Mtu mjinga ni yule anayenyang'anywa mali zake huku akicheka

Mr Why

JF-Expert Member
Nov 27, 2019
1,126
1,922
Mtu mjinga ni yule anayenyang'anywa mali huku akicheka pasipo kujiuliza kwanini amenyang'anywa.

Mtu mjinga anamiliki mali nyingi lakini anaruhusu mali hizo kuharibiwa na maadui na hata anaponyang'anywa kabisa basi yeye anabaki kuduwaa akitazama huku na kule pasipo kuchukua hatua kali kupigana kufa na kupona ili arejeshe mali alizonyang'anywa.

Wenzake wanaonyang'anywa mali kama yeye wanapomwamsha ili waunganishe nguvu na kuanza mapigano yeye anabaki akiduwaa tu.

Mtu mjinga anaruhusu mpaka wageni kuingia katika nyumba yake na kuanza kumtumia mke wake huku yeye akizidi kuduwaa na kusema kuwa anamwachia Mungu.

Mtu mjinga watamnyang'anya mali zake pamoja na mke wake yeye anakuwa tena kibaraka kwa wale waliomnyang'anya.
 
Back
Top Bottom