengi mno kwa kuwa washiriki wake wengi hawakuwa wazanzibari.
 
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema suala la Mwafaka wa kisiasa kati yake na Chama Cha Mapinduzi (CCM), limekwisha na walikuwa wakijipanga, na sasa wako tayari kuwapa Watanzania fursa ya kuchagua Dira ya Mabadiliko na kuitumia kuongoza harakati za kuing'oa madarakani CCM kupitia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baadaye mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani.

Aidha, chama hicho kimeeleza kushangazwa na hatua ya CCM ‘kuchumpa' katika suala la kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini, suala ambalo liliwekwa katika Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho tawala ya mwaka 2005, na katika siku za karibuni, kuzua mjadala nchini.

"Mwafaka ulikwisha. Tulikuwa tumeshafikia makubaliano na wenzetu na kilichobaki ni ceremony (sherehe) za kusaini Mwafaka, lakini wenzetu wakachumpa. Hatuzungumzii tena suala hili. Tutaicheza ngoma kwa kadri itakavyokuwa inadundwa," ilikuwa kauli ya Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipozungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini jana Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ‘Operesheni Zinduka'.

Profesa Lipumba akiwa na viongozi wengine wakuu wa CUF, alisema suala la Mwafaka halina nafasi tena, bali chama hicho kitakabiliana na mambo kwa kadri yatakavyokuwa yakitokeza, lakini muhimu kwa sasa ni kuwapelekea wananchi Dira ya Mabadiliko ambayo inatilia mkazo mambo 13.

Aliyataja mambo hayo kuwa ni kila raia popote alipo kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi; kujenga umoja wa kitaifa wa kweli; kuhakikisha kuwa kila mwananchi ana uwezo na anawezeshwa kupata milo mitatu kwa siku; kuhakikisha kuwa kila raia ana haki na anapata huduma za msingi za afya; kujenga maadili ya kuwaheshimu na kuwaenzi wazee na watoto wote wa Tanzania wawe na haki ya kupata elimu bora ya msingi na ya sekondari.

Mambo mengine ni motisha maalumu utolewe kwa wasichana na familia zao ili wamalize elimu ya msingi na waendelee na sekondari; kuwaelimisha wasichana na wanawake washiriki katika soko la ajira; Taifa litoe kipaumbele maalumu katika kuendeleza elimu ya sayansi na teknolojia.

"Kujenga uchumi wa kisasa wenye ushindani wa kimataifa na utakaohimili misukosuko ya utandawazi; wananchi wahisi na waone kuwa uchumi wa Taifa unatoa fursa kwa wananchi wote; kukuza uchumi na kuongeza ajira na kuwapo kwa uongozi imara na utawala bora katika kukuza uchumi," alisema Profesa Lipumba na kuongeza kuwa CUF imeandaa dira huyo ya kuleta mabadiliko kupitia mijadala.

Alisema kwa kuanzia, CUF itazindua ‘Operesheni Zinduka' Julai 11, mwaka huu katika Jiji la Mwanza, na itafanya kampeni hiyo kwa awamu ya kwanza katika mikoa 11 ya Bara itakayohusisha mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Tabora na Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Morogoro.

Alisema CUF itaongoza kampeni hiyo ya mabadiliko kwa sababu ndicho chama kikuu cha upinzani Tanzania, kiko imara na kina viongozi makini. "Vyama vingine vya siasa vimejionyesha kuwa ni vyama vilivyopo kwa maslahi ya viongozi wake wachache wanaovifanya kama ni miliki yao na ambao hawawezi kuhojiwa na hivyo kupelekea vyenyewe kuzama katika ufisadi na kushindwa kujiendesha.

Vingine ni dhaifu na visivyo na mtandao wa kitaifa wa kuweza kuleta mabadiliko ya maana yatakayoleta tija," alisema Lipumba na kuongeza: "Kwa chama makini cha siasa kinachopigania mabadiliko, kufichua maovu na ufisadi au kwa lugha ya mtaani ‘kulipua mabomu' pekee hakutoshi kuleta ukombozi wa kweli wa Mtanzania. Kauli za hamasa na jazba ni muhimu kuwapa wananchi ari ya kujiletea mabadiliko katika maisha yao."

Alisema mabadiliko wanayotaka Watanzania hayawezi kuja kwa njia za kushitukiza na kuongeza kuwa "Watanzania wanastahili kuwa na Dira ya Taifa ya kujenga nchini inayoheshimu haki za binadamu, yenye misingi mizuri ya demokrasia ambapo raia wote watu wazima wenye akili timamu wana haki ya kushiriki kikamilifu katika uamuzi wa masuala yanayohusu maisha yao na hatma ya nchi yao."

Akijibu maswali mbalimbali ya wahariri, Profesa Lipumba alisema CUF itaendelea kudai Katiba na Tume huru ya uchaguzi, huku akimtupia lawama Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame akidai ni ‘goigoi' ambaye atastaafu wadhifa huo akiwa hana la kukumbukwa.

Aligusia suala la Mahakama ya Kadhi, akisema, "Hili limewekwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM, na wenzetu, tena wasomi baada ya kuisoma wakasifu sana, lakini sasa wanachumpa. Hili litaleta vurumai."

Aidha, Profesa Lipumba pia alimsifu Mbunge wa Ilemela, Anthony Diallo (CCM) kwa hoja yake bungeni kuhusu mgawanyo wa fedha za barabara, ingawa alisema kumekuwa na vituko vingi bungeni kutoka kwa wabunge wa chama tawala katika michango yao hivi sasa.

Kuhusu Operesheni Zinduka na pigo la hivi karibuni la CUF kuondokewa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake Tanzania Bara, Wilfred Lwakatare aliyehamia Chadema, Profesa Lipumba alisema muhimu ni kujenga chama kama taasisi na siyo kutegemea sifa ya mtu binafsi.

"CUF inaamini katika kujenga chama kama taasisi, chama ni demokrasia, personality ni muhimu katika siasa, lakini chama kijengwe kama taasisi, ili anapoondoka mtu hakiathiriki. Hili la kuondoka kwa watu tunaowajenga, linasikitisha, linanifedhehesha, lakini huwezi kulikwepa," alisema mchumi huyo.
Source: HabariLeo, Julai 06, 2009.
 
Good move...better late than never! wamechelewa kufanya jambao hili..lakini ni bora kuchelewa kuliko kutofanya kabisa...nafikiri wapeleka timu ambayo inaweza kuongeza wanachama katika mikoa hiyo pamoja na wapenzi wa chama katika mikoa hiyo..
All the best CUF GO GO CUF... ulikuwa mwamba utabaki mwamba ukiamua ...
 
Nawatakia kila la kheir, ila naona kama wanatafuta pa kutokea baada ya kupoteza mwelekeo ktk mambo mengi muhimu ya kisiasa na kijamii.
 
Kila siku mazungumzo ya muafaka yanavunjwa then it's back to square one. Politics as usual. It's become like a real life soap opera.
 
Mwafaka ulikuwa ni mwanzo wa kuwapotezea mwelekeo CUF na ilikuwa ni mbinu ya CCM kuwapooza, sasa wameshituka. Lakini baada ya kukubali mwafaka, wakaanza kupoteza mwelekeo kwa kuwa chama kinachoshindwa kusoma alama za nyakati na hiyo imewaponza sana CUF, chama kilichokuwa na nguvu kubwa Tanzania.

Nguvu ya CUF iliegemea kwenye mvutano na serikali na hasa ya Mkapa iliyotumia mabavu kupambana nao (Ngangari vs Ngunguri) lakini sasa wanapambana na wasanii, wanaowabembeleza na kuwalipia hoteli na gharama nyingine, kiulainiii!!!! Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu.
 
Ndiyo mjue hatuna wanasiasa wa kweli. Hata hao baadhi ya upinzani wanaojidai kuhubiri madhambi ya serikali majukwaani ni wanafiki pia. They have a price and sadly their price is so small. Matokeo yake ndiyo hivyo vyama vingine vinakuja juu na nguvu zao zinabaki za upande mmoja.
 
Warudi kwenye, "jino kwa jino, mapanga shaaa", huku na wenzao Chadema wakijifunza, na wao muda si mrefu watakuja na mwafaka wa "Biharamulo" wenzao wanachukua, wanaweka, waaa!!!! Hata kwa wizi, waaa, hata kwa mtutu, waaa!!! Hata kwa majeshi, waaa!!!

Nimeandika kama utani, lakini demokrasia ya nchi hii ina safari ndefu sana.
INAUMA SANA MJOMBA
 
Wadugu wa CUF mupooo??? Juma Duni Haji wapi? Wapi Machano? Wapi Saidi Miraji? Wapi Salim Bimani? Wapi wana mkakati?
 
Nawatakia kila la kheir, ila naona kama wanatafuta pa kutokea baada ya kupoteza mwelekeo ktk mambo mengi muhimu ya kisiasa na kijamii.
Mkuu Halisi,

Labda una jua mengi ambayo wengine hatujui ila statement hiyo hapo juu mbona kama ni over the top?

CUF bado ndio chama kikuu cha upinzani Zanzibar kama ambavyo CHADEMA kilivyo Tanzania bara. Hivyo ndivyo ilivyokuwa mwaka jana, ndivyo ilivyo sasa.
 
Mkuu Halisi,

Labda una jua mengi ambayo wengine hatujui ila statement hiyo hapo juu mbona kama ni over the top?

CUF bado ndio chama kikuu cha upinzani Zanzibar kama ambavyo CHADEMA kilivyo Tanzania bara. Hivyo ndivyo ilivyokuwa mwaka jana, ndivyo ilivyo sasa.
Lakini inabidi kibadilike. Chambilecho -CUF itayoyoma na CCM itapaa. Lakini mimi nina imani kabisa na Chama mbadala (alternative Party) Hakijaundwa kutokana na nguvu za CCM na CUF. Lakni nikuleleze -asilimia kubwa ya walio CCM hawafurahi na halkadhalika asilimia kubwa ya walio CUF hawafurahi. sasa maji tu yanafuata mkondo.
 
Mkuu Halisi,

Labda una jua mengi ambayo wengine hatujui ila statement hiyo hapo juu mbona kama ni over the top?

CUF bado ndio chama kikuu cha upinzani Zanzibar kama ambavyo CHADEMA kilivyo Tanzania bara. Hivyo ndivyo ilivyokuwa mwaka jana, ndivyo ilivyo sasa.
Kuna watu hawataki kuamini kuwa chama cha CUF kinaelekea ikulu kutokea upinzani. Silazima iwe kesho au keshokutwa, kwakuwa inaeleweka kuwa demokarasia ina mikondo mingi ya kupita mpaka kufikia ufukweni salama. Nikimkumbuka Abdulaye Wade alivyo suffer na PDS yake tokea mwaka 1974, wakati bado Leopard Sedar Senghor mwenyewa yu hai, Wade kawa mpinzani tokea siku zote hizo, na alishindwa katika chaguzi 4 katika kitu cha urais, mpaka kizazi kipya cha Wasenegal kinafumbua macho na kumuelewa(baada ya kufa au kupoteza dira kwa wahafidhina) mwaka 2000 ndo PDS ya Wade na Wade mwenyewe wanaingia ikulu.
Kwa hiyo kufikia mafanikio kuna taka mipango ya muda mfupi na muda mreefu kama PDS ya Wade na usatahamilivu wa kuwavumilia wananchi katika kipindi cha mpito kuelekea demokarasia ya kweli,ambacho wengine hawajaifahamu hada madhumuni yake na vyama vinavyotawala vinatumia hila na vitimbi kuchezea ridhaa na matakwa ya wananchi walioifahamu hiyo demokarasia ya uchaguzi na wananchi kubakia kimya wakiwaachia viongozi wao wa vyama vya siasa wapege kelele.
Ila kwa kumalizia, chama cha Mapinduzi kisitazamie kutawala nchi hii comfortably miaka yote, kama UNIP ya Kaunda kama KANU ya Moi n.k kuna siku kitapumzishwa na siku zenyewe zinaanza kusogea taratiiibu. time will tell.
 
CUF bado is the big disappointment. Wana mtaji mkubwa zaidi wa kisiasa lakini wanautumia vibaya sana.
Sijakuelewa mkuu disappointment kivip? fafanua.
Siasa ni process. nafikiri they have learnt the lesson kwamba CCM ni wasaniii waanze upya...
 
Sijakuelewa mkuu disappointment kivip? fafanua.
Siasa ni process. nafikiri they have learnt the lesson kwamba CCM ni wasaniii waanze upya...
CCm sio wasanii, bali ndio magwiji wa siasa za hapo Bongo! Vyama vingine vyote kwa namna moja ama nyingine vimekuwa vinakopi mambo mengi ya CCM na hivyo kuonekana kuwa hawana jipya!
 
Back
Top Bottom