Mtu Muhimu Sana Maishani Mwako

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,813
59,393
Kila mtu aliye karibu na wewe ana umuhimu, kila mmoja kwa kiasi chake.

Swali linakuja je, MTU GANI NI MUHIMU KULIKO WOTE MAISHANI MWAKO??

Uko tayari kumlinda kwa lolote?:fencing:
Uko tayari kufa kwaajili yake?:rip:

Na kama angekua tofauti na alivyo (tabia,sura,elimu,n.k)/au akibadilika bado atakua na umuhimu alio nao maishani mwako?:A S thumbs_up:
 
Mke wangu ndio mtu wa muhimu kuliko wote maishani mwangu. niko tayari kumlinda na kumtetea kwa lolote hata kama amewakosea watu wengine etc. ila, siko tayari kufa kwaajili yake kwasababu Yesu peke yake ndo aliyekuwa na uwezo wa kufa kwaajili ya wengine. Mungu anatusaidia, hawezi kuwa tofauti wala hawezi kubadilika kwa lolote.

namtetea na kumpenda. mfano: yeye kama mwanamke wenye mapungufu kama walivyo wanawake wengine,hata kama atakuwa amewakosea kwa bahati mbaya majirani,rafikize au mtu yeyote, sitakubali mtu yeyote anyooshe mkono kumpiga, kumtukana, kumdhalilisha kwa lolote. anayeona waifu wangu ana matatizo anatakiwa aje aniambie mimi imrekebishe, kama hataki kuniambia mimi basi anyamaze kimyaaa aniachie waifu wangu. niko tayari kumlinda asiumie moyo ili sote tuishi maisha marefu,

nimemtetea na hakuna hata ndugu yeyote mwenye mamlaka ya kuingilia ndoa yetu, ndugu yeyote akitaka anichokoze basi aingilie ndoa yetu, amsema mke wangu vibaya au afanye lolote...awe dada yangu(wifi yake waifu), maza wangu au yeyote, mimi nilishajiunga kuwa mwili mmoja na wafu wangu, so anayemgusa yeye ananigusa mimi. However, wanaweza kutoa ushauri tu kwa busara na heshima nyingiiiii. out of that, watuache tu, byebye.
 
mama yangu huwa hana mpinzani, na ataendelea hivyo siku zote za uhai wangu

mama yako naye anasema "baba yako" hana mpinzani na ataendelea kuwa hivyo maishani mwake. wewe kama umeolewa na huna kitu kama hiyo moyoni kwaajili ya bwanako, basi ndoa hiyo ina mashaka. mamako mwenyewe anampenda zaidi babayako kuliko hata wewe, au unaonaje angempenda zaidi bibi yako kuliko wewe? kama ni mamayako, basi, wawili hao wakiwa hatarini utamwokoa mama kwanza kabla ya baba?
 
upande wangu ni wengi muhimu katika maisha yangu. lakini wa karibu sana ni mama yangu, mume wangu, watoto. nipo tayari kuwatetea na kuwalinda wote hao kwa kadiri ya uwezo wangu. lakini kwa kusema ukweli, sipo tayari KUFA kwa ajili ya yeyote.
 
Kila mtu aliye karibu na wewe ana umuhimu, kila mmoja kwa kiasi chake.

Swali linakuja je, MTU GANI NI MUHIMU KULIKO WOTE MAISHANI MWAKO??

Uko tayari kumlinda kwa lolote?:fencing:
Uko tayari kufa kwaajili yake?:rip:

Na kama angekua tofauti na alivyo (tabia,sura,elimu,n.k)/au akibadilika bado atakua na umuhimu alio nao maishani mwako?:A S thumbs_up:

Swali lako limejifungafunga mno! ungeishia hapa..".MTU GANI NI MUHIMU KULIKO WOTE MAISHANI MWAKO??"..ningesema
ni Yesu Kristo..Lakini pia ulipoongeza hayo ya chini umenitoa hamu kabisa! kwani baba na mama wote wana 100% respectively.....
Wewe je, unaonaje nani muhimu kwako??
 
[/B]

Yesu ni zaidi ya mtu, yeye ni Mungu. ndo maana hata hatujagusa kusema Yesu ni mtu wa muhimu. angesema nani wa muhimu kuliko vitu vyote, hapa kila mtu angeshasema "Mungu". lakini yeye kasema "mtu tani wa muhimu, na Yesu si mwanadamu, ni Mungu.
 
Mungu hazaliwi!!! Hebu acha kamba zako!!!!
 
Yesu ni zaidi ya mtu, yeye ni Mungu. ndo maana hata hatujagusa kusema Yesu ni mtu wa muhimu. angesema nani wa muhimu kuliko vitu vyote, hapa kila mtu angeshasema "Mungu". lakini yeye kasema "mtu tani wa muhimu, na Yesu si mwanadamu, ni Mungu.

Jamani yesu alikuwa mwanadamu pia!!!!!!!!!! mbona mnakuwa wazito hivyo kuelewa? ndio maana alikula samaki, alitengeneza vitanda n.k alikuwa mwanadamu kweli na mungu kweli mimi nimeongelea kama mwanadamu..
 
Mke wangu ndio mtu wa muhimu kuliko wote maishani mwangu. niko tayari kumlinda na kumtetea kwa lolote hata kama amewakosea watu wengine etc. ila, siko tayari kufa kwaajili yake kwasababu Yesu peke yake ndo aliyekuwa na uwezo wa kufa kwaajili ya wengine. Mungu anatusaidia, hawezi kuwa tofauti wala hawezi kubadilika kwa lolote.

namtetea na kumpenda. mfano: yeye kama mwanamke wenye mapungufu kama walivyo wanawake wengine,hata kama atakuwa amewakosea kwa bahati mbaya majirani,rafikize au mtu yeyote, sitakubali mtu yeyote anyooshe mkono kumpiga, kumtukana, kumdhalilisha kwa lolote. anayeona waifu wangu ana matatizo anatakiwa aje aniambie mimi imrekebishe, kama hataki kuniambia mimi basi anyamaze kimyaaa aniachie waifu wangu. niko tayari kumlinda asiumie moyo ili sote tuishi maisha marefu,

nimemtetea na hakuna hata ndugu yeyote mwenye mamlaka ya kuingilia ndoa yetu, ndugu yeyote akitaka anichokoze basi aingilie ndoa yetu, amsema mke wangu vibaya au afanye lolote...awe dada yangu(wifi yake waifu), maza wangu au yeyote, mimi nilishajiunga kuwa mwili mmoja na wafu wangu, so anayemgusa yeye ananigusa mimi. However, wanaweza kutoa ushauri tu kwa busara na heshima nyingiiiii. out of that, watuache tu, byebye.

Maneno mazito sana haya nimerudia kuyasoma mara mbili. wanaume wote wangekuwa na msimamo huu ndoa zote zingedumu milele. be blessed
 
Jamani yesu alikuwa mwanadamu pia!!!!!!!!!! mbona mnakuwa wazito hivyo kuelewa? ndio maana alikula samaki, alitengeneza vitanda n.k alikuwa mwanadamu kweli na mungu kweli mimi nimeongelea kama mwanadamu..

tusibishane hapa, kama ndo hivyo, basi Yesu ndo wa muhimu kuliko wooote, hapo hata waifu akae pembeni...kwasababu Yesu atanipa uzima wa milele.
 
....nanyi si wawili tena bali ni mwili mmoja!

Ubavu wangu...alas yaani mke wangu mpenzi Ney!

HAPPY MOTHERS Day! to all Mama za watoto wetu wote!
 
[/B]

Swali lako limejifungafunga mno! ungeishia hapa..".MTU GANI NI MUHIMU KULIKO WOTE MAISHANI MWAKO??"..ningesema
ni Yesu Kristo..Lakini pia ulipoongeza hayo ya chini umenitoa hamu kabisa! kwani baba na mama wote wana 100% respectively.....
Wewe je, unaonaje nani muhimu kwako??

Niliongeza hayo maswali ili jibu liwe mwanadamu.....YESU ana nafasi yake.
Mwenye umuhimu kwangu kupitiliza ni mwanangu!!:rofl:
 
Jamani yesu alikuwa mwanadamu pia!!!!!!!!!! mbona mnakuwa wazito hivyo kuelewa? ndio maana alikula samaki, alitengeneza vitanda n.k alikuwa mwanadamu kweli na mungu kweli mimi nimeongelea kama mwanadamu..

Hata kama alikua mwanadamu sio sawa na sisi
 
Back
Top Bottom