Mtikila kufungua kesi kudai Tanganyika

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
MWENYEKITI wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, anakusudia kufungua kesi mpya katika Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika iliyoko Arusha, kudai serikali ya Tanganyika.

Mchungaji Mtikila aliyasema hayo jana mjini hapa, mara baada ya kuahirishwa kwa kesi aliyoifungua katika mahakama hiyo kudai uwepo wa mgombea binafsi.

Mtikila alisema kuwa kutokana na imani kubwa aliyonayo kwa mahakama hiyo, ana imani haki aliyokua akiitafuta kwa muda mrefu sasa iko mbioni kupatikana.

Alifafanua kuwa katika kufungua kesi hiyo ya kudai Tanganyika, kuna wanasheria kutoka Nigeria wako tayari kuja kusimamia katika kesi hiyo ambayo alidai itakuwa ni ukombozi kwa Watanganyika wote.

Aidha alisema kuwa wakati yeye anakusudia kufungua kesi hiyo tayari ana taarifa za kuwepo kwa baadhi ya Wazanzibari wanakusudia kufungua kesi katika mahakama hiyo kupinga muungano.

Awali katika mahakama hiyo, kesi iliyoanza kusikilizwa juzi na mahakama hiyo juu ya hoja ya mgombea binafsi iliyofunguliwa na Mtikila pamoja na kituo cha msaada wa sheria na haki za binadamu mara baada ya kusikilizwa hoja za pande zote mbili iliahishwa.

Kesi hiyo inayosikilizwa na majaji tisa kati ya 10 wa mahakama hiyo iliahirishwa hadi baada ya siku 90 ambapo itakuja kutolewa hukumu kutokana na pande zote mbili kukamilisha ushahidi wao.

Katika kuwasilisha maelezo ya mwisho na kujibu maswali yaliyotolewa na majaji wa mahakama hiyo, upande wa Mtikila uliiomba mahakama hiyo itamke kuwa na haki kuwepo na mgombea binafsi katika chaguzi zote za kisiasa hapa nchini.

Aidha kupitia kwa wanasheria James Jesse, Clement Mashamba, Donald Deye na Profesa Lajovi waliiomba mahakama hiyo pia iiamuru serikali ya Tanzania kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Jaji Elsien Thompson alimuuliza Mtikila ni kwa nini anataka kuwepo kwa mgombea binafsi wakati yeye tayari ana chama chake kinachomuwezesha kupata fursa ya kugombea.

Kupitia mawakili wake, Mtikila alijibu kuwa kutokana na kuwepo na taratibu ngumu za uidhinishwaji wa vyama kuruhusiwa kusimamisha wagombea, imepelekea mteja wao kushindwa kupata haki hiyo.


Mie naunga mkono na mguu
Source T. Daima
 
hoja ya kupinga mgombea binafsi ni ya magamba na lengo lake ni kuzuia watakaobaniwa ndani ya chama kutopata nafasi ya kugombea wao kama wao kwani wanajua hii itapeleka chama kupasuka sana kwani kila mtu atakua anaondoka na watu wake...

ila ni kitu cha maana sana kwa maslahi ya nchi
 
Back
Top Bottom