Elli
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 55,503
- 86,051
Ndugu wadau, nachukua fursa hii, kuwajulisha na kuwashukuru kwa mchango wenu wa kuandika Habari za mtoto Tuntufye Julius Mwakasaka.
Nikiwa kama mjomba wa Tuntufye na ambae nimeishi nae tangu kuzaliwa kwake, nawiwa kusema kua Tuntufye Julius Mwakasaka alitutoka tarehe 17 mwezi wa Pili 2010 kule KCMC Moshi ambapo alipelekwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake.
Mazishi yalifanyika Lushoto- Kialilo kwa bibi yake mzaa mama; Mwalimu Esther Mshana na baadae kilio kupelekwa Mbeya.
Tulimpenda sana, alikuwa Mcheshi na mtundu sana, alikuwa rafiki wa wote ( si kwa unafiki bali kwa hali halisi) Mchokozi ili kutafuta maana na urafiki lakini pia mpole kwa mambo ambayo alikose kama Mtoto. Ninampenda kwa Binasfi yangu.
Ameacha vilio na simanzi kwa wote ZAIDI AMEWAACHIA UPWEKE Ndugu zake; Tunosye na Alice. Nakumbuka sana maneno aliyoandika Tunosye ( 10) kwenye chumba chao wakati mdogo wake huyu anaumwa, maneno haya ambayo yalikuwa faraja kwangu na kwao yalisomeka hivi : TUNTUFYE IS OUR HERO huku mengine yakisomeka kwa kifupi tu Surprise pengine waliamini baada ya ndugu yao kuzunguka na kuhangaika huku na kule angerudi na kucheza nao na pengine kwao ingekuwa kama Surprise!!
Tunaamini ameenda kupumzika baada ya shida na mateso mengi aliyoyapata.
Taarifa zaidi na picha bofya hapa: http://servetanzaniacommunity.blogspot.com/2010/03/if-tomorrow-starts-without-me.html
Nawapenda wote sana na MUNGU AWABARIKI