Mtikila ashinda tena kesi ya mgombea huru; Afungua upya Mahakama ya Afrika Mashariki

MKJJ,
Am looking at it positively.
Mtikila ni mtu asiyeogopa kusimamia na kutetea kile anachoamini; na nadhani ndo maana wanamtumia kama ni kweli wanamtumia. All they have to do is to point out the unconstitutional issue and assure him of the available remedies then make it possible for him to make his way to court.
Hii inampa credit Mtikila; but the coward guys sits back and wait for the outcome.
Na kama hivi ndivyo basi pana hatari hapa: wale wenye sababu ambazo sio za kujenga nchi nao wanaweza kujaribu kumtumia, na kama akifikia mahali akalewa na hako katabia..theres no limit to the extent to which he can go
 
Mzee Mwanakijiji,

Mimi naweza kuamini kabisa kwa sababu hata Seif Sharrif Hamad wa Zanzibar ni mtumiwaji ambaye yupo kubabaisha wananchi. Na kweli kafungwa sana Jela lakini wakati huo huo ni tajiri mkubwa sana...
Ndio maana matumaini yangu makubwa yapo kwa Freeman (as a leader)kama kweli amesimama kutetea haki za wanyonge
 
jamani i know mtikila ,he is just poor like any tanzania..ila ana convincing power ,wakati tupo versity baadhi yetu walikuwa wakijitolea kuuza kanda za mtikila chuoni na tulizinunua na kusikiliza kwa siri vyumbani ,hiyo ilikuwa 1992..waliokuwa wakimsaidia walikuwa hawalipwi chochote.
mtikila ni mtanganyika tu anayeishi kwenye apartment ya room2 pale ilala na hana hata gari ..lalikuwa na 504,na benz old model zipo juu ya mawe hata kabla ya mageuzi...hata wapambe wanaomfuata hawalipi kama unavyozani wengi wanajitolea tu...hata mawakili wengi hujitolea na kiukweli mawakili hupenda kesi za mtikila kwa sababu nyingi wanashinda na zinawasaidia kuwajenga jina.ndio maana kila siku mtikila anapata wakili mpya ,kila mtu anataka kuwa wakili wake ,baada ya kupata uwakili ili afahamike.

mtikila ni mtu aliyejitolea maisha yake.
 
Phillemon mikael,

Duuuh! kama ndio hivyo narudisha mfukoni mchango wangu wa awali!...
Lakini kitu kimoja tu, siasa ni mchezo mchafu na vizuri sana awe anajipanga kabla ya kutoa maoni yake. Ile kuomba ruzuku kusema kweli sasa naelewa mwenzetu katoka wapi! - NJAA jamani adui mkubwa wa haki!
 
Mkandara, I like that too.. rushwa siyo adui wa haki.. njaa ndiyo adui wa haki kwani inasababisha rushwa!!!
 
Mkandara,
Mtikila aliomba ruzuku strategically. Alichokusudia ni kumetega JK akubali ofa hiyo, ili ijustify madai ya upinzani kuwa ameshinda kwa kuiba kura.

Na JK naye akaingia kwenye 18 za Mtikali kwa kukubali hilo deal la ruzuku.

Kazi kwelikweli, msikilize Mtikila vizuri akizungumzia suala hili, then you'll know what am talking about.
 
Zinduka,
Hizi habari umezipata wapi tena na kiasi gani tunaweza kuziamini!...
Ndugu yangu Mtikila kwa jinsi nilivyosimuliwa hapa najua kabisa kipi kimemsukuma - NJAA
Haiwezekani kumwandikia RAIS wa nchi barua yenye mchezo wa mtaani! tena ukitumia haki inayokupa sauti na nguvu ya kuweka madai. JK angeweza kabisa kumtega Mtikila kuliko Mtikila mwenyewe kwa sababu Mtikila alisha jifunga mwenyewe kwa maandishi kukubali kufuta madai.
Wrong political move!
 
kweli askofu mtikila ni mwana mapambano. ana vyanzo vyake vya habari amabvyo vinampa taarifa za kiuhakika husimamia kile anachoamini kwamba ni haki ya watanganyika.
kitu kinachonitatiza ni kwamba sioni mtu mwingine ndani ya chama chake ambaye ni mwanamapambano kama yeye (au ndio maana anapigania mgombea binafsi). kutokuwepo/kutojulikana kwa viongozi wengine ndani ya chama inaweza kuashiria mkakati wa kiongozi wa chama kuwazima wengine (udikteta?), viongozi wengine ni waoga hivyo wanamuachia mwenyekiti mikikimikiki au wananchi wenye uwezo wanaogopa kujiunga na kujitokeza kwani wanaweza mulikwa na kushughulikiwa.
kama kuna mwenye kufahamu kwanini mtikila "anajulikana" peke yake atueleze.
ni mawazo yangu tuu
 
mtikila anaendesha siasa katika mazingira magumu,..hana pesa kama nilivyosema lakini pia kunakitu kingine kwa ntikila yeye ni MASIKINI JEURI kwa maana nyingine hanunuliki ,hii pia inatokana na msimamo wake kiimani...so msitegemee kuwa njaa itamfanya akengehuke....
miaka ile ya mwanzo ya upinzani alivyowaandama wahindi NA ILE SERA YA MAGABACHOLI ,jumuia za wahindi na jamaat zao walikusanya pesa ili wampelekee aache kelele ALIZITOLEA NJE...TENA wakati anakataa hiyo pesa kuna nyumba yake gofu nafikiri ipo mikocheni [sijui kama bado ipo]aliijenga tangu mwanzo wa miaka ya 1980 na haijaisha ,ilikuwa inataka kupigwa mnada kufidia madeni ya ujenzi still hawakumpata na sijui kama walijikwamua na lile deni...
 
Ushuri huu umetoka kwa watanzania waishio marekani kumuomba REV.MTIKILA kujiunga humu JAMBOFORUMS ili kuchangia mawazo waTZ wasomi waishio nje zanchi.

Ombi hili tunaomba watanzania waliopo nyumbani basi kuhabarisha kwa mchango wake ni muhimu sana kwa taifa letu

mchungaji amekuwa mstari wa mbele kuwe mambo sawa muda hote wa maisha yake akianzia kwenye imani ya dini mpaka serikalini na kwa wananchi kwa ujumla,

mchungaji ameonekana katika miono mbalimbali lakini wengi hawakujua ni mkombozi wa wanyonge sisi wote ambao ni wadau wavyama mbalimbli tumegundua wanao tendewa haki ni wachache nao ni makada tu,

sasa kwa wale walio karibu na mchungaji basi au katibu wake au msaidiazi wake basi tunaoma wamuhabarishe wananchi wana muhitaji humu JF kwa mchango wake mkubwa kwa taifa letu

viongozi wengi wa kitaifa wamo humu JF pia yeye anakaribishwa sana

mungu amlinde ampe nguvu maisha marefu alunta kontinua amen
 
I think he still use the contacts below;

Mchikichini Ilala
P.O Box 63102 DSM
Tel:0741 -430516 ; 0741 - 625349 {Update the codes b4 calling}

Interested person(s) may envite him to JF.
 
I think he still use the contacts below;

Mchikichini Ilala
P.O Box 63102 DSM
Tel:0741 -430516 ; 0741 - 625349 {Update the codes b4 calling}

Interested person(s) may envite him to JF.

Codes 0741have been replaced by 0713

JUST FOR QUICK REF.
 
Wazo ni zuri lakini Je hawatajitokeza kumtukana?

Au KUSEMA AAAAAAAAHH MTIKILA KAJIMALIZA KISIASA NK!!
 
Wazo ni zuri lakini Je hawatajitokeza kumtukana?

Au KUSEMA AAAAAAAAHH MTIKILA KAJIMALIZA KISIASA NK!!
Mbona mtikila yumo humu? au mnapenda atumie jina lake halisi?

Hata hivyo amepitwa na wakati na tayari amefilisika kisiasa, enzi zake zilikuwa miaka 15 iliyopita sio sasa.
 
Mbona mtikila yumo humu? au mnapenda atumie jina lake halisi?

Hata hivyo amepitwa na wakati na tayari amefilisika kisiasa, enzi zake zilikuwa miaka 15 iliyopita sio sasa.

Kakalende,

In which 'political world' are you living in??
 
Ndiyo maana Mkira kauliza hamtamtukana ? Maana kabla ya jibu kesha tukanwa .Yaani Mtikila kesha isha kisiasa Kakalende are you out of your mind ?
 
Labda Kakalende anamaanisha nini hasa akisema " amefilisika kisiasa"? Siku hizi kila tukimsikia yupo Mahakamani, na mara nyingi anashinda, lakini sina uhakika na success ya mahakamani na uhusiano wa career yake ya siasa.
 
Ushuri huu umetoka kwa watanzania waishio marekani kumuomba REV.MTIKILA kujiunga humu JAMBOFORUMS ili kuchangia mawazo waTZ wasomi waishio nje zanchi.

Ombi hili tunaomba watanzania waliopo nyumbani basi kuhabarisha kwa mchango wake ni muhimu sana kwa taifa letu

mchungaji amekuwa mstari wa mbele kuwe mambo sawa muda hote wa maisha yake akianzia kwenye imani ya dini mpaka serikalini na kwa wananchi kwa ujumla,

mchungaji ameonekana katika miono mbalimbali lakini wengi hawakujua ni mkombozi wa wanyonge sisi wote ambao ni wadau wavyama mbalimbli tumegundua wanao tendewa haki ni wachache nao ni makada tu,

sasa kwa wale walio karibu na mchungaji basi au katibu wake au msaidiazi wake basi tunaoma wamuhabarishe wananchi wana muhitaji humu JF kwa mchango wake mkubwa kwa taifa letu

viongozi wengi wa kitaifa wamo humu JF pia yeye anakaribishwa sana

mungu amlinde ampe nguvu maisha marefu alunta kontinua amen

Watu wasiomjua Mtikila, wanaomsoma magazetini, hasa kuhusu kesi zake mahakamani ndio wanaomtamani! Mimi si mmojawapo.

Uongo mbaya. Panapomfaa Mtikila ni huko aliko. Katika mengine, hana jipya, anazungusha yale yale tu, tuliyokwishachoka, au ambayo wenye akili wanayajadili kwa kujenga hoja, yeye kwa matusi.

Kama unamtaka Mtikila kutana naye ana kwa ana...Mtafute; mchungaji mwenye chama bila wanachama, lakini machachari mahakamani. Tumpe haki yake, mahakamani amepaweza kuliko jukwaani.
 
Sidhani kama kuna Ubaya wa kuwaalika akina Mtikila kuja humu lakini kwanza tuanze kwa kupeana heshima humu ndani

Tuache tabia za kuwatukana watu kwa sababu wanafanya kazi serikalia u ni CCM

nadhani we can do beter than petty politics ambazo kila kukicha tunazisoma kwenye magazeti ya Bongo
 
Back
Top Bottom