Mtikila ashinda tena kesi ya mgombea huru; Afungua upya Mahakama ya Afrika Mashariki

sikumuuliza hilo la yeye kugombea Urais.. lakini ilo jingine nimemuuliza na mambo mengi yanayohusu sheria na katiba yetu..
 
Kuunganisha Vyama ni kitu kigumu na shida ni sera za Vyama . Pia Uongozi na mambo mengine .Wacha kwanza tungoje matangazo kabla hatujaanza kuchambua mambo hapa .
 
Pia kwa nini wagombea urais ni wale wale toka 1995?...isipokuwa Chadema kwa nini wasiwape nafasi watu wengine wao wakabaki pembeni kama JM na CCM.

Mwanakijiji,
Mtikila kaniacha hoi pale aliposema kuwa alimwandikia barua JK, hasa pale alipodai wapewe RUZUKU kisha wao watasahahu madai yote!...
Damn....yaani hapa tumbo lao bora kuliko haki ya wananchi hata kama tuliibiwa.
 
Sasa mwanakijiji, kabla sijasikiliza hiyo interview, mbona hujatualika tukupe maoni mengine ya maswali ya kumhoji? Kwa mfano kama angepewa vielelezo vyote the IPTL scandal hangeweza kusaidia kuwabana hawa walaji mahakamani? Au tu atumia mbinu zake kufanya probe.
 
IO.. kwenye mahojiano haya niliyawekea mipaka ya kuzungumzia masuala ya Katiba na kesi ambazo amekuwa akizileta mara kwa mara. Next time bila ya shaka tutapanga kuzungumzia mambo mengine..
 
niliyasikiliza mahojiano ,mtikila hajaacha moto wake ...it is very interesting ,nampongeza mjj kwa kumpa air time
 
Kiu niliyo nayo ni kutaka kuona Mtikila anafungua kesi ya kudai mali yetu sisi kama watanzania ambayo CCM imegeuza kuwa Miradi yake.Kwanini wakati wanaingia mfumo wa vyama vingi resources za chama kimoja kwanini hazikuwa analyesed?
By the way, Bravo Mkjj kwa kuwasiliana na Mtikila
 
Ndugu zanguni wana JF
kwanza naanza kwa kutoa pongezi kubwa sana kwa Mzee MKJJ. Huyu kwa mara ya kwanza kafanya mahojiano mazuri saana . Mzee MKJJ umebadilika na sasa unajua unacho kifanya . Hongera na usikate tamaa .Nimependa maswali yako na mtiririko wa maongezi yako na ulivyo kuwa unamchomekea Mchungaji.HONGERAAAAAAAAAAAAAAA

Sasa baada ya kumsikia Mchungaji naomba sana kutoa wazo . Kwa kuwa wana JF wengi mnapenda kuandika hapa lakini waoga hata wa kuchukua Jimbo moja na muanze kujipanga basi tumoe support Mtikila . Support ya kila namna kuanzia data , Malalamiko yetu na hata pesa kwa ajili ya kesi Mahakamni.

Tuache kuandila hapa tuu .Tumpe nguvu huyu Mzee maana anafanya kazi ambayo Watanzania wote wanaiona kwamba ni hatari kwa kuwa wamezoea kukaa na watoto wao na kunywa bia nk lakini Mchungaji yeye anapasuka kichwa na kuishia Mahakamani.

Wana JF tunaweza kuwasiliana wenyewe na kujipanga na kuamua tumpe vipi support maana yeye issues zake za mahakamani zinatugusa sote na ndiyo huwa tunaziongelea hapa lakini hakuna wa kuanza kutafuta suluhu ama Mahakamani ama popote pale .

Naomba kuwasilisha kwamba Tumpe Mchungaji msaada tuache bla bla bla . Ana kesi 13 na chache sana ni zake personal lakini zingine sote ni kwa ajili ya ama Katiba ama kutetea haki ya Mtanzania .
 
Mkjj ahsante sana kwa kutuletea mahojiano haya na Askofu Mtikila. Ni kweli kabisa kwamba askofu huyu ana nia nzuri ya kuibadilisha na kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye shida mbalimbali zinazotukabili kwa kutumia katiba yetu wenyewe tofauti kabisa na wababaishaji wengine. Haleluya ndugu Mtikila!!
 
Nachotaka kujua mimi, ni kwa nini alimwandikia barua JK kudai walepwe RUZUKU zao ili wa-drop madai?...
Je, haya madai ni kwa maslahi yake, chama au wananchi?
 
Lakini pamoja na mazuri yote ambayo huyo mzee amelifanyia taifa letu, bado anaonekana ni mbabaishaji. Lakini wababaishaji kama kina Marando, Mrema, Ngawaiya na wengineo wanazidi kupeta tu.
 
Mafuchila.... kama kuna mtu ambaye amekuwa ishara ya mgongano (sign of contradiction) ni Askofu Mtikila. Kama nilivyosema kwa wengine ni mtu ambaye ametetea sana maslahi ya Tanzania kwa kupitia Katiba lakini wakati huo huo ameonekana kama Mwehu kutokana na maneno yake makali. Katika yote ya yote hata hivyo.. anasimama katika kundi la peke yake kati ya wapinzani Tanzania.

Lunyungu asante... nitajitahidi kujiandaa zaidi na kuwa na kujiamini zaidi....
 
Ni kweli kabisa Mwanakijiji,
ukiondoa maneno yake Rev. ni mtu wa vitendo na kwa kiwango kikubwa amesaidia sana mchakato mzima wa demokrasia Tanzania, kuliko wanasiasa wengine ambao wana wajibu huo kwa kiasi kikubwa, kwani wanapokea ruzuku kila mwezi ambayo ni pesa ya walipa kodi.
 
Mzee Mkandara
Inaonyesha hawatu woye wababaishaji tu Vipi aombe ruzuku halafu aache madai yake ambayo eti kwa madai yake anawatetea waTz,sasa
uongozi wa mtu kama huyu ndio tunaoutaka?mimi naona huyu mtu ni sawa na SIMBA WA ZOO, ni bora arudi kwa bwana.
 
Naomba niseme hili with caution and a lot of respect for all.
Nimekuwa nasita sana kuongelea suala la Mtikila kwasababu ya tetesi nilizowahi kuzisikia mtaani; kwamba kesi nyingi anazofungua Mtikila anafanya hivyo kwa kuombwa kutumia jina lake: yaani wako watu ambao kwa sababu za usalama wa kazi zao au vinginevyo, wanaogopa kutumia majina yao kufungua kesi za jinsi hiyo. Kwa kufahamu kuwa Mtikila ni dare-devil, wanamfuata, wanamweleza, wanaweka wazi kuwa wanaandaa madai na kulipa wanasheria, ilimradi tu yeye aonekane kuwa ndo mwenye kesi. Na inadaiwa kuwa ndivyo inavyotokea.

Nimekaa kimya nikijaribu kutafuta ukweli wa madai haya, bado sijafanikiwa; naleta hapa JF ili kama kuna aliyewahi kusikia hilo nae atuambie
 
Mwendapole... kama unayosema ni kweli, inaonesha ni jinsi gani Mtikila alivyohuru..lakini ni mtu atakayekubali kufungwa jela mara 25 ili kuwafurahisa watu wachache kama yeye mwenye haamini yale anayoyatetea?
 
Back
Top Bottom