Wakuu,
Nilipata fursa ya kuwasiliana na mtonyaji wetu ambaye ameseniambia kwamba Chadema tuwashukuru sana waandishi wa habari za Iringa na Tundu Lissu kwa sababu wameifanya serikali ishindwe cha kufanya katika sakata la Mwangosi.
Awali ya yote alisema Ifahamike kuwa;
Serikali haikutaka kabisa kumshtaki askari wake kwa kuwa hilo litawafanya Askari kupungukiwa na ujasiri wa kuwathibiti Chadema kwa hofu ya kushtakiwa mbele ya safari, na ndo maana walichelewa kuchukua hatua wakipisha upepo wa Mwangosi upite upepo ukagoma kupita hasa baada ya waandishi kuandamana. Hili jambo nalo lilizua mjadala wa ndani lakini mwisho ikalazimika walau kumshtaki.
Pili, Serikali kwa sasa haiko tayari kuunda tume ya uchunguzi ya kimahakama kama inatavyotakiwa kisheria na kama ilivyoombwa na Chadema, wanahabari, wananchi nk.
Nini kimeitatiza serikali?
Mosi, uundaji wa Tume ya kiuchunguzi wa kimahakama umekwama kwa sababu Majaji wote ambao wangeweza kuisaidia serikali endapo uchunguzi utaleta sura mbaya zaidi dhidi ya Serikali, wako ktk Listi ya Tundu Lissu. Hili ndilo tatizo kubwa sana. Tatizo kubwa ktk ripoti ile ya Lissu ni ripoti ya mapendekezo ya kamati ya Rais ya kuchunguza majaji ambayo iko mikononi mwa Tundu Lissu. Ripoti hiyo ilionesha kwamba majaji waliomaliza muda wao wakaongezewa muda na Rais ni kinyume na katiba ya nchi kama ilivyoelezwa na Lissu Bungeni kwa kujiamini ktk sakata lake. (Kumbuka utetezi wa tundu Lissu Bungeni). Hawa ndio walikuwa wawe tegemeo la Serikali ktk sakata hili na ndio hawateuliki kwa sababu itaanzisha mjadala wa Lissu na kuupanua zaidi.
Lengo lilikuwa ni tume ambayo uchunguzi wake usiiumize serikali badala yake uelekeze tuhuma kwa ama chadema au vurugu wananchi. Na pili, upendekeze kuundwa kwa sheria ya kudhibiti mienendo ya vyama vya siasa na hasa maandamano. Kwa hiyo, azimio lililopo ni kwamba Tume hiyo haitaundwa kwa kuwa serikali ina hofu kuchafuka zaidi.
Pili, sakata la Iringa kwa jinsi lilivyorekodiwa ktk kamera na picha zilizokwisha kurushwa ktk vyombo vya habari ni tatizo. Tatizo jingine kubwa ni hofu ya serikali kutojua vitu vilivyopo ktk kamera za waandishi wahusika kama vipo vilivyofichwa hadi sasa. Kwa hiyo, mambo haya (kama yapo yaliyofichwa) yakiletwa kwenye tume ya kimahakama yanaweza kuleta sura ambayo ingeshindikana kwa tume ya kimahakama kuisafisha serikali badala yake serikali ikaingia ktk tope kubwa zaidi bila kujali kama Tume inaongozwa na jaji wa aina gani (neutral au one sided).
Kwa hiyo, mambo mawili hapo juu yameiharibia kabisa serikali ktk mpango wake wa kuithibiti sakata hili na sasa tuko njia panda.
Na ni mambo hayo hayo ndo yalimfanya Rais ashindwe kuongea na wananchi kwa sababu hana cha kusema, jambo lililowafanya walazimike kumtuma Steven Wasira aje aongee kwa Niaba ya Rais kupunguza hasira za wananchi. Hata hivyo, wengi wanamlaumu Wasira huku serikali kwa madai kuwa heri asingeongea kwa kuwa hakufanikiwa kabisa kufanya kile alichotumwa. (Awali hotuba ya Wasiri ilikuwa aitoe Rais mwenyewe)
Nakumbuka kuliko na uzi wa Rais kuongea na waandishi humu JF kabla ya wasira kama sikosei.
Ushauri wake.
Chadema waendelee kudai Tume ya uchunguzi ya Kimahakama kwa kuwa tume ya Nchimbi ni danganya toto. Ina lengo la kuisafisha serikali. Upepo huo ukizidi serikali pengine inaweza kulazimika kuiunda tume hiyo bila kumhusisha jaji yo yote aliyetajwa na Lissu.
Pili, washukuruni sana waandishi majasiri wa Iringa walioweza kupiga picha matukio yale kwa uwazi kabisa na kuilazimisha serikali ilazimike kusema kweli na hoja ya Tundu Lissu kuhusu uwapo wa majaji wasiotambuliwa na katiba, vinginevyo mngechafuliwa sana na sheria husika kutungwa.
My take;
Hivi propaganda ya Mwangosi kupigwa na kitu kizito imeota mbawa?.
Hivi kama siyo Mungu, kwanini polisi walishindwa kuwazuia waandishi kurekodi tukio lile badala yake walichukua tukio lote wakaondoka na kamera zao Na sasa limekuwa kitanzi kwa serikali?
kwanza iliyoundwa na nchimbi si tume ni kamati (kichwa maji, kila siku unasahau) waziri hana mamlaka ya kuunda tume kikatiba, na kubwa kabisa kesi ipo mahakamani, lets waits and see.