The Dreamer
JF-Expert Member
- Feb 2, 2009
- 1,282
- 20
Kama huyu jamaa amepewa kazi rasmi ya kuzusha majungu hapa CCM wamechemka. Maana jamaa anajua kutembeza kalamu lakini siyo kujenga hoja. Hakuna mahali popote alipotoa ushahidi kulinda hoja zake bali anajaribu kuunganisha mambo na matukio yasiyo na uhusiano. Kwa mfano hakuna popote anapoonyesha kwamba kweli Nyerere alikuwa na chuki na Mtei. Angewezaje basi amfanye Gavana wa Benki Kuu, Katibu Mkuu, Waziri, Katibu Mkuu wa EAC na baadaye (baada ya kuacha Ugavana) kumfanya mwakilishi wa Kanda ya Afrika kwenye IMF? Kwangu hii inaonyesha imani badala ya chuki. Ni watu wajinga sana wanaoweza kuamini upuuzi wake.
Mtu mjinga hawezi kujua contradiction ipo wapi...anaangaika tu kuunganisha ili na lile na kujenga sababu kama vile za ajira ya Mtei iliwezekana kwa vile hawakuwepo wasomi (This is a credit to Mtei, by the way)