Mtoto wa Malecela amshukia Mukama

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
JUMAMOSI, JULAI 14, 2012 08:35

NA MWANDISHI WETU WA MTANZANIA,

DAR ES SALAAM


WILLIAM Malecela, mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, John Malecela, amemshukia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, akisema amepitwa na wakati na hana uwezo wa kuongoza chama hicho katika mazingira ya sasa.

Katika mchango wake katika mtandao wa jamii wa Jamii Forum, William alisema Mukama hawezi kukimbizana na siasa za sasa.

"Sina uhakika kama bado Mkama anaweza kukimbizana na siasa za sasa, kama ni kweli ameandika barua ya kujiuzulu then ingekuwa ni kwa sababu ya kukubali kupitwa na wakati wa modern politics, lakini siyo kwa sababu ya Nape.

"Haya ndiyo mambo niliyoyasema Mlimani TV, CCM ifike mahali ibadilike, iwe sawa na wananchi inaowaongoza maana so far haiko hivyo," alisema.

William, ambaye ni mjumbe wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam na CCM Wilaya ya Ilala, alisema kimsingi kazi anayoifanya Nape ni nzuri, ambayo ni kwa ajili ya chama na mwenyekiti pia.

"Nape ni kijana makini ambaye ni muhimu katika mkakati wa siasa, kwa sababu anafikiri haraka katika nafasi yake, na anaelewana na Januari Makamba. Wote wawili wanaweza kufikiri na kutoa majibu kwa haraka ambayo ni sauti, kitu ambacho ni kigumu sana kukipata ndani ya CCM, wengi wamekuwa na mazoea ya kusubiri mwenyekiti," alisema.

Mtoto huyo wa Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM Tanzania Bara, alisema chama hicho kinasumbuliwa na msongo wa uchaguzi wa mwaka 2005, lakini mpaka leo haujaisha na kukifanya kuwa makini katika mkakakati.

"Zile stress (msongo) bado hazijaisha na haukufanyika mkakakati makini baina ya wanachama kumaliza zile tofauti za kambi za uchaguzi, na pia ‘washikaji' waliomsaidia Rais wa sasa kuingia madarakani na kushindwa matarajio yao ya kufanya lolote wanalotaka kwa sababu tu ni washikaji," alisema.

William alisema masuala hayo mawili yamechangia kuleta matatizo makubwa ndani ya chama, ambako sasa imekuwa vuta nikuvute inayoishia kuwapa nafasi wapinzani kufaidika zaidi.

Hata hivyo, aliponda upinzani, akisema baadhi yao wameishia kuwa mawakala wa makundi ya ndani ya CCM, ambako wamekuwa wakihangaika kutafutia kura wagombea wa CCM, huku wakijua wazi kwamba wana wagombea wa vyama vyao, lakini wapo karibu na makundi ya CCM.

"Siamini hata kwa dakika kwamba Nape anajichukulia madaraka, lakini ninaamini kwamba anafanya kazi kwa muda na mazingira tulionao sasa, ambayo ni magumu sana kulinganisha na viongozi kama Mukama.

"Namaanisha hawa wote ni rafiki zangu wazuri, lakini kwa taarifa za hili gazeti siogopi kusema kwa sababu kama kweli unakipenda chama na kwa faida ya baadaye huwezi kusema kwamba Nape anakivuruga chama, labda kama una suala binafsi," alisema William.

Katika mtandao huo, William alisema tatizo la wanasiasa wakubwa wa Tanzania ni kwamba hawana washauri wanaofaa, wengi wamejijazia washauri waliopitwa na wakati.

Alisema anaunga mkono harakati za Nape kwa asilimia 100 kwa sababu anakisaidia chama na yeyote anayedai kwamba anakivuruga ina maana moja tu, hana nia njema na chama hicho.

"Nape anafanya kazi inavyotakiwa kama kufikiria kwa haraka na kutoa uamuzi mgumu bila kumsubiri mwenyekiti kwa kila kitu, ni lazima itakuwa inawaudhi baadhi ya waliozoea kukimbilia kwa Mwenyekiti kila wakati.

"Juzi nilikuwa kiwanjani kwenye mechi ya wabunge, nilikuwa karibu na kiongozi mmoja mkubwa wa CCM nikamwambia subiri Zitto na Nassari watakapotajwa kuingia uwanjani utaona kelele za wananchi, akaniuliza kwa nini, nikamjibu ni kwa sababu wanafanana na wananchi wengi waliopo hapa uwanjani.

"Wakati umefika wa CCM kuanza kubadilika ifanane na wananchi inaowaongoza, sina tabia ya kuzunguka mbuyu, viongozi kama Mkama wabaki nyuma kutoa ushauri lakini hatuwezi tena kuwa nao mbele katika sura ya chama wakati umepita," alisema William.

 
Wakulima na Wafanyakazi asilimia 90 bado wanafikira CCM bado ni CHAMA cha JEMBE na NYUNDO

Walakini Wakuu Wetu wa CCM sasa hivi na Washabiki wake wachache 5% ni Mabeberu wa kutupwa
 
Huyu mwana JF mwenzetu hana mshiko kabisa. Hivi anaijuwa siasa au anapayuka tu? aliwahi kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi kule NY?
 
Huyu mwana JF mwenzetu hana mshiko kabisa. Hivi anaijuwa siasa au anapayuka tu? aliwahi kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi kule NY?

Siku hizi kuna msemo kwamba "Amejipambanua" na nini? Sijui
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hapa naona kajiweka kwenye kundi fulani; Anajua Katibu Mkuu ni dhaifu na Nadhani kwenye pita pita yake kwa

wakubwa anasikia maneno yao jinsi wanavyomsema, kwahiyo yeye kwenda kwenye GAZETI na kumkosoa KATIBU MKUU

ni waridi wake wa kupanda ngazi kichama, kuna HABARI niliisoma humu kuwa KATIBU MKUU alitaka kujiuzulu sababu ya

kuingiliwa na NAPE... so kaka yetu MALECELA naona kaona upenyo....
 
Kaka Willy take care. Siasa sio rahisi kama unavyodhani japo faza wako alikuwa kwenye system.
 
Huyu mwana JF mwenzetu hana mshiko kabisa. Hivi anaijuwa siasa au anapayuka tu? aliwahi kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi kule NY?

Acha bana!!! huyu si @NY au umemsahau... ni mwenzetu bana... usiharibu.....au nitakushtaki vikaoni kwa manufaa ya chama chetu........ilisikika sauti kwa mbali ikijibu ....chama gani hiki cha Mabwepande ....nyingine ikajibu no, cha Magangster!!!:flypig:
:flypig::flypig::flypig::flypig:
 
- ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Le biig shoow jf stress sydrome, so the biig shoow is still on! Ha! Ha! Ha1

i am humbled sana you know!!


Le biig shoow!!

I did like some explanations on your presentation... and also about Nassari and Zitto...
 
haya bwana...!
naona media zimeanza kukuangalia na kukusikiliza....!

le big show
 
Haya W. J. Malecela safari ya kuelekea kwenye uchaguzi 2015 inapamba moto, sijui utakuwa Dar au Dodoma na ukiangukia pua 2015 ujue ni bora uende ukahangaike na mabox huko Brooklyn na ukiondoka umbebe na Nape.

2015 nchi inarudi kwa wenyewe wananchi sasa sijui nyie chama cha mafisadi mtajificha wapi
 
- ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Le biig shoow jf stress sydrome, so the biig shoow is still on! Ha! Ha! Ha1

i am humbled sana you know!!


Le biig shoow!!

Le Mutuz!

Japo nina kipinga kwa nguvu zote chama chenu, ktk gazeti kuna vitu baadhi umedhungumza ukweli mtupu hasa swala la Mukama kupitwa na wakati, hizi ni zama za dot com.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom