Mtoto anakunywa maji kiasi cha kutisha

Nndu wa Selote

JF-Expert Member
Jun 21, 2012
733
520
Ni mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minane. Usiku analala usingizi wa vipindi vifupifupi huku kila mara anaposhtuka usingizini huomba maji. Anapopewa anakunywa glass nzima akimaliza analala kidogo. Baada ya muda kama saa moja huamka tena na kudai maji, mama yake akichelewa kidogo kumpa atashuka kitandani na kuanza kuyatafuta. Bado ananyonya sana tu. Je wataalamu hili laweza tatizo gani ?
 
Kama wazazi wana wasiwasi wajaribu kumuona daktari wa watoto. Kwa mtazamo wangu labda ni mazoea au wanaishi mazingira ya joto sana
 
Nenda hospitali muone daktari wa watoto halafu atakayokujibu usisahau kuja kutujulisha hapa.
 
Back
Top Bottom