Mtonyaji: CHADEMA mshukuruni Lissu na waandishi wa Habari sakata la Mwangosi vinginevyo...

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Wakuu,

Nilipata fursa ya kuwasiliana na mtonyaji wetu ambaye ameniambia kwamba Chadema tuwashukuru sana waandishi wa habari za Iringa na Tundu Lissu kwa sababu wameifanya serikali ishindwe kitu cha kufanya katika sakata la Mwangosi.
Awali ya yote alisema Ifahamike kuwa;

Serikali haikutaka kabisa kumshtaki askari wake kwa kuwa hilo litawafanya Askari kupungukiwa na ujasiri wa kuwathibiti Chadema kwa hofu ya kushtakiwa mbele ya safari, na ndo maana walichelewa kuchukua hatua wakipisha upepo wa Mwangosi upite – upepo ukagoma kupita hasa baada ya waandishi kuandamana. Hili jambo nalo lilizua mjadala wa ndani lakini mwisho ikalazimika walau kumshtaki.

Pili, Serikali kwa sasa haiko tayari kuunda tume ya uchunguzi ya kimahakama kama inatavyotakiwa kisheria na kama ilivyoombwa na Chadema, wanahabari, wananchi nk.

Nini kimeitatiza serikali?
Mosi, uundaji wa Tume ya kiuchunguzi wa kimahakama umekwama kwa sababu Majaji wote ambao wangeweza kuisaidia serikali endapo uchunguzi utaleta sura mbaya zaidi dhidi ya Serikali, wako ktk Listi ya Tundu Lissu. Hili ndilo tatizo kubwa sana. Tatizo kubwa ktk maelezo/utetezi wa Lissu ni Lissu kuwa na ripoti ya mapendekezo ya kamati ya Rais ya kuchunguza majaji walio kinyume na katiba. Ripoti hiyo ilionesha kwamba majaji waliomaliza muda wao wakaongezewa muda na Rais ni kinyume na katiba ya nchi kama ilivyoelezwa na Lissu Bungeni kwa kujiamini. (kisha Kumbuka maelezo ya utetezi wa tundu Lissu hapa JF). Hawa ndio walikuwa wawe tegemeo la Serikali ktk sakata hili na ndio hawateuliki kwa sababu itaanzisha mjadala wa Lissu na kuupanua zaidi.

Lengo lilikuwa ni tume ambayo uchunguzi wake usiiumize serikali badala yake uelekeze tuhuma kwa ama chadema au vurugu wananchi. Na pili, upendekeze kuundwa kwa sheria ya kudhibiti mienendo ya vyama vya siasa na hasa maandamano. Kwa hiyo, azimio lililopo ni kwamba Tume hiyo haitaundwa kwa kuwa serikali ina hofu ya kuchafuka zaidi.

Pili, sakata la Iringa kwa jinsi lilivyorekodiwa ktk kamera na picha zilizokwisha kurushwa ktk vyombo vya habari ni tatizo. Tatizo jingine kubwa ni hofu ya serikali kutojua vitu vilivyopo ktk kamera za waandishi wahusika kama zipo taarifa zilizofichwa hadi sasa. Kwa hiyo, mambo haya (kama yapo yaliyofichwa) yakiletwa kwenye tume ya kimahakama yanaweza kuleta sura ambayo ingeshindikana kwa tume ya kimahakama kuisafisha serikali badala yake serikali ikaingia ktk tope kubwa zaidi bila kujali kama Tume inaongozwa na jaji wa aina gani (neutral au one sided).

Kwa hiyo, mambo mawili hapo juu yameiharibia kabisa serikali ktk mpango wake wa kuithibiti sakata hili na sasa tuko njia panda.

Na ni mambo hayo hayo ndo yalimfanya Rais ashindwe kuongea na wananchi kwa sababu hana cha kusema, jambo lililowafanya walazimike kumtuma Steven Wasira aje aongee kwa Niaba ya Rais kupunguza hasira za wananchi. Hata hivyo, wengi wanamlaumu Wasira huku serikali kwa madai kuwa heri asingeongea kwa kuwa hakufanikiwa kabisa kufanya kile alichotumwa. (Awali hotuba ya Wasiri ilikuwa aitoe Rais mwenyewe)

Nakumbuka kulikuwa na uzi wa Rais kuongea na waandishi humu JF kabla ya wasira kama sikosei.


Ushauri wake:
Chadema waendelee kudai Tume ya uchunguzi ya Kimahakama kwa kuwa tume ya Nchimbi aka kamati ya Nchimbi ni danganya toto. Ina lengo la kuisafisha serikali. Upepo huo ukizidi serikali pengine inaweza kulazimika kuiunda tume hiyo bila kumhusisha jaji yo yote aliyetajwa na Lissu.

Pili, washukuruni sana waandishi majasiri wa Iringa walioweza kupiga picha matukio yale kwa uwazi kabisa na kuilazimisha serikali isema kweli bila kusahau hoja ya Tundu Lissu kuhusu uwapo wa majaji wasiotambuliwa na katiba, vinginevyo mngechafuliwa sana na sheria husika kutungwa.

My take:
Hivi propaganda ya Mwangosi kupigwa na kitu kizito imeota mbawa?

Hivi kama siyo Mungu, kwanini polisi walishindwa kuwazuia waandishi kurekodi tukio lile badala yake walichukua tukio lote wakaondoka na kamera zao Na sasa limekuwa kitanzi kwa serikali?


FREEMAN MBOWE; WAO WANA RISASI NA MABOMU SISI TUNA MUNGU.
 
Kwa hili la kifo cha Mwangosi, serikali ya CCM hata ikitumia mkorogo au corolite ya aina gani haitaweza kamwe kupendeza mbele ya watanzania.
 
Safii safi sanaaa!!

Watanzania tutumie nafasi na usomi wetu kutetea haki za wanyonge.

Watawala wana pesa na nguvu lakini sisi tuna akili na Mungu, ni lazima tutashinda tu.
 
Tume juu ya Tume na aliyeundiwa Tume nae anasema ataunda Tume, kabla Tume ahaijabainisha yaliyojiri kwenye Tume ya Polisi ya Kudhibiti CDM, yule aliyepaswa kuhojiwa amepandishwa kizimbani ili waseme sasa mkae kimya kwa kuwa jambo mnalolilalamikia lipo Mahakamani!!

390487_180553948747468_1690226419_n.jpg
 
kunamitanzania mingine imerogwa na ccm, jana nimesafiri safari ndefu Zenji hadi Kahama,huku kunamijitu inasema chadema ndo wamemuua muandishi
 
IF GOD IS WITH US WHO CAN BE AGAINST US!
Might is not neccessarily right; But right is devine; it will always prevail, whereas MIGHT which often times is susceptible to abuse is evil and will fail.
 
IF GOD IS WITH US WHO CAN BE AGAINST US!
Might is not neccessarily right; But right is devine; it will always prevail, whereas MIGHT which often times is susceptible to abuse is evil and will fail.
 
namuomba mungu aepushe kadhia hii huko tuendako katika tanzania yetu tuipendayo
 
Aweda,ukiwa kama mjumbe wa baraza kuu la Chadema,mutawasaidiaje watu waliokamatwa Nyololo kutokana na vurugu zilizotokea wakati wa ufunguzi wa Tawi la Chadema na kufunguliwa kesi Mafinga? Kuna gari lilikodiwa kusafirisha wanaM4C kutoka Mbeya kwenda Nyololo kwenye ufunguzi huo,lakini wakati linarudi kwenda Mbeya lilikamatwa Igawa na kurudishwa Mafinga ambako ndiko kuna kesi.

Dereva na kondakta wa gari hilo waliwekwa ndani kwa siku kadhaa na sasa hivi wamefunguliwa kesi ya kushiriki katika vurugu hizo!Kumbuka wao walikodiwa tu kusafirisha abiria ambao ni wanaM4C. Mheshimiwa Mbilinyi(a.k.a Mr Sugu) funguka kuhusu issue hii. Namba yako 0716...344 haipatikani!
 
Tumeshindwa kila kitu..., ukiachia wizi wa mali za umma tunachoweza ni kuunda tume. Maji machafu wanatiririka barabarani,naunda tume! Mbuzi amekula ktk shamba la mkulima, NAUNDA TUME! Ni tume juu ya tume ktkat ya tume pembeni ya tume
 
Wakuu,

Ushauri wake.
1) Chadema waendelee kudai Tume ya uchunguzi ya Kimahakama kwa kuwa tume ya Nchimbi ni danganya toto. Ina lengo la kuisafisha serikali. Upepo huo ukizidi serikali pengine inaweza kulazimika kuiunda tume hiyo bila kumhusisha jaji yo yote aliyetajwa na Lissu.

2) W
ashukuruni sana waandishi majasiri wa Iringa walioweza kupiga picha matukio yale kwa uwazi kabisa na kuilazimisha serikali ilazimike kusema kweli na hoja ya Tundu Lissu kuhusu uwapo wa majaji wasiotambuliwa na katiba, vinginevyo mngechafuliwa sana na sheria husika kutungwa.

My take;
Hivi kama siyo Mungu, kwanini polisi walishindwa kuwazuia waandishi kurekodi tukio lile badala yake walichukua tukio lote wakaondoka na kamera zao Na sasa limekuwa kitanzi kwa serikali?

Michael kwa mara nyingine tena asante sana.

Naunga mkono, sana tu, hoja ya kwanza 110%.

Hoja ya pili, ni kweli kabisa waandishi wale ukianzia na Mwangosi mwenyewe walikuwa na ujasiri wa ajabu. Ndiposa naunganisha na hoja yako KAMA SIO MUNGU...! Kwa wengi wetu ni mkono na mpango wa Mungu kuwa CCM na vibaraka walikuwa waumbuke hadharani big time. Nazidi kuwapa hongera nyingi sana wale waandishi; kwa heshima niwataje mashujaa wetu wa Iringa:-

1) Daudi Mwangosi (R.I.P.) - Channel 10, huyu ndiye aliyebeba (epitomise) ujasiri na umahiri wa kipekee ktk matukio yote ya siku ya kifo chake.
2) Abdallah Khamis - Tanzania Daima
3) Godfrey Mushi - Nipashe
4) Clement Sanga - Mwananchi
5) F. Godwin - kujitegemea (?)
6) Joseph Assenga - Tanzania Daima
7) Renatus Mtabuzi - ITV

Heshima kwenu wazalendo wetu, majina yenu nimeyaandika kwa wino wa dhahabu.
 
Aweda,ukiwa kama mjumbe wa baraza kuu la Chadema,mutawasaidiaje watu waliokamatwa Nyololo kutokana na vurugu zilizotokea wakati wa ufunguzi wa Tawi la Chadema na kufunguliwa kesi Mafinga? Kuna gari lilikodiwa kusafirisha wanaM4C kutoka Mbeya kwenda Nyololo kwenye ufunguzi huo,lakini wakati linarudi kwenda Mbeya lilikamatwa Igawa na kurudishwa Mafinga ambako ndiko kuna kesi.

Dereva na kondakta wa gari hilo waliwekwa ndani kwa siku kadhaa na sasa hivi wamefunguliwa kesi ya kushiriki katika vurugu hizo!Kumbuka wao walikodiwa tu kusafirisha abiria ambao ni wanaM4C. Mheshimiwa Mbilinyi(a.k.a Mr Sugu) funguka kuhusu issue hii. Namba yako 0716...344 haipatikani!

Mkuu hizi habari ndo napata kwako.
Lakini hopefully viongozi wetu wa ngazi ya wilaya na mkoa na hata Taifa hawawezi kukaa kimya. Nitawataarifu wahusika. Hatulali mkuu.

 
Michael kwa mara nyingine tena asante sana.

Naunga mkono, sana tu, hoja ya kwanza 110%.

Hoja ya pili, ni kweli kabisa waandishi wale ukianzia na Mwangosi mwenyewe walikuwa na ujasiri wa ajabu. Ndiposa naunganisha na hoja yako KAMA SIO MUNGU...! Kwa wengi wetu ni mkono na mpango wa Mungu kuwa CCM na vibaraka walikuwa waumbuke hadharani big time. Nazidi kuwapo hongera nyingi sana wale waandishi; kwa heshima niwataje mashujaa wetu wa Iringa:-

1) Daudi Mwangosi (R.I.P.) - aliyebeba ujasiri na umahiri wa kipekee ktk matukio yote ya siku ya kifo chake.
2) Khamis Abdallah - Tanzania Daima
3) J. Mushi - Nipashe
4) Sanga - ?
5) F. Godwin - kujitegemea
6) Assenga - ?

Heshima kwenu wazalendo wetu.

Juzi kwenye maandamano ya Waandishi wa habari nilisikia tamko la kutaka Jeshi la Polisi warudishe Video Camera na Laptop za Marehemu Mwangosi.Je. zimesharudishwa? Kama hazijarudishwa ziko wapi na kwanini Polisi hawataki kuziachia?????

 
Back
Top Bottom